Kuangushwa kwa mawaziri na manaibu waziri tumepata somo?

Jang Bo Go

JF-Expert Member
Oct 22, 2011
854
250
Habari wadau

Mawaziri wa Jakaya Kikwete wamezidi kuangukia pua katika uchaguzi unaoendelea.

Baadhi ya waliokumbwa na dhahama hiyo ni Wassira, Chiza, Mwanri, Nundu, Kilango na Zambi..

Hata walioshinda ni kibahati nasibu mfano Mwakyembe.

Je Watanzania wenzangu tunapata somo gani hapa? Na tutegemee jipya gani kwa baraza jipya litakaloundwa na either Magufuli au Lowasa?
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,743
2,000
Hii inatoa picha sahihi kuwa serikali ya Kikwete ilikuwa mbovu kuliko maelezo kwani haijawahi tokea mawaziri wengi hivyo kuangushwa katika Uchaguzi mkuu na wengi pia waliangushwa katika kura za maoni.
 
Kwa ufupi inaonyesha nchi ilikua inaendeshwa bila mawaziri.
 
Jang Bo Go

JF-Expert Member
Oct 22, 2011
854
250
Me nafikir wananchi wameamua kuvunja baraza la mawaziri wenyewe,ni kitu kizuri pia maana raisi kashindwa

Wananchi wanavunja baraza ila dalili zinaonyesha Makufuli atashinda na baadhi ya walioshindwa watapewa kazi. Tutegemee hali ile ile kujirudia after five years?
 
mtebetini

JF-Expert Member
Jul 5, 2015
1,889
2,000
Habari wadau

Mawaziri wa Jakaya Kikwete wamezidi kuangukia pua katika uchaguzi unaoendelea.

Baadhi ya waliokumbwa na dhahama hiyo ni Wassira, Chiza, Mwanri, Nundu, Kilango na Zambi..

Hata walioshinda ni kibahati nasibu mfano Mwakyembe.

Je Watanzania wenzangu tunapata somo gani hapa? Na tutegemee jipya gani kwa baraza jipya litakaloundwa na either Magufuli au Lowasa?

Mkuu nadhani niongeze kidogo kwenye bandiko lako mpaka sasa waliokuwa bado mawaziri na wameshindwa ni pamoja na Mhe Steven Kebwe na ambao walikuwa mawaziri na waliondoka kwa sababu mbali mbali ni Mhe Kagasheki,Mhe Gaudes Kabaka,Mhe Makongoro Mahanga,Mhe Cyril Chami,Mhe Adam Malima,Mhe Dr Seif. Mhe Prof. Kapuya
,Mhe Amos Makala.
Kwangu somo ni kuwa kumbe umma ndiyo wenyewe nguvu ya maamuzi kuwaweka viongozi kwenye nafasi hizo na lingine kuwa umma unahitajika upewe Elimu zaidi ya nguvu walionayo.
Kwa Baraza jipya wagombea walituahidi kwenye kampeni muundo wa serikali utakuwaje tusubiri tuone ahadi walizotoa watazitekeleza?
 
Naungana na wewe mkuu, ngoja tusubiri.
 
Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,784
2,000
Mkuu nadhani niongeze kidogo kwenye bandiko lako mpaka sasa waliokuwa bado mawaziri na wameshindwa ni pamoja na Mhe Steven Kebwe na ambao walikuwa mawaziri na waliondoka kwa sababu mbali mbali ni Mhe Kagasheki,Mhe Gaudes Kabaka,Mhe Makongoro Mahanga,Mhe Cyril Chami,Mhe Adam Malima,Mhe Dr Seif. Mhe Prof. Kapuya
Kwangu somo ni kuwa kumbe umma ndiyo wenyewe nguvu ya maamuzi kuwaweka viongozi kwenye nafasi hizo na lingine kuwa umma unahitajika upewe Elimu zaidi ya nguvu walionayo.
Kwa Baraza jipya wagombea walituahidi kwenye kampeni muundo wa serikali utakuwaje tusubiri tuone ahadi walizotoa watazitekeleza?

Mbona Fenela unamruka Simbilisi wewe!
 
nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,051
2,000
Habari wadau

Mawaziri wa Jakaya Kikwete wamezidi kuangukia pua katika uchaguzi unaoendelea.

Baadhi ya waliokumbwa na dhahama hiyo ni Wassira, Chiza, Mwanri, Nundu, Kilango na Zambi..

Hata walioshinda ni kibahati nasibu mfano Mwakyembe.

Je Watanzania wenzangu tunapata somo gani hapa? Na tutegemee jipya gani kwa baraza jipya litakaloundwa na either Magufuli au Lowasa?
....mawaziri wengi wa serikali inayotoka madarakani walikua mizigo isiyobebeka...na wengi wao walipata vyeo kwa fadhila za mkuu wao...hivyo sishangai wakiangukia mapua....nitashangaa kama wale waliobahatika kupita hawatakuwa sehemu ya mawaziri wa magufuli(kama atashinda)...maana sioni atawatoa wapi wapya...wengi wao ni vihyo waliochaguliwa na watanzania waliopumbazwa na ccm kwa miaka mingi....Ndio maana tunasema ccm hawana jipya...
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
49,567
2,000
CCM ni ile ile.

Hakuna somo hapo.

Hata 2005 na 2010 waliangushwa mawaziri.
 
DuppyConqueror

JF-Expert Member
Mar 30, 2014
9,465
2,000
Habari wadau

Mawaziri wa Jakaya Kikwete wamezidi kuangukia pua katika uchaguzi unaoendelea.

Baadhi ya waliokumbwa na dhahama hiyo ni Wassira, Chiza, Mwanri, Nundu, Kilango na Zambi..

Hata walioshinda ni kibahati nasibu mfano Mwakyembe.

Je Watanzania wenzangu tunapata somo gani hapa? Na tutegemee jipya gani kwa baraza jipya litakaloundwa na either Magufuli au Lowasa?

Somo ni.
1. Ccm haijatumia mabavu hata pale ambapo heavy weights wameangushwa!
2. Uchaguzi huu ni huru na haki
3. Upinzani nanyie mkubali kushindwa, acheni kulialia
 
Ntaluke.N.

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
1,341
1,500
Somo ni.
1. Ccm haijatumia mabavu hata pale ambapo heavy weights wameangushwa!
2. Uchaguzi huu ni huru na haki
3. Upinzani nanyie mkubali kushindwa, acheni kulialia

Angalia ulichoandika halafu linganisha na maelezo ya mtoa post kama vinaendana ulicho andika wewe,ndio maana tunasema elimu,elimu,elimu.
 
iCode

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
732
250
Mbona mnamsahau Naibu waziri wa mifugo na uvuvi, kaika ole telele. Yeye na Titus Kamani walipigwa chini tangu kura za maoni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom