Kuanguka Mzee Sitta Uspika ni chereko na vifijo Mahakamani?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Huko nyuma Mheshimiwa Sitta alishawahi kuzozana na Jaji Mkuu kuhusiana na hukumu iliyotolewa na mahakama ya hakimu Mkaazi kule Manispaa ya Morogoro Mjini...............Kisa ni uchakachuaji wa mafuta.............EWURA ilimshitaki mmiliki wa kituo cha mafuta kuwa alikuwa ameyachakachua mafuta...................EWURA ndiyo waliokusanya ushahidi kulingana na sheria inayoanzisha Mamlaka hiyo.........

Mtuhumiwa alipoenda mahakamani alilalamikia haki zake za kimsingi kuwa sheria hiyo ya EWURA imezikiuka kwa vile EWURA ilikuwa ni hakimu kwenye kesi yake mwenyewe............EWURA wao ni mapolisi, mashahidi kwa maana ya wakusanya ushahidi n.k kwa hiyo wasingeweza kumtendea haki kwani hana uhakika yale mafuta waliyoyachukua kutoka kituo chake ndiyo yale yale au nao EWURA wameyachakachua kwa kumbadilishia....................

Hakimu aliafiki hoja za mtuhumiwa tajwa na hivyo kumfutia kesi.............

Ni kweli hakimu alikosea kwa sababu hakuwa na mamlaka ya kisheria kuhoji sheria zilizopitishwa na Bunge katika ngazi yake ila kwa maamuzi ya Mahakama Kuu.........

Lakini tatizo ni kuwa EWURA walipaswa wakate rufaa kupinga uamuzi huu lakini kwa sababu wajuazo wao hawakupinga uamuzi huo.................ikimaanisha ya kuwa waliuafiki.................Nao bunge walipaswa wairekebishe sheria hiyo ili kuondoa mianya ya kuidhoofisha EWURA Mahakamani lakini hadi leo haijarekebishwa..........Vile vile Bunge lilipaswa lidai maelezo kutoka serikalini ni kwa nini EWURA hawakukata rufani jambo ambalo Bunge chini ya Mzee Sitta hawakulifanya.......................kama huu sio uzembe wa Bunge sijui ni nini?

Sasa Mheshimiwa Sitta akiwa Spika wa bunge akalalamika Bungeni akiungwa mkono na wabunge wengi kuwa maamuzi yale ya kimahakama yalikuwa yameshawishiwa zaidi na mlungula.....na hapo Jaji Mkuu naye akawajia juu Bunge kwa kila alichokiita ni kuingilia uhuru wa mahakama...................Huo ukawa ni mvutano Babu K...........

Sasa baada ya Sitta kutupiwa virago na CC ya chama chake yawezekana kabisa kuna chereko na vifijo kwenye Mahakama zetu kuwa yule Spika ambaye sasa ni mstaafu aliyekuwa akishabikia Mahakama kudhalilishwa na Bunge sasa hana hiyo nafasi hiyo tena................

What do you think?
 
heshima kwako Ruta,

Mkuu kuanguka kwa Sitta ni zaidi ya ulichokileta jamvini !.
 
heshima kwako Ruta,

Mkuu kuanguka kwa Sitta ni zaidi ya ulichokileta jamvini !.

Fafanua la ziada ni lipi kama lipo......kwenye uwanja wa mahakama zetu?
 
Sitta ni mpiganaji wa ukweli na tunamuamini. na anaishi kwenye akili na mioyo yetu SITTA 2015
 
heshima kwako Ruta,

Mkuu kuanguka kwa Sitta ni zaidi ya ulichokileta jamvini !.

Soma kichwa cha habari.................suala hapa siyo sababu za Mzee Sitta kuanguka kwenye nafasi ya Uspika ila Mahakama imefurahi au la.........kutokana na mazingira niliyoyataja na au kama yapo mengineyo unayoyafahamu...........................
 
Sitta ni mpiganaji wa ukweli na tunamuamini. na anaishi kwenye akili na mioyo yetu SITTA 2015
Ni sawa lakini je mahakama zinamwonaje? Na haya mapungufu ya kutoichukulia hatua serikali kwa EWURA kufanya uzembe wa kutokata rufani na Bunge kutochukua hatua za kuirekebisha sheria inayoanzisha mamlaka ya EWURA ili kuondoa mianya ya kudhoofishwa mahakamani katika kutekeleza majukumu yake huoni naye Mzee Sitta kuwa uwezo wake kiutawala pale Bungeni nao ulikuwa ni wa kusua sua tu.............................Mzee Sitta pamoja na mikogo yake yote ukweli ni kuwa hajatusaidia sana katika kujenga mazingira mazuri ya utawala bora?
 
Back
Top Bottom