Kuanguka Lowassa: Tumaini la Bunge Wajibikaji?

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Nimekaa nikitafakari maneno aliyotoa Seleli kujibu hoja za Lowassa kulaumu Kamati na Riposti ya Mwakyembe. Kitendo cha Seleli kusimama kidete na kumjibu aliyekuwa Waziri Mkuu kwa ufundi, ukakamavu na bila woga na hata matokeo ya ukweli usiofichika kuwa Wabunge wengi wamefurahia kuangka kwa Lowassa, kunaashiria kuwa Lowassa hakuwa kiongozi mzuri wa Serikali bungeni!

Nafikiri pamoja na ubwegebwege na usanii wa ki-CCM uliokuwa umetawala Bungeni na hata kulifanya bunge kuishiwa hadhi, sababu kubwa ya Bunge letu kushindwa kufanya kazi ipaswavyo na kwa faida ya taifa inatokana na kiongozi wa Serikali Bungeni=Waziri Mkuu.

Tujiulize, hivi Lowassa aliharibu na kudhoofisha bunge letu kwa namna gani mpaka bunge likawa kama ni kikaragosi na si mhimili wa serikali?

Nukuu ya majibu ya Seleli kwa Lowassa

Drama as Mp Seleli challenges Lowassa

2008-02-08 09:06:55
By Guardian Reporter


A hushed Parliament was yesterday treated to breathtaking drama when Nzega MP Lucas Seleli, who is a member of the Parliamentary Select Committee on the Richmond power generating contract, took to the podium to tear apart earlier allegations made by Prime Minister Edward Lowassa that the committee had condemned him unheard, fabricated the allegations on his complicity in the controversial deal and annexed clippings from yellow tabloids as part of the testimonies presented to the House.

Prime Minister Edward Lowassa had made the allegations when he was announcing his resignation during the morning Bunge session.

Looking composed and bidding his time, Seleli said the committee comprised competent persons who done their homework, that there was documentary evidence to implicate the PM, and that there was no single attachment in the select committee`s findings that was from the gutter press.

Seleli said the committee had not lied. He challenged the Prime Minister to withdraw his allegations, short of which he would seek the application of Parliamentary Standing Orders to compel the Prime Minister to apologize.

House Speaker Sawel Sitta somehow eased the challenge when he asked the MP to confine his demand to the Prime Minister`s concern that the charges made by the probe team against him were fabricated.

When Lowassa rose to respond to Seleli`s demand that he withdraws his remarks, he said a line that was contained in the report that had particularly disturbed him was to the effect that ``the proprietors of Richmond are Prime Minister Lowassa and his close friend (Igunga MP) Rostam Aziz.``

Nevertheless, the Speaker skillfully sidestepped Seleli`s demands by inviting other MPs to contribute to the debate on the probe team?s findings.
  • SOURCE: Guardian
 
Naomba nimnukuu Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhsiana na uwajibikaji na utawala bora. Hapa inaonyesha wazi kuwa Lowassa alishindwa kazi

"Mapungufu yote tutayasimamia vizuri. Kama serikali tutayafanyia kazi na kuyarekebisha," alisema Waziri Mkuu Pinda. Alisema endapo watafanikiwa kutekeleza mambo hayo, anaamini mabadiliko makubwa ndani ya serikali na nchi yatapatikana
Waziri Mkuu Pinda alisema imani yake ni kwamba, kilichofanywa na Kamati Teule ya Bunge, si mambo ya visasi au chuki na kusisitiza umuhimu wa kuangalia mambo ya mbele na kusahau tofauti na mambo yaliyopita.

Katika kuonyesha msisitizo wa kutaka uwajibikaji ndani ya serikali, Pinda aliwataka Watanzania kujenga ushirikiano na serikali kwa kufichua taarifa zote za maovu nchini.

Waziri Mkuu Pinda akisisitiza hilo, alitaka wabunge kuondoa tofauti zao za kiitikadi na kuweka mbele mambo ambayo yanalenga kuleta maendeleo kwa nchi na watu wake.

"Kama lengo letu ni moja, kuleta maendeleo na kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania, hoja si vyama, ni kuleta maendeleo," alisema Waziri Mkuu Pinda na kuongeza:

"Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ningeomba ushirikiano kutoka kwa Watanzania wote, ushirikiano wa kufichua maovu yote nchini".

"Dalili zote za maovu zihakikishe zinasimamiwa na kudhibitiwa kikamilifu. Mapungufu yote tutayasimamia vizuri," alisisitiza.

Aliwataka watendaji ndani ya serikali ambao ni wasaidizi wakiwemo mawaziri, Mmnaibu mawaziri na makatibu wakuu, kutoa ushauri makini na wa kweli katika shughuli zao za kiutendaji.
Pinda alifafanua kwamba, alichojifunza katika ripoti ya kamati hiyo ya Bunge kuhusu Richmond ni mapungufu ya ushauri na kuongeza kwamba wakati mwingine mambo juu yanaweza kufikiriwa mazuri kumbe chini yameharibika.
 
Uwajibikaji na Ufanisi ndio vibwagizo anavyosema Pinda kwa Serikali!

Katika hatua nyingine, Pinda amesema kipaumbele chake ni kuimarisha utawala bora na kusimamia fedha za umma ambazo zinapotea katika Halmashauri za Wilaya na katika miradi mingine ya maendeleo.

Pinda alisema atachukua hatua hiyo ikiwa ni mkakati wake wa kuhakikisha kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania yanafanikiwa tofauti na ilivyo sasa.

“Kipaumbele changu kwa kweli ni kusimamia utawala bora, hapo ndipo ninaona kumekuwa na tatizo kubwa sana, maana hata pesa nyingi za miradi ya maendeleo ya wananchi imekuwa inapotelea mikononi mwa wajanja, nadhani nitajitahidi kudhibiti hali hiyo,” alisema Pinda.

Waziri Mkuu huyo aliongeza kuwa, amekuwa akilifuatilia suala la utawala bora pamoja na uwajibikaji tangu akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kuona mapungufu ambayo sasa ndiyo changamoto katika uongozi.

Waziri Mkuu Pinda alisema anachukua nafasi hiyo akiwa anafahamu matatizo kadhaa yaliyopo katika serikali, likiwamo la matumizi mabaya ya fedha, kutokuwajibika na suala la utawala wa sheria.

“Nina imani nikilivalia njuga suala la matumizi mabaya ya fedha, utawala wa sheria na uwajibikaji, nchi hii itabadilika na hatimaye kuwaonjesha Watanzania maisha bora ambayo Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiwaahidi,” alisema.

Alifafanua kuwa utawala bora ni pamoja na kusimamia vizuri fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, ambazo zimekuwa zinatumiwa vibaya na hakuna mtu anayewajibishwa kutokana na hilo.

Akizungumzia kashfa ya Richmond, Pinda alisema imetokana na kutokuwepo utawala bora, hivyo yeye ameahidi kusimamia dhana hiyo kwa kuamini kwamba, umma wa Watanzania una matarajio makubwa sana kutoka katika serikali hii mpya.
Pinda alisema katika sehemu kubwa wananchi wameanza kupoteza imani na serikali yao kutokana na watendaji wabovu, ambao wamekuwa hawaweki mambo yanayowahusu wananchi wazi, ili kila mmoja afahamu kinachoendelea katika serikali yake.
 
Haya ni kutoka Mama Kilango yanaonyesha wazi kuwa Lowassa hakuwa kiongozi muadilifu au makini. Hivyo kuanguka kwake ni daliliya ukombozi!

Mbunge Anne Kilango Malecela aliyekuwa akizungumza moja kwa moja kutoka Dodoma alisema kuwa, huo ni mwanzo wa ukombozi wa Watanzania kwa kuwa sasa wamechoka kulinda watu ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao ndani ya chama kuwanyamazisha wabunge ili kulinda ufisadi wao.

Alisema hatua iliyofikiwa sasa inatokana na uamuzi waliochukuwa wa kuvunja wigo wa kulinda maslahi ya watu binafsi kwa mwavuli wa chama, baada ya kunyamazishwa kwa muda mrefu na kutowatendea haki Watanzania.

“Tulikuwa tunazuiwa kuzungumza mambo muhimu bungeni, niliwahi kuuliza swali nikaandikiwa barua muda huo huo nikiitwa na kuambiwa nisirudie kuzungumza mambo hayo bungeni bali kwenye chama, lakini baadaye niligundua kuwa suala siyo chama, kumbe tunatakiwa kufanya hivyo kulinda maslahi ya watu wachache na si chama,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa hawatakubali kuwa raba chafu kwa kulinda watu wachafu, bali wataendelea kutetea maslahi ya chama na serikali, akiahidi kufanya mambo makubwa zaidi kwenye suala la BoT na kuibua hoja zaidi katika Bunge hili, ikiwemo kuangalia hatua za kisheria zinazoweza kuchukuliwa.
 
“Tulikuwa tunazuiwa kuzungumza mambo muhimu bungeni, niliwahi kuuliza swali nikaandikiwa barua muda huo huo nikiitwa na kuambiwa nisirudie kuzungumza mambo hayo bungeni bali kwenye chama, lakini baadaye niligundua kuwa suala siyo chama, kumbe tunatakiwa kufanya hivyo kulinda maslahi ya watu wachache na si chama,”

Please; hebu nisaidienei kidogo; Nani anaweza kujaribu kubuni..Ni nani alimuandikia huyu Mama barua..ya Kutisha? Nafikiri ni vema afahamke kwa ajil ya recods na Mambo mengine ya siku zijazo..!!

Huwezi Kuamini Mtanzania, Mbunge, aliyechanguliwa na wanchi anaweza Kuwa Intimidated within the "house" kwa kiwango cha kudhalilisha namna hii!

Kama Kilango na "FIRE" aliyokuwa nayo anaweza Kupigwa mkwara hivyo..jiulize itakuwaje kwa mwananchi wa kiwaida mtaani??

No No No!! There must come a time in our life where b the right thing should be done..And it must be done .. hata kma ni imposible!!
 
"Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ningeomba ushirikiano kutoka kwa Watanzania wote, ushirikiano wa kufichua maovu yote nchini".

"Dalili zote za maovu zihakikishe zinasimamiwa na kudhibitiwa kikamilifu. Mapungufu yote tutayasimamia vizuri," alisisitiza

Jiulize hata kama umepungukiwa na Utu kiasi gani! Kama MUOVU ndiye kiogozi mahali.. What do you xpect?
Muovu lazima atakuwa anaongoza sio kwa "kuwajibikia watu" ila kuficha Maovu yake na washiriki wake.

Kwa kuondoa nguvu ya maovu na dalili zake...Au kuifichua...uovu then there is a possibility bunge litakuwa effective!

uongozi ni jambo la muhimu sana wkenye maedeleo ya kijamii a kimaisha..Ukiwa na UOVU kama uongozi...Kinachopatikana ni bunge rojorojo kama la EL
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom