Kuanguka kwa shule za Jumuiya ya Wazazi ya CCM; nini kifanyike kizinusuru?

Mbwichichi

JF-Expert Member
Dec 19, 2018
267
1,331
Wasaalam,

Kwa kipindi ya miaka sita iliyopita hadi sasa kumekua na mdororo mkubwa kwenye uhai wa shule kubwa na kongwe za Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Hali hii imepelekea shule hizo kuwa na hali mbaya sana kiuchumi kiasi cha nyingi kushindwa kujiendesha.

- Kushindwa kulipa malipo ya mikataba(gratuity).

- Kushindwa kulipa mishahara kwa wakati.

- Kushindwa kulipa fedha za mafao ya wastaafu.

- Madeni makubwa ya kodi za TRA pamoja na wazabuni.

pamoja na mengine mengi.

Hizi zilikua shule bora sana miaka ya nyuma kabla ya utawala wa awamu ya tano ambao baada ya kuingia ulibadili mfumo ya ukusanyaji wa fedha kwenye kutumia "control number" ambazo ziko linked moja kwa moja na jumuiya, tofauti na mwanzo ambapo mkuu wa shule ndio alikua top wa maamuzi na alikua akipeleka capitation kwenye makao makuu ya jumuiya kulingana na idadi ya wanafunzi.

Tangu kuanza kwa mfumo wa controll number, mamlaka ya wakuu wa shule kufanya maamuzi yamepokwa na kuhamishwa kwa viongozi wa jumuiya ngazi ya wilaya ambao wengi wana upeo wa chini sana kwenye uendeshaji wa taasisi ikichangiwa na maamuzi yanayoongozwa na siasa na ulafi wa fedha bila kujali maendeleo ya shule.

Iidadi ya wanafunzi inashuka kila mwaka na hakuna tumaini kwamba zitarudi maana mama samia mwenyewe kasema sahivi yuko na serikali kwanza halafu chama kitafuatia baadaye.

Nini kifanyike kuzinusuru?
 
zitaje
 
Back
Top Bottom