From Mwanahalisi:
Katika sakatala Richmond, Kikwete alishauriwa na hatimaye akakubali kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge. Kikwete hakujua mkenge aliokuwa anauingia. Alipotoshwa na washauri wake ane akapotoka. Baada ya uchunguzi, Edward Lowassa mwenyewe anasema alimshauri Kikwete afike Dodoma usiku ili "kuzima" maasi ya wabunge wa CCM. Lakini washauri wakampotosha kuwa amshauri Lowassa aandike barua ya kujiuzuru lakini asiikubali.
Lowassa alipoondoka kurudi mjini, Kikwete akashauriwa naye akakubali Kujiuzulu kwaLowassa. Hii ilikuwa usiku wa manane na bila kumshirikisha Lowassa. Kikwete hakujua madhara ya jambo hilo. Alipotoshwa, akapotoka.
Serikali ikavunjika. Akalazimika kuiunda upya. Vita kali ya makundi ikahamia ndani yabaraza la mawaziri na kwenye chama. Hadi sasa, si Lowassa wala Kikwete aliye nafuraha na maamuzi yale yaliyotokana na ushauri mbaya aliyopewa rais.