Kuanguka kwa Demokrasia Tanzania: U-Magufuli na mabadiliko yasiyo na baraka za Watanzania

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Kwenye viunga vya wasomi na wanasiasa, wachambuzi na wanaharakati hili jambo linaendelea kujadiliwa sana.

Katika dhamira ya kuleta mabadiliko Rais Magufuli anaonekana kuwa na dhamira lakini amekosa wapi na lipi ashike.

Amekosa mipango ambayo ingeihakikishia Tanzania mabadiliko aliyokusudia kupita kwenye njia nzuri na sasa dhamira hiyo inwakwaza watanzania wengi.

Kilichoko CCM
Si tu kwamba Magufuli ametengeneza CCM mpya ya wakuja na wanaomuunga mkono, hata ilani ya chama na vipaumbele vyake havifuati.

Zipo taarifa za mgawanyiko mkubwa wa siri na tofauti za kimtazamo kuhusu namna anavyoendesha nchi.

Zipo taarifa za kujiamulia mambo ambayo hayapati baraka za chama na zipo taarifa za wazee kumsusa.

Zipo taarifa za kuvigawa vyombo vya kiutawala na kuweka watu wake hata kama wana makandokando ilimradi wanamuunga mkono na wale anaohisi watamsaidia kufika dhamira yake hata kama anavunja taratibu.

Kwa hali hiyo hata CCM kuna kuugulia na kuchukizwa kuhusu mambo yanavyokwenda ndani ya nchi.

Hata huko CCM kuna lawama na kutukuza . Kuna lawama za Kujifanyia mambo kwa mtazamo wa mtu na si wa chama na nchi kwa ujumla.

Kuhusu mageuzi anayotaka Magufuli kuelekea uzalendo na maendeleo chini ya chama kimoja na kuviza demokrasia kuna lawama kwa nini asipitishe mabadiliko katika utaratibu na maelewano na kuamua kutumia nyenzo zilizowekwa kisheria badala yake anaonekana kubaka tu na kuamrisha?

Lawama hizi zinakuja kwa kule kuichafua nchi na kutumia mbinu zinazoweza kuhatarisha amani. Hata CCM watu wamenuna. (Vyanzo vyetu mbalimbali)

Wanasiasa na makundi mengine
Kundi hili nalo linachukizwa, hapa wapo wanasiasa, wanaharakati, asasi za kiraia na kisheria na baadhi ya taasisi za dini. Wakati mwengine hulazimika kutumika Uzalendo tu ili mambo yasiharibike.

Niliwahi kupata taarifa kuhusu maamuzi ambayo yangekwisha kuchukuliwa dhidi ya kudai demokrasia lakini utu na uzalendo unawapa wakati mgumu wanasiasa na wanaharakati kiasi cha kujipa matumaini ya viongozi kujifunza na kutoa muda zaidi wakiamini wazee na wastaafu wataingilia kati.

Kikubwa ni huu Umagufuli na sio UCCM. Kama ni CCM tu hayo mabadiliko yangepitishwa kwenye njia zake kwa maslahi mapana ya Taifa hata kama kungetumika mbinu ovu lakini zilizokwenda shule.

Magufuli anafeli si tu kwa mbinu lakini kuwachukulia wapinzani kuwa si watu muhimu kwenye nchi na hatima yake anaidhoofisha kwanza nchi mbele ya ulimwwengu na CCM mbele ya uso wa dunia.

Ieleweke kwamba njia za mabadiliko ya kimfumo huulizwa wananchi jambo ambalo Magufuli hajalifanya.

Mifano inayotolewa ni kuja kwa vyama vingi na kuondowa mfumo wa chama kimoja wananchi waliulizwa na likawa jambo la kitaifa. Hata kama wachache walitaka mabadiliko lakini mfumo wa mabadiliko ulifuatwa kwa kiasi chake.

Leo Magufuli anauwa demokrasia na vyama vingi kinyemela ambayo ni njia isiyo salama kwa afya ya nchi. Hatima yake kunajitokeza chuki, visasi, na kuvunja umoja wetu.

UMAGUFULI v/s UTARATIBU
Bahati mbaya Rais anapotoshwa na baadhi ya wateule na viongozi wenye maslahi binafsi.

Kwani kuna ubaya gani kama Rais angeleta mjadala mezani wa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kuwachukuwa wanasiasa wote kwenye mjadala wa kitaifa ili kutengeneza strong politics zenye vionjo vya uzalendo kwa kuandaliwa mfumo, ambapo watu wote muhimu wakiwemo wanasiasa kuhakikishiwa vipawa vyao na mitazamo yao ingeheshimiwa kwenye mabadiliko hayo?

Kwa nini kusingeanza na Ajenda ya Kitaifa ya Mjadala wa mabadiliko na kupelekwa kwa wasomi kisha ndio kukatazamwa uungwaji mkono.

Baadae zingetumika njia za kidemokrasia Bungeni kuamua kwa wengi wape ili jambo likapata Baraka za wananchi na uwakilishi?

Kwa nini Magufuli kaamua kufanya kinyemela na kufuata mtazamo wake na si mtazamo wa wananchi walio wengi?

Kuwa na nia nzuri ni jambo moja na kuwa na mikakati mizuri ni jambo la pili. Magufuli ana nia nzuri lakini ana mipango mibovu.

Kwa Tanzania ilipofika katika demokrasia mabadiliko yoyote yasiyopata Baraka za makundi muhimu ni kuhatarisha umoja wetu na ustawi wa Tanzania.

USHAURI
Rais Magufuli tumia fursa iliyobaki ya kutuliza hali ili ukiondoka tukupe tuzo ya kitaifa bila kujali vyama. Anzia mwanzo na usianzie mwisho katika njia ya kutaka kuleta mabadiliko.

Itisha mjadala wa kitaifa na ukubali kukosolewa ili upate kupenyeza fikra zako. Watanzania ni waelewa na ni rahisi kusamehe.

Naamini watakusamehe na watakuwa nawe kwenye safari ya kweli ya mabadiliko. Nenda pale UDSM na kwenye vigoda upate ushauri hutojuta.

Walete wanasiasa pamoja na wewe uwe mlenzi wa maridhiano, sikiliza kilio chao, fuata ushauri mzuri utakaotolewa jenga gurudumu moja tu utaeleweka na sio kubaguwa na kuwaweka wanaokupinga kwenye kapu la wasio wazalendo.

Fikiria Katiba mpya hii ni kete iliyobaki kwa haya mambo ya kuchukiza na kutukuza ambayo ndani ya miaka 4 yamejitokeza.

Tanzania ni yetu sote.

Kishada.
 
Hapo kwenye ushauri mpaka sasa alipofikia ni vigumu kujishusha hivyo kwa sasa yupo ki pole la mbali na kwa kiasi kikubwa alichofanikiwa kushika baadhi ya vyombo vya dola kubadili mfumo huo ni ngumu tena
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi kupata Baraka za Watanzania imeanza leo kwenye matokeo ya huu uchaguzi wa serikali za mitaa na baraka hizo kukamilishwa mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

Kwa wasio fahamu kuhusu Tanzanian Democracy na African Democracy, nitembeleeni hapa

Rais Magufuli, please don't bow down kwa hawa mabeberu wa US na EU, waeleze Tanzania ni nchi, a sovereign state

P
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
mkuu nawe umo kwenye kundi la kumpumbaza mh wetu ? Hivi hio mada umeipitia kweli?

Angalia na risk zilizopo? UTARATIBU UFUATWE kufikia mabadiliko ya mfumo sio kubaka na kuhatarisha. Hio Tanzania democracy sio hiyo anayofanya Mzee. Labda iwe tumeanza kupotoka.
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Maendeleo hayawezi kuwa sababu ya kutufanya tuwe watumwa wa kifikra.
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Usilazimishe upuuzi wako kila mtu uauunge mkono, kati ya baba wa taifa na huyu jiwe ni nani anapaswa kufuatwa zaidi, yaani JK aanzishe utaratibu wa vyama vingi kwa maslah ya kujenga selikari inayokosolewa arafu atokee mtu/kikundi cha watu wavunje utaratibu kwa maslah yao binafsi..huu sio uungwana hata kidogo.
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Sawa
 
Mkuu,vipi uchaguzi wa viongozi serikali za mtaa hapo mtaani kwako unaendeleaje?
 
Tanzania Tunafuata Tanzanian Democracy model ambayo ni part of African Democracy.

Swali la msingi ni Watanzania wanataka nini kati ya demokrasia na maendeleo?. Watanzania wanataka maendeleo, na maendeleo hayana chama, hivyo rais Magufuli analeta maendeleo kupitia mwelekeo wa chama kimoja, kazi imeanza leo kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa na kukamilika mwakani katika uchaguzi Mkuu kwa Tanzania kurejea kuwa nchi ya chama kimoja, tukiisha pata maendeleo ndipo tutaigeukia demokrasia.

P
Ili chama kiwe na sifa ya kupewa nchi inatakiwa kikubalike na Jeshi, Usalama na Wananchi. Sasa kuna watu wanadhani ukishajua kujaza watu kwenye mkutano wako basi unapewa nchi. kwasababu wameshindwa kuwa na ushawishi hata kwenye awamu waliyoiita ya dhaifu basi Wacha turudi tulipotoka labda watakuja wenye ushawishi.
 
I am very sorry sikubaliani na ww hata kidogo, ushauri wako una chembe chembe za uchadema, unaposema umagufuli in English is Magulification sasa hebu google upate majibu yako kutoka kwa mmoja wa wasomi bora kabisa Africa. Acha mimi nikushauri ondoa uchadema kichwani mwako na ukubaliane na mimi this country or any country in Africa wanahitaji umagufuli you hate it or like it but Magufuli is the best president this country has ever had.

Ni Rais anaethubutu na amefanya makubwa mengi and of course ana mapungufu yake but mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Sasa hebu turudi kwa the so called demokrasia. Hivi ww unaielewaje demokrasia? Hivi vyama vya upinzani kila siku wanapiga kelele demokrasia inabakwa lakini wanasahau wabakaji wakubwa ni wao.

Hakuna demokrasia yoyote vyama vya upinzani kuna udikteta wa hali ya juu but you don’t see that, Leo kuna kesi ya mkulima kuhusu ukomo wa urais antaka katiba itafsiriwe lakini ACT pamoja na TLS (chama kipya cha upinzani) wamejiunga all they want is to make sure mahakama haiondoi ukomo wa rais but at the same time upinzani wao ruksa kukalia viti vyao for as long as they want. My question to you now hivi kweli unaamini kuna demokrasia ya kweli upinzani especially ACT and chadema???

If your answer is yes then you don’t know what does democracy mean. Tatizo kubwa upinzani ni ubinafsi na wanafanya mambo mengi yasyostahili kama udikteta wa wazi kabisa lakini bahati mbaya mazwazwa kama wewe hamuoni, leo hii magufuli akitaka kufanya mchakato wa kuondoa ukomo wa urais OMG Hiyo kelele itasikika dunia nzima, so please upinzani nendeni shule demokrasia sio maandamano, demokrasia ya kweli ni lazima iwe na ukomo wa uongozi sasa hivi bongo unfortunately hatuna vyama vya upinzani bali tuna makampuni binafsi yanayojiita opposition’s kumbe ni mafisadi. La mwisho watanzania tuwe na shukurani kwa JPM kafanya mengi makubwa na sikatai ana mapungufu yake kama binadamu wengine but i do know mazwazwa wengi kazi kuwaelimisha but we won’t give up.
 
Ili chama kiwe na sifa ya kupewa nchi inatakiwa kikubalike na Jeshi, Usalama na Wananchi. Sasa kuna watu wanadhani ukishajua kujaza watu kwenye mkutano wako basi unapewa nchi. kwasababu wameshindwa kuwa na ushawishi hata kwenye awamu waliyoiita ya dhaifu basi Wacha turudi tulipotoka labda watakuja wenye ushawishi.
Hakuna haja ya kuwaumiza ndugu zetu , kuharibu mali zao na kupandikiza chuki kisa kurejesha chama kimoja kwa njia ovu. Ndio tukasema kufuatwe butaratibu tu na nyenzo zipo.
 
I am very sorry sikubaliani na ww hata kidogo, ushauri wako una chembe chembe za uchadema, unaposema umagufuli in English is Magulification sasa hebu google upate majibu yako kutoka kwa mmoja wa wasomi bora kabisa Africa. Acha mimi nikushauri ondoa uchadema kichwani mwako na ukubaliane na mimi this country or any country in Africa wanahitaji umagufuli you hate it or like it but Magufuli is the best president this country has ever had. Ni Rais anaethubutu na amefanya makubwa mengi and of course ana mapungufu yake but mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Sasa hebu turudi kwa the so called demokrasia. Hivi ww unaielewaje demokrasia? Hivi vyama vya upinzani kila siku wanapiga kelele demokrasia inabakwa lakini wanasahau wabakaji wakubwa ni wao. Hakuna demokrasia yoyote vyama vya upinzani kuna udikteta wa hali ya juu but you don’t see that, Leo kuna kesi ya mkulima kuhusu ukomo wa urais antaka katiba itafsiriwe lakini ACT pamoja na TLS (chama kipya cha upinzani) wamejiunga all they want is to make sure mahakama haiondoi ukomo wa rais but at the same time upinzani wao ruksa kukalia viti vyao for as long as they want. My question to you now hivi kweli unaamini kuna demokrasia ya kweli upinzani especially ACT and chadema??? If your answer is yes then you don’t know what does democracy mean. Tatizo kubwa upinzani ni ubinafsi na wanafanya mambo mengi yasyostahili kama udikteta wa wazi kabisa lakini bahati mbaya mazwazwa kama wewe hamuoni, leo hii magufuli akitaka kufanya mchakato wa kuondoa ukomo wa urais OMG Hiyo kelele itasikika dunia nzima, so please upinzani nendeni shule demokrasia sio maandamano, demokrasia ya kweli ni lazima iwe na ukomo wa uongozi sasa hivi bongo unfortunately hatuna vyama vya upinzani bali tuna makampuni binafsi yanayojiita opposition’s kumbe ni mafisadi. La mwisho watanzania tuwe na shukurani kwa JPM kafanya mengi makubwa na sikatai ana mapungufu yake kama binadamu wengine but i do know mazwazwa wengi kazi kuwaelimisha but we won’t give up.
Kuna aliyefahamu hapa? Sisaelewa unekusudia nini hapa CDM inahusikaje hapa.
 
Umetumia haki yako ya uhuru wa kutoa maoni (freedom of expression), ila ulichoandika ni pumba, chakula cha nguruwe.

Kusema Magufuli ni best president ever wakati ni dikteta mwenye mapungufu kibao inaonyesha ubongo wako hauna uhusiano na vidole vilivyoandika.
 
Hakuna haja ya kuwaumiza ndugu zetu , kuharibu mali zao na kupandikiza chuki kisa kurejesha chama kimoja kwa njia ovu. Ndio tukasema kufuatwe butaratibu tu na nyenzo zipo.
Ushawishi ninaoongelea mm si wa kuumiza mtu. Kwann inashindikana kushawishi majeshi na usalama watoe sapoti kama mmna Nia njema na kitu cha tofauti kwa nchi? Kila siku kulalamikia polisi Mara usalama. Nani anataka kuongozwa na walalamishi?
 
Ili chama kiwe na sifa ya kupewa nchi inatakiwa kikubalike na Jeshi, Usalama na Wananchi. Sasa kuna watu wanadhani ukishajua kujaza watu kwenye mkutano wako basi unapewa nchi. kwasababu wameshindwa kuwa na ushawishi hata kwenye awamu waliyoiita ya dhaifu basi Wacha turudi tulipotoka labda watakuja wenye ushawishi.
Mifumo yetu haikuandaliwa kukubali mabadiliko. mimi nadhani CCM ingempinga tu Mwalimu Nyerere aliyeleta Vyama vingi. Hizi hadaa za kuumizana na kutumia nguvu nyingi baada ya CCM kushindwa baada ya miaka 25 ya vyama vingi ndio unakuja Uzalendo.
 
Unapimaje kukubalika chama na jeshi, usalama na wananchi? Kwa hiyo jeshi, usalama na wananchi ndio wanakubaliana na huu mwenendo wa kunajisi box la kura?
 
Mifumo yetu haikuandaliwa kukubali mabadiliko. mimi nadhani CCM ingempinga tu Mwalimu Nyerere aliyeleta Vyama vingi. Hizi hadaa za kuumizana na kutumia nguvu nyingi baada ya CCM kushindwa baada ya miaka 25 ya vyama vingi ndio unakuja Uzalendo.
Kama mfumo hauruhusu mabidiliko basi tusibadilike. Uzalendo oye?
 
Ushawishi ninaoongelea mm si wa kuumiza mtu. Kwann inashindikana kushawishi majeshi na usalama watoe sapoti kama mmna Nia njema na kitu cha tofauti kwa nchi? Kila siku kulalamikia polisi Mara usalama. Nani anataka kuongozwa na walalamishi?
Mbona unazunguka mbuyu. Hao usalama na Jeshi si ndio wafaidika wakubwa wa Mfumo tawala?. Kwani wameandaliwa kukubali mabadiliko? Miaka yote hiyo nchi ilipopigwa walikuwa wapi mbona walimiliki migodi?

Kaja Rais ambaye pengine ana nia njema lakini kakosa mbinu sasa Taifa Linaumiya na chuki inazidi kisa tu kutaka kurejesha chama kimoja. Kwa nini basi kusifuatwe taratibu?
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom