Kuanguka kwa CCM: Kutimilika kwa Unabii...

4. Mparangano mkubwa wa watawala ukilenga maslahi binafsi. Yaani "conflict of interest"
 
viongozi wakubwa ku-defect kwenda kwa rebels ambao huungwa mkono na dola kubwa duniani
 
Dola kutokili mapungufu yake na kutumia gharama yoyote ile kuwanyamazisha wakosoaji hata km ni kwa kuwaua au kuwapoteza
 
Maandamno yasiyokoma katika nchi nyingi duniani, Mvutano mkali kati ya wenye nacho na wasio nacho, Viongozi nguli kuwa dictators na kukataa kuondoka madarakani hata kama hawahitajiki, ugaidi wa ndani kutokana na chuki pandikizi....
 
Ni dhahiri kuwa ccm kinaelekea ukingoni kwani kimezidi kupoteza makundi mihimu ya wapiga kura.makundi hayo ni kama ifuatavyo

Sekta ya afya
wauguzi, waganga na wahudumu wa kada zote za afya ni watu wenye heshima iliyotukuka katika jamii.ni watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii yetu.leo hii serikali ya ccm imeonyesha dharau kwa watumishi wa sekta ya afya hivyo hukumu itafanywa na wananchi ambao tunahisi ni wavivu wa kifikiri.pia uko uwezekano wa watumishi wa kada ya afya kuwashawishi 'wagonjwa' kutoa asante kwa kuiangusha ccm.

Sekta ya elimu

waalimu kwa miaka mingi sana wamekuwa ni ngome muhimu ya ccm.kukusanya wanafunzi kwa ajili ya mbio za mwenge au mikutano ya chama.lakini sasa tuna idadi kubwa ya walimu vijana ambao wanajitahidi kuleta mabadiliko ya fikra za kale za walimu.
Mgomo wa walimu kesho unaweza kutupa mwanga ni kwa jinsi gani waalimu wako tayari kumpa mkono wa kwaheri swahiba wao wa siku nyingi ccm.

Vijana waajiriwa sekta binafsi
kundi hili limekuwa muhimu kutokana na mabadiliko ya sera za mafao ya uzeeni hasa kwa wale wa NSSF.hapa unaongelea walioajiriwa migodini,NGOs,Mashamba makubwa ya maua,viwanda vya nguo n.k
kiukweli wamechukizwa mno na jambo hili.

Wanavijiji
ukiona wazee wa kimasai wameshaanza kujua kuna vyama vingine zaidi ya ccm basi ujue mambo yamewiva kwa ccm kuondoka madarakani.watu wa vijijini ni wapinzani wa asili na wakikukataa itakubidi uhame kabisa.kuna story moja huko maeneo ya arumeru,wanakijiji ambao walikuwa ccm walohamia chadema na kuigeuza ofisi ya ccm kuwa ya chadema.

Wanafunzi wa vyuo
hii ndio chachu ya kuanguka kwa ccm.ni wanafunzi hawa hawa waliokosa ajira na kuingia mitaani na sumu ya ushawishi.sumu ambayo imeshaanza kuwatafuna wazee.najua njia ya kuwanyamazisha vijana hawa ni kuwapa madaraka lakini ubaya ni kwamba wamekuwa wengi mno.

wanajeshi wa vyeo vya chini
ni kundi linaloishi kwa manungu'niko makubwa kwa mfano kuchangishwa fedha za uniform,kutokupanda vyeo kama sio mtoto wa kigogo n.k kinachosaidia hapa ni nidhamu ya hali ya juu iliyoko JWTZ.sina uhakika kama nidhamu hiyo itaendelea kuwepo hivyo hivyo au la.wanajeshi hawa wanapashwa habari za ufisadi na uzembe wa serikali kupitia vilabu vya pombe,vyuo mbalimbali,vyombo vya habari na vijiweni kwa ndugu zao.

Hebu tuendelee kujadili wakati nikifikiria makundi mengine ya kijamii yaliyotupa mkono ccm.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
KWANZA NIKUPONGEZE KWA MJADALA HUU! MIMI NAJIKITA KATIKA KUNDI LA WAFANYAKAZI KADA YA AFYA: Hawa ndugu zetu (wafanyakazi katika kada ya afya) mara nyingi wamekuwa wakifanya kazi masaa ya usiku na BUNGE lilipitisha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004 iliyotoa haki ya mfanyakazi kulipwa japo 5% ya mshahara wa saa kwa kila saa aliyofanya kazi usiku (kuanzia saa 2.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri) lakini Serikali hii ya CCM inawazungusha na kuwanyima maskini watumishi hawa haki hiyo.

Ushauri wangu kwa CCM ni huu, kama kweli wanataka wapate kurejea mbele ya watanzania mwaka 2015 ajili ya kuwaomba tena ridhaa, basi makovu madogo madogo kama haya yaepukwe. Naomba Viongozi wa Serikali wajiulize, mfanyakazi wa umma anayefanya kazi usiku na ambaye mshahara wake ni Tsh. 400,000.00 kwa mwezi, mshahara wa saa utakuwa Tsh. 2,308.00. Asilimia 5 ya mshahara huo ni Tsh. 115.40. Kama Mtumishi huyu ameingia kazini usiku kwa siku 16 kwa mwezi na kila siku alifanya kazi masaa 10 kwa usiku mmoja, atakuwa na haki ya kulipwa 115.40 x 16 x 10 = 18,463.00 kwa mwezi! Je, hii ni ngumu kwa Serikali kulipa? hata kama tunadai kuwa hali ya uchumi ni mbaya kiasi hiki ni kidogo sana! Tuheshimu sheria zetu tunazoridhia wenyewe. Let's be Serious, otherwise 2015 will be a night mare! it will be a ':israel:' to CCM
 
Nadhani kundi lililobaki ambalo CCM wana uhakika nalo ni ndugu na familia ambazo ni wanachama wa CCM tena wanaonufaika moja kwa moja na ulaji kutoka CCM.
Sina uhakika sana na kundi la akina mama wasio na ajira maalumu ambao wengi wao ndio wanaojitokeza kwa wingi katika upigaji kura.
 
- Naongeza wakulima na hasa wakulima wa PAMBA ambao wamekatishwa tamaa na bei yakuuzia mazao yao, na tukiangalia kanda ya Ziwa inaongoza kwa kuwa na watu wengi kwa hiyo hii pia ni dalili ya anguko kwa CCM
- Pia Maeneo yaliyo jirani na machimbo ya madini wananchi wamekata tamaa na utawala wa CCM kwani hawafaidiki na rasilimali zilizopo katika maeneo yao
 
Nani aliekwambia kuwa CCM inashinda kwa kutegemea wapiga kura ? Na kwa kutegemea hayo makundi hata mkijipanga kama makobe waliomshinda sungura basi ,jamaa ataibuka kidedea ,na dalili moja siku ukitangazwa ushindi wa CCM wewe ndio wa mwanzo kusema ~~~~~ae wameiba tena !
 
hata wakulima wa korosho wamewachoka,juzi juzi tulishuhudia wakipanga magogo barabarani kweli hii ni dalili ya mauti ya ccm
 
Nani aliekwambia kuwa CCM inashinda kwa kutegemea wapiga kura ? Na kwa kutegemea hayo makundi hata mkijipanga kama makobe waliomshinda sungura basi ,jamaa ataibuka kidedea ,na dalili moja siku ukitangazwa ushindi wa CCM wewe ndio wa mwanzo kusema ~~~~~ae wameiba tena !
nadhani ulifuatilia uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki.wananchi wenyewe walifuatilia masanduku ya kura kuhakikisha ccm inapoteza.
 
Nadhani kundi lililobaki ambalo CCM wana uhakika nalo ni ndugu na familia ambazo ni wanachama wa CCM tena wanaonufaika moja kwa moja na ulaji kutoka CCM.
Sina uhakika sana na kundi la akina mama wasio na ajira maalumu ambao wengi wao ndio wanaojitokeza kwa wingi katika upigaji kura.
Kweli kabisa, mfano:
  1. Familia ya Mzee Malecela
  2. Familia ya Job Ndugai
  3. Familia ya Anna Makinda
  4. Familia ya Ngeleja
  5. Familia ya JK
  6. Familia ya Pinda
  7. n.k...
 
Mkuu mleta mada; kuna kundi moja muhimu sana ambalo hukuligusia katika mada yako na limekuwa likituamulia viongozi mara kadhaa. Kundi hili lina-cut across makundi yote uliyoyataja na kupitia viongozi wao wakati mwingine limekuwa na huenda kwa SIASA UCHWARA tunazoendekeza litaendelea kuwa na athari kubwa sana kwa chaguzi za nchi yetu.

Kimsingi kama hatutabadili mtazamo na kuhakikisha UZALENDO ndicho kigezo kikuu cha mtu kuchaguliwa katika nafasi yoyote ya utumishi wa umma, bado kundi hili litaendelea kuyumbisha siasa za nchi hii kwa faida ya mafisadi na makuwadi wao. Kundi hili mara nyingi limekuwa likitumika vibaya na sio jingine bali ni DINI.

Tunatazamana kidini badala ya uwezo na uzalendo wa mgombea. Tunatumia faida za dini zetu kujinadi pale inapowezekena na tunatisha wananchi wamkatae mgombea au chama fulani kidini kwa faida yetu na ya vyama vyetu! Hata Mwl. aliwahi kuzungumzia hili kwa mapana. Nawasilisha.
 
ni kweli kabisa kundi hili lina athari sana katika uchaguzi ingawa ninavyoamini viongozi wa dini hupima upepo wa waumini unavuma kuelekea wapi ndipo waingie kwenye matamko.
all in all wananchi wakiamua huwa hawasikii kama kuna padre,shehe,mchungaji,legwanani au mshiili.bahati mbaya ccm imeshawatosa hata hao viongozi wa dini na kuamua kuwakumbatia mafisadi.

KWA HISANI YA MTU WA MAREKANI
 
Back
Top Bottom