umedadavua vizuri
hata wakulima wa korosho wamewachoka,juzi juzi tulishuhudia wakipanga magogo barabarani kweli hii ni dalili ya mauti ya ccm- Naongeza wakulima na hasa wakulima wa PAMBA ambao wamekatishwa tamaa na bei yakuuzia mazao yao, na tukiangalia kanda ya Ziwa inaongoza kwa kuwa na watu wengi kwa hiyo hii pia ni dalili ya anguko kwa CCM
- Pia Maeneo yaliyo jirani na machimbo ya madini wananchi wamekata tamaa na utawala wa CCM kwani hawafaidiki na rasilimali zilizopo katika maeneo yao
nadhani ulifuatilia uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki.wananchi wenyewe walifuatilia masanduku ya kura kuhakikisha ccm inapoteza.Nani aliekwambia kuwa CCM inashinda kwa kutegemea wapiga kura ? Na kwa kutegemea hayo makundi hata mkijipanga kama makobe waliomshinda sungura basi ,jamaa ataibuka kidedea ,na dalili moja siku ukitangazwa ushindi wa CCM wewe ndio wa mwanzo kusema ~~~~~ae wameiba tena !
Kweli kabisa, mfano:Nadhani kundi lililobaki ambalo CCM wana uhakika nalo ni ndugu na familia ambazo ni wanachama wa CCM tena wanaonufaika moja kwa moja na ulaji kutoka CCM.
Sina uhakika sana na kundi la akina mama wasio na ajira maalumu ambao wengi wao ndio wanaojitokeza kwa wingi katika upigaji kura.
ni kweli kabisa kundi hili lina athari sana katika uchaguzi ingawa ninavyoamini viongozi wa dini hupima upepo wa waumini unavuma kuelekea wapi ndipo waingie kwenye matamko.Mkuu mleta mada; kuna kundi moja muhimu sana ambalo hukuligusia katika mada yako na limekuwa likituamulia viongozi mara kadhaa. Kundi hili lina-cut across makundi yote uliyoyataja na kupitia viongozi wao wakati mwingine limekuwa na huenda kwa SIASA UCHWARA tunazoendekeza litaendelea kuwa na athari kubwa sana kwa chaguzi za nchi yetu.
Kimsingi kama hatutabadili mtazamo na kuhakikisha UZALENDO ndicho kigezo kikuu cha mtu kuchaguliwa katika nafasi yoyote ya utumishi wa umma, bado kundi hili litaendelea kuyumbisha siasa za nchi hii kwa faida ya mafisadi na makuwadi wao. Kundi hili mara nyingi limekuwa likitumika vibaya na sio jingine bali ni DINI.
Tunatazamana kidini badala ya uwezo na uzalendo wa mgombea. Tunatumia faida za dini zetu kujinadi pale inapowezekena na tunatisha wananchi wamkatae mgombea au chama fulani kidini kwa faida yetu na ya vyama vyetu! Hata Mwl. aliwahi kuzungumzia hili kwa mapana. Nawasilisha.