Kuanguka kibiashara na namna ya kuweza kuinuka tena

Miss trinity

Member
Feb 18, 2014
95
24
Hii JF,

Naombeni msaada wenu,

Nimeshindwa kulinda biashara yangu kutokana na kuugua hapo awali, nilikuwa na Duka lenye thamani ya sh.ml.5 nilikuwa nauza vinywaji baridi, biscuits, juice, bites, cake and luxury items.

Nilikuwa nafanya biashara vizuri kabisa coz bites nyingi ni kazi ya mikono yangu na nilikuwa na wateja wengi sana but sasa hivi nasikia kuchanganyikiwa sana coz biashara imeisha yaani mafriji hayana hata vinywaji mtaji umekufa.

Naombeni ushauri wenu natamani sana kuinuka tena ila mkononi nina laki 200000 tuu sijui nifanyaje location ya biashara yangu ni mjini.
 
Hii jf,
Naombeni msaada wenu .nimeshindwa kulinda biashara yangu kutokana na kuugua
Hapo awali nilikuwa na Duka lenye thamani ya sh.ml.5 nilikuwa nauza vinywaji baridi ,biscuits, juice,bites,cake and luxury items. Nilikuwa nafanya biashara vizuri kabisa coz bites nyingi ni kazi ya mikono yangu.na nilikuwa na wateja wengi sana but sasa hivi nasikia kuchanganyikiwa sana coz biashara imeisha yaani mafriji hayan hata vinywaji mtaji umekufa .
Naombeni ushauri wenu natamani sana kuinuka tena ila mkononi Nina laki 200000 tuuu sijui nifanyaje.
Location ya biashara yangu ni mjini


Kuanguka na kusimama kwa wafanyabiashara wengi waliofanikiwa LEO kwao lilikuwa ni jambo la kawaida, usiache kumuomba Mungu sawasawa na imani yako. Atakupa kujua wapi ulikosea na wapi ufanye vipi ili biashara yako isimame tena kwa upya. Mungu akupe mwanzo mpya mwema wenye mafanikio
 
Asante
Kuanguka na kusimama kwa wafanyabiashara wengi waliofanikiwa LEO kwao lilikuwa ni jambo la kawaida, usiache kumuomba Mungu sawasawa na imani yako. Atakupa kujua wapi ulikosea na wapi ufanye vipi ili biashara yako isimame tena kwa upya. Mungu akupe mwanzo mpya mwema wenye mafanikio[/QUOTEasante sana
 
Kwa kuwa una ujuzi wa hio biashara na eneo la kazi unalo, na sababu ya mtaji kukata inaeleweka, unakopesheka. Nenda kny benki ndogo watakupa mkopo
 
Pole kwa yaliyokukuta, kabla ya ushauri nataka kujua wakati unaanza ulianza na mtaji kiasi gani..
 
nilikuwa nae but ndiye aliyenifikisha hapa nilipo
Hiki ndio kikwazo ulichokuwanacho kwa sasa na ukiweza kukitatua bas bila shaka biashara yako itainuka tena .......pengine ningependa kufahamu alikufikishaje hapo.....samahan lakin
 
achana na vyote hiyo laki mbilo anza kupika vitafunio na bites hadi usimame.
Inawezekana, Mungu akutangulie
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom