Kuandika Orodha ya Majina ya Kiafrika/Kitanzania na Maana Zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuandika Orodha ya Majina ya Kiafrika/Kitanzania na Maana Zake

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Companero, Sep 23, 2009.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ndugu Wanajamii, kuna ndugu zetu Wamarekani wenye Asili ya Afrika wanakuja Tanzania kutafuta mizizi (roots) yao katika programu ya African Diaspora Heritage Trail (ADHT) < http://www.africa-ata.org/adht.htm >. Sasa hawa wenzetu watahitaji kupata majina ya Kiafrika ili kila mmoja wao achague jina la kujiita. Pengine hili suala kwetu wenye majina kama Chairika ambayo wazazi wetu eti walitupa ili tuachane na kasumba na tuwe wazalendo ni suala la kawaida tu ila kwa wenzetu ni suala muhimu sana hasa ukizingatia kuwa utumwa ulijaribu kuwafanya wasahau asili yao. Kwa wale ambao mmepata kuitazama filamu ya 'Roots' mtakumbuka kuwa Kunta Kinte alilazimishwa kulisahau jina lake ili aitwe Thobi na alipambana sana ili asipoteze hiyo kumbukumbu ambayo Ngugi wa Thiong'o anatuelezea umuhimu wake katika Kitabu chake kipya cha 'Re-membering Africa', yaani, 'Kuikumbuka na Kuiunganisha Afrika iliyovunjwavunjwa'.

  Hivyo, naomba tuanze kuchangia kuijaza orodha hii hapo chini ili tupate majina ya kutosha kwa ajili ya wenzetu na kwa wale mnaojua programu za mtandao za kutafuta majina hayo na maana zake naomba mtume anuani za mitandao hiyo:

  1. Mkunde - Upendo/Love (Kichagga & Kipare), Male & Female Name respectively
  2. Wende - Upendo/Love (Kibena & Kihehe), Female Name
  3. Nyendo - Upendo/Love (Kigogo), Female Name
  4. Pendo - Upendo/Love (Kiswahili), Female Name
  5. ...
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,055
  Trophy Points: 280
  5. Butogwa-Upendo (Sukuma), female
  6. Lughano- Upendo (Nyakyusa), both for male and female
   
 3. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Che Kalizozele- wa Kujitafutia (Kwa wayao huko bandugu) Hili lilikuwa jina la utani la babu mzaa baba na alijipa mwenyewe.
   
Loading...