Kuandaa kanuni za vyama vya siasa kufanya mikutano ni hisani, haikubaliki

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,664
22,256
Tangu rais alipopiga marufuku vyama vya upinzani CCM imekua ikifanya mikutano kinyume na katiba kwa kigezo cha kijimilikisha nchi!

Chini ya mfumo wa vyama vingi zipo sheria zinazoelekeza jinsi mikutano ya vyama vyote vya siasa vinavyotakiwa kufanya mikutano na si kuandaa taratibu ambayo ni hisani kinyume na matakwa ya katiba.

Vyama vya siasa vinatakiwa visiingie kwenye mtego wa kupewa hisani ambayo kisheria haina nguvu badala yake wasimame kwenye matakwa ya katiba ambayo yapo na yanasimamia vyama vyote badala ya vyama vya upinzani kuundiwa kanuni!
 
thinkstupid.png

Uko sahihi chief.
 
Wataandaa kanuni ila watapangia watu maneno ya kuzungumza maana kwenye siasa maneno ndo hatari na sumu KUU.
 
Tangu rais alipopiga marufuku vyama vya upinzani CCM imekua ikifanya mikutano kinyume na katiba kwa kigezo cha kijimilikisha nchi! Chini ya mfumo wa vyama vingi zipo sheria zinazoelekeza jinsi mikutano ya vyama vyote vya siasa vinavyotakiwa kufanya mikutano na si kuandaa taratibu ambayo ni hisani kinyume na matakwa ya katiba.
Vyama vya siasa vinatakiwa visiingie kwenye mtego wa kupewa hisani ambayo kisheria haina nguvu badala yake wasimame kwenye matakwa ya katiba ambayo yapo na yanasimamia vyama vyote badala ya vyama vya upinzani kuundiwa kanuni!
KATIBA iliyopo ina KANUNI Za Vyama vya Siasa kufanya Shughuli zake bila Matatizo TATIZO ni CCM ,MSAJILI wa VYAMA na POLISI kuipendelea CCM
 
KATIBA iliyopo ina KANUNI Za Vyama vya Siasa kufanya Shughuli zake bila Matatizo TATIZO ni CCM ,MSAJILI wa VYAMA na POLISI kuipendelea CCM
Kama ni hivyo, kwanini vyama vya upinzani hawajawahi kwenda mahakamani kupinga kuzuiliwa kufanya hiyo mikutano ambayo ni haki yao kikatiba.?
 
Kama ni hivyo, kwanini vyama vya upinzani hawajawahi kwenda mahakamani kupinga kuzuiliwa kufanya hiyo mikutano ambayo ni haki yao kikatiba.?
Kwenda mahakamani kumshitaki Rais aliyepiga marufuku si jambo jepesi kwenye katiba ya Tanzania ambayo Rais hashitakiwi.
 
Back
Top Bottom