Kuaminishwa kuwa suluhisho la matatizo ya Waafrika itatokea kupitia ubobezi katika duru za diplomasia zenye mtazamo wa nchi za Ughaibuni

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
12,078
12,752
MAWAZO YALIYONIJAA KICHWANI DHIDI YA MSAADA WA VYANDARUA VYA KUJIZUIA NA MALARIA TULIVYOWAHI KUPATIWA NA MARAFIKI ZETU WA UGHAIBUNI NA JITIHADA YA WENZETU WOTE NCHINI WALIOIFANIKISHA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE

Kwanza, nimekuwa nikimfikiria sana yule mfanyakazi wa ofisi ya Ubalozi wa Marekani ambaye kwa nafasi yake aliona umuhimu wa kuandaa chapisho la ombi la vyandarua dhidi ya mbu waenezao malaria(itn) kutoka serikali yake mjini Washington kupatiwa Watanzania kama suluhisho dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Nimekuwa nikiwaza juu ya wapi ,na madhumuni gani ya huo msukumo wake,yapi malengo ya uthubutu wake huo katika "kutusaidia Watanzania"

Pili, kwa upekee kabisa nimemtafakari sana yule mtu wa wizara yetu ya afya aliyepeleka maombi ya kupatiwa vyandarua kupitia Wizara ya Mambo ya Nje. Nikawazua sana ujasiri alioupata wa kuona umuhimu wa hilo.

Tatu, mawazo yangu yakanipeleka kwa waziri wa wakati huo wa wa mambo ya nje na UHUSIANO wa kimataifa msomi mh.BENARD CAMILLIUS MEMBE katika NGUVU YA UJASIRI HUO pale alipoona ni Suluhisho na muhimu kuomba msaada wa vyandarua hivyo ima kwa maandishi ama kwa maneno wakati akiwa ndani ya tanzania ama nchini marekani.

Nne, nikaufikiria ujasiri wa Rais George Bush kuuona umuhimu wa Tanzania kupatiwa hivyo vyandarua.

Nikaganda nuktani hapa kuyasaili mawazo yake juu ya alivyokuwa anatufikiria tunavyofikirisha mawazo yetu humu bongoni mwetu?

Haki ya mungu nilifarijika sana kumuona Naibu Waziri wa Afya wa awamu hii ya 5 Dr. Laizer akichangia nondo za haja pale bungeni mjini dodoma siku chache kabla ya uteuzi wake wa nafasi wizarani pale.

Naibu huyu alipendekeza serikali iliwezeshe JWTZ kuwekeza katika mental integrity ya wataalamu wake wa afya watakaobobea katika kutafuta "masuluhisho ya kweli" katika kupambana na magonjwa ya mlipuko, endemics na pandemics.

Utajiri wa mawazo hayo ndiyo uhuru wenyewe wa kifikra; ndiyo uhuru walioupambania wazee wetu toka Vita ya Majimaji mpaka kushushwa kwa bendera ya Union Jack pale Shamba la Bibi tisa Desemba 61.

Inashangaza kuchusha na kusikitisha kuona bado eti kuna "aila" ya Watanzania wenzetu wanaofikiriwa kufikiri.

Wanaoweza kuomba na kuagiza vinavyoweza kutengenezwa hata na vijana wa jkt na makundi mengineyo.

Mwisho kabisa, nawafikiria wote waliofanikisha ujaji wa vile vyandarua vya George Bush sasa hivi wanajisikiaje wakiiona serikali ya awamu ya 5, serikali inayoamini katika mental integrity yetu wenyewe.

Serikali iliyoamua kuamua yaliyoshindikana huko nyuma kwa kisingizio cha "kujichosha" kufikiri.

Serikali inayoendelea kuichakata Tanzania ya viwanda na kuwa na malengo makubwa zaidi ya yale maombi ya vyandarua kutoka kwa marafiki zetu.

Wasalaam,

Jumbe brown
 
Tungeweza kwa kufundisha elimu yetu sisi wenyewe tunavyotaka. Hii mitaala takataka ya wazungu ndio mwanzo wa hayo yote! Hatuwezi badili hatma yetu bila kufundisha kile kinapaswa kufundisha na sio wazungu wanachotaka tusome!

Hatuwezi tegemea watu kama huyo waziri mpya wa afya!!Lazima tufumue elimu yetu iwe dira hasa katika kipindi hiki ambacho hatuna ajira ya kukidhi idadi kubwa ya wahitimu waliosomea ujinga wa wazungu!
 
Tungeweza kwa kufundisha elimu yetu sisi wenyewe tunavyotaka!!!hii mitaala takataka ya wazungu ndio mwanzo wa hayo yote!!!Hatuwezi badili hatma yetu bila kufundisha kile kinapaswa kufundisha na sio wazungu wanachotaka tusome!!Hatuwezi tegemea watu kama huyo waziri mpya wa afya!!Lazima tufumue elimu yetu iwe dira hasa katika kipindi hiki ambacho hatuna ajira ya kukidhi idadi kubwa ya wahitimu waliosomea ujinga wa wazungu!!!
Hiyo mitaala unayoiits takataka ya wazungu ndio.waliyoipitia viongozi wako na ndio msingi wa elimu hapa nchini. No offence. Simaanishi iendelee kutumika. Lakin je, tuna mtaala the best than hiyo tuliyoikuta?

Maana hata wanaotunga bado wanachezea keenye model ile ile ya mtaala wa kizungu.
 
Tungeweza kwa kufundisha elimu yetu sisi wenyewe tunavyotaka!!!hii mitaala takataka ya wazungu ndio mwanzo wa hayo yote! Hatuwezi badili hatma yetu bila kufundisha kile kinapaswa kufundisha na sio wazungu wanachotaka tusome! Hatuwezi tegemea watu kama huyo waziri mpya wa afya!!Lazima tufumue elimu yetu iwe dira hasa katika kipindi hiki ambacho hatuna ajira ya kukidhi idadi kubwa ya wahitimu waliosomea ujinga wa wazungu!
Umenena. Binafsi nilipomaliza udaktari wangu nilikuwa nafarijika kuitwa daktari ila sasa hivi sitaki kuitwa hivyo.

Elimu niliyopata baada ya kuisotea kwa miaka mingi sasa imeniongeza tu katika safari yangu ya kujitafsiri na kujifungamanisha zaidi kujikomboa kiukweli kama Mwafrika na si sifa za kijinga za titles koko.
 
Hiyo mitaala unayoiits takataka ya wazungu ndio.waliyoipitia viongozi wako na ndio msingi wa elimu hapa nchini. No offence. Simaanishi iendelee kutumika. Lakin je, tuna mtaala the best than hiyo tuliyoikuta?

Maana hata wanaotunga bado wanachezea keenye model ile ile ya mtaala wa kizungu.
Komredi HATUNA budi kubadilika...
 
Back
Top Bottom