Kuamini sana miujiza na kupenda kuombewa ndo sababu kuu ya wakristo kuburuzwa na matapeli Africa

Ebale

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
943
1,683
Ni ukweli usiopingika kuwa wakristo wanaamini sana miujiza! ukiwaambia unauwezo wa kuponya vilema na kuwaombea wapate magari kesho watafurika hadi ukose nafasi ya kukaa. Ni watu wasiojiamini kuwa wanaweza kujiombea wao wenyewe na kwamba Mungu atawasikia bila kupitia kwa mtu -mchungaji! hizi ndo sababu kubwa kwanini wamekuwa rahisi kutapeliwa na wanaojiita manabii
 
Inaskitisha ndugu yangu misingi ya kikristo imebebwa na neno LA mungu na ndo katiba ya mkristo cha ajabu wengi tumesahau neno LA mungu linasemaje maana neno LA mungu linasema "mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu ombeni lote mtakalo nanyi mtapewa, sasa Leo hatuamini kuna uweza wa kipekee ndani yetu Ila tupo tayari kuhonga ata nyumba ili uwezo wa anayejiamini ukutendee muujiza,,,, kuwa turudi kwenye msingi wa neno tusiangamie kwa kukosa maarifa jamani
 
Ni ukweli usiopingika kuwa wakristo wanaamini sana miujiza! ukiwaambia unauwezo wa kuponya vilema na kuwaombea wapate magari kesho watafurika hadi ukose nafasi ya kukaa. Ni watu wasiojiamini kuwa wanaweza kujiombea wao wenyewe na kwamba Mungu atawasikia bila kupitia kwa mtu -mchungaji! hizi ndo sababu kubwa kwanini wamekuwa rahisi kutapeliwa na wanaojiita manabii

Acha wataperiwa tu hakuna namna
 
Mzee wa bapa mpaka kajengewa barabara na yule jamaa aliyesafiri mpaka Loliondo kufuata kutapeliwa
 
Dini ni biashara toka enzi hizo za mababu na mabibi zetu, hakuna dini inayoendeshwa bila ya kuwa na malengo ya kibiashara, lengo ni moja tu, pesa, sasa manabii feki, kama kina Joshua, Gwajima, Lwakatare, Nsekelo, Kakobe na wengine wote, wale ni opportunists, wao na na jamaa zao ni MATAPELI, period, hakuna neno lingine la kutumia au kuwaita zaidi ya hilo. Hawa wanatumia shida, uzuzu, ujinga na umaskini wetu ili wao watajirike. Hawa yale sio makanisa, zile ni ofisi za kitapeli, ni kampuni, wamejipanga vilivyo na watu wao kila idara, kuanzia uhamasishaji, ulinzi na masoko. Hawavunji sheria, na wanatupata kweli kweli..Humu wamejaa, watakuja kuwatetea..
 
Hii mada inawahusu wakristo,itapata wachangiaji wachache ambao ni waisilamu lakini kama ingelikuwa ni mada inayowahusu waisilamu,wangejazana wakristo wa madhehebu yote na kuanza kujadili kuidandia kwa mbele matusi ya kuudhi na kuharibu siku za watu upingaji nk.nk.utafikiri simba na yanga.
 
unajua dini hiwe uislamu au ukristo kivuli chake ni imani
jinsi imani kwa mwanadamu inavo mtawala.
imani hii utengeneza vitu vingi ili mwanadamu ashawishiwe kwa kitu chochote kwa kuwa asilimia kubwa ya bindamu kiakili imetawaliwa na imani .
ukijua haya basi acha kuwa unatoa lawama.unajua hata al shabab,bokoharamu nao utumia imani ili kuwa danganya watu kwa njia kuwa ukijitoa muhanga una kwenda peponi
 
Imani inatumiwa kama silaha ya kutugawanya kutuchonganisha huku wao wakichukua mchanga wa dhahabu.
 
Umenena kweli mkuu... Hii ndio sababu kuu inayowavuta watu kujaa kwny makanisa wakitafuta miujiza. Ikumbukwe kuwa hata shetani naye anayo nguvu ya kufanya miujiza. So ndo kama hvyo hakuna namna zaid ya kusoma vitabu vya dini ili kujifunza zaid kiliko kutemea miujiza
 
Back
Top Bottom