Kuambiwa upeleke kondoo mweupe kama mahali, hii imekaaje wakuu?

nchonga aliyebaki

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
571
1,000
Nina mdogo wangu amepata mchumba kutoka uhayani yaan huko, Bukoba,

Sasa katika mambo aliyoorodheshewa kuambatanishwa kwenye mahali wamesema haya

1. Ng'ombe mmoja wakaandika (Nkoromoijo) sikuelewa,

2.Shilingi 800,000 kwa ajili ya baba mzazi

3. Wakaandika 500,000 kwa ajili ya mama mzazi

4. Wakaandika 300,000 kwa baba mdogo na mashangazi,

5. Mbuzi kwa ajili ya babu-Beberu

6.Mbuzi kwa ajili ya baba mtoto-Beberu

7.Mbuzi kwa ajili ya Ma baba mdogo- Beberu

8. Mwishoni kwa msisitizo wakasema (entama ekwela) yaan kondoo mweupe na ni muhimu kwenda,

Hii imetuchanganya sana akili,

Huyu kondoo ni kwa ajili ya nini?

Wahaya naomba mnipe uzoefu wa huko kama hakuna masuala ya kutambikia hapo
 
Oct 3, 2017
64
150
Jesus Christ eheee, umepeleleza vizuri familia mnayotaka kuoa hiyo?

Sisi tunaamini kwamba masuala ya kondoo uhusisha tambiko, lakin kwetu sisi wenye dini zaid tunaamini hayo ya kutambikia yaliisha zamani tokea mwana wa Mungu Yesu Kristo alipowekwa msalabani na kumwaga damu pale (INRI) ikimaanisha imekwisha, yaan masuala ya Tambiko hayana maana tena,

Sasa kwanini umetumwa kondoo ni ukute pale kuna mizimu ambayo kama haitaridhiswa utazaa watoto wana kufa, au walemavu, au mataahira kidogo, kwahiyo wanatambikia ili mizimu iridhike,

Kazi unayo ya kumbadilisha huyo mke mpaka awe mkristo kweli kweli itakuchukua muda sana
 

roselina john

JF-Expert Member
Aug 17, 2017
756
1,000
Muwage mnauliza hata Koo si kuparamia tu, ona sasa unaenda kulazimika kuyashape mataahira kwa damu ya Kondoo
 

instanbul

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
7,333
2,000
Mambo ya kutambika yalishaisha uhayani tangu ukristu ulivyoingia kutia mizizi ipasavyo miaka ya 1880

Sasa kama kuna koo na familia zinaomba mara mbuzi mweupe huo ukoo uchunguze vzr labda Una mambo ya kishirikina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom