Kuajiriwa walimu wapya kuna siasa ndani yake?

Patflax jr

Member
Apr 11, 2011
72
1
Wapendwa kuna mambo mengi yanaumiza vichwa. Mlio karibu na Wizara ya Elimu hebu nidokezeni: hivi ajira kwa WAALIMU wa Diploma na Grade "A" waliofanya mtihani may mwaka huu na matokeo kutoka mwezi AUGUST ni kwanini hawajapewa POST zao hadi leo? au shule za Tanzania WALIMU wametosha? au ndo bajeti ya MISHAHARA YAO ilipelekwa IGUNGA?
 
Inashangaza sana kuona wizara na idara kadhaa za serikali zinatolewa nje ya majengo ya NHC kwa kulimbikiza kodi ya pango.
Inashangaza kwa vile serikali hii hii inaweza kusaidia chama tawala katika kampaign za uchaguzi na kuingia gharama kubwa wakati mambo ya msingi kama kodi ya pango hayatiliwi maanani. Bila kuwakaba koo hawalipi kodi! Ingekuwa NHC ni shirika binafsi tungeona jinsi viongozi wanavyokumbushana kulipa haraka!
 


amka2.gif

Njama za kumhonga Waziri Tibaijuka zafichuka

• Yeye asema wasipoteze muda bure


na Mwandishi wetu


MPANGO kamambe wa wafanyabiashara watatu, wawili kati yao wakiwa ni wenye asili ya Kiasia wa kula njama za kumhonga Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ili auondoe uongozi mzima wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) umekwama.Habari kutoka vyanzo vya habari vya kuaminika, zimesema kuwa wafanyabiashara hao wakishirikiana na mwenzao Mtanzania, walikula njama za kutaka kumhonga Waziri Tibaijuka kiasi cha sh milioni 500, lakini ikashindikana baada ya mbinu zote za kumkaribia kushindikana.

Imedaiwa kuwa baada ya kushindwa, wafanyabiashara hao walipanga kumwona mmoja wa wasaidizi wa Waziri Tibaijuka, ama mtu makini na aliye na mahusiano ya karibu zaidi na Rais Kikwete na kumweka ‘sawa’ ili watimize malengo yao hayo.
Habari zinasema watu hao ambao wamesitisha kwa muda mpango huo baada ya kuhisi wanafuatiliwa na watu wasiojulikana, walipanga kutumia maneno mazuri ya kuupongeza uongozi wa NHC, na kuomba ikiwezekana, mkurugenzi mkuu wake, Nehemia Mchechu, aondolewe na kupelekwa katika shirika jingine linalolegalega kwa madai ya kwenda ‘kulifufua’.
Awali imedaiwa kwamba walikusudia kumchongea mkurugenzi huyo kwa tuhuma mbalimbali, lakini ikabainika kuwa njia hiyo isingefanikiwa baada ya kukosa ushahidi wa tuhuma walizofikiria.
Habari zimedai kuwa watu hao wanaungwa mkono na baadhi ya watu wanaochukizwa na utendaji kazi wa shirika hilo, kwa madai kuwa limewaharibia mambo mengi waliyokuwa wakifaidika nayo na hivyo kuondoka kwake kungerudisha fursa zilizokuwa zikiwapa ulaji.
Kwa mujibu wa habari hizo, watu waliokula njama hizo wanadai kupanga kufanya kile kilichotokea miaka kadhaa iliyopita, wakati aliyepata kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, alipohamishwa katika wizara hiyo baada ya kuendesha kwa muda operesheni zinazofanana na zile za Mchechu.
Waziri Tibaijuka alipoulizwa juu ya taarifa hizo, alidharau na kuuponda vikali mpango huo kama upo na akaweka bayana kuwa ingawa hajasikia wala kuona jitihada zozote za watu wenye nia hiyo, wasijisumbue maana watapoteza muda wao bure.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, waziri huyo alisema anamuunga mkono Mchechu na timu yake kwa kazi anayofanya na hana wazo la kumshawishi Rais na wala hawezi kufanya hivyo kwa sasa kwa vile kazi ya kuboresha na kuinua hali ya NHC ni ya kujivunia.
“Kwanza sijasikia wala kuona dalili zozote za jambo hilo. Lakini kama wapo wanaoota ndoto hizo, waambie wanajisumbua bure,” alisema Tibaijuka na kuongeza: “ Wizara yangu inajivunia utendaji kazi wa kijana huyu (Mchechu) na timu yake katika kuinua shirika hili ambalo lilielekea kufa.”
Waziri Tibaijuka alisema hatashangaa kusikia kuwepo kwa mbinu hizo kwa kuwa kazi ya kupambana na maovu sio lele mama na inahitaji mtu jasiri na mwenye nia njema kwa taifa kuweza kushinda maadui.
“Wanaweza kuwapo watu wa aina hiyo. Lakini kwangu mimi na uzee wangu hizo pesa chafu nizipeleke wapi? Naridhika na hiki kidogo ninachokipata na nina furaha na amani,” alisema na kulitaka gazeti hili na vyombo vingine vya habari kutosita kufichua maovu hata kama vitachukiwa na baadhi ya watu.
“Tusiogope kutenda haki na mema, kama linavyofanya gazeti lenu. Chapeni na tuchape kazi bila uonevu wala upendeleo. Nanyi nawapongeza sana,” alisema waziri huyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu huyo wa NHC, (Mchechu) bila kukiri kama amesikia habari hizo au hapana, aliweka bayana kuwa hataogopa vitisho wala ushawishi wa aina yoyote wenye kumkatisha tamaa kwa kuwa anaamini anachokifanya ni haki na sahihi.
Alisema yuko tayari hata leo kuachia ngazi ikiwa mamlaka iliyomteua itasema hivyo, kwa vile hakuzaliwa awe mkurugenzi wa shirika hilo na anatambua kuwa cheo ni dhamana na sio mahali pa ulaji ama kujitajirisha kwa fedha chafu.
“Nimeletwa hapa kuwatumikia watu na nitafanya hivyo kwa uadilifu, uaminifu na ukweli kwa taifa langu bila kumwonea mtu kutokana na rangi, kabila ama uwezo wake. Wale wanaodhani nitatishika kwa lolote wasahau,” alisema.
Aliongeza kuwa haogopi kuondolewa katika nafasi hiyo, na wala haogopi kutishiwa maisha kwa sababu hakuna mwanadamu aliyepangiwa kuishi duniani milele.
“Hakuna atakayeishi milele hapa. Kwa hiyo suala la mtu kuniambia kuwa ataniua kwa sababu tu nimetekeleza wajibu wangu kwa taifa langu na faida ya Watanzania ni kupoteza muda wake bure,” alisema na kuongeza: “Niko tayari kuishi miaka michache kwa utumishi uliotukuka, kuliko miaka 70 ya wizi na ufisadi wa mali ya taifa.”
Alikiri kwamba amekuwa akipata changamoto nyingi zikiwemo za kumkatisha tamaa, lakini yeye na wenzake katika shirika hilo hawatatetereka katika kuchapa kazi.
Mchechu ambaye aliteuliwa kushika wadhifa wa ukurugenzi katika shirika hilo katika kipindi kisichozidi miaka miwili, amefanya mabadiliko makubwa ya shirika lililoelekea kufilisika hadi kuwa moja ya taasisi za umma zenye nguvu.
Shirika hilo limethubutu kufanya kile ambacho ilionekana ni ndoto kufanyika hasa baada ya kuwatimua kutoka katika nyumba zake, wapangaji wote waliokuwa na madeni sugu na ambao walikataa kulipa fedha za pango kwa miaka mingi.
Katika operesheni kadhaa zilizofanyika, shirika hilo lililopata timu mpya, limewatimua baadhi ya watu wazito ‘vigogo’ wa idara za serikali zilizoshindwa kulipa madeni.Hivi karibuni, NHC ilitoa dodoso kadhaa za kusaidia kuboresha utendaji kazi wake, lakini zikalalamikiwa na baadhi ya wapangaji wake hususan wenye asili ya Kiasia kuwa lilikuwa la kibaguzi wa rangi na lililojaa unyanyasaji mkubwa.

Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya wala msikate tamaa , Watanzania wote wenye nia nzuri na taifa hili wapo nyuma yenu wanawaunga mkono


 
KAMPUNI ya Singita Grumeti Reserves , inayomiliki hoteli ya nyota tano ya Sasakwa imeahidi kuchangia ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa. unaotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Burunga, wilayani Serengeti.​

Ahadi hizo zilitolewa juzi na Ofisa Maendeleo ya Jamii wa kampuni hiyo, Richard Ndaskoi, baada ya kusaini makubaliano kuhusu kampuni yake, kusaidia utekelezaji wa miradi ya jamii.Makubaliano hayo ni kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kampuni hiyo, inayoendesha shughuli zake ndani ya kampuni hiyo.

"Suala la uwanja wa ndege wa kimataifa limo ndani ya makubaliano hayo ,uwanja si wa kampuni lakini kwa kuzingatia kazi za utalii zinazofanywa na kampuni, kampuni itachangia ujenzi huo na katika hatua za awali imelipa Sh400 milioni kwa ajili ya fidia kwa wananchi watakaopisha ujenzi wa uwanja,"alisema.

Napata shida kuelewa ni kwanini kijiji cha Burungi kimeweka ujenzi wa kiwanja cha ndege tena cha kimataifa katika vipaumbele vyake?? Hapa nadhani kijiji kimetumika kutimiza matakwa ya Mwekezaji mkubwa wa kimarekani na wahujumu uchumi wa nchi hii. Kampuni inasema "itachangia" 400mil, je mjenzi hasa wa kiwanja hicho ni nani?????Kijiji cha Burungu/Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti/Serikali kuu?? Kama serikali ilishindwa kuzuia utoroshwaji wa wanyamapori wetu hapo KIA kweupeeeeeeee, hivi itaweza kweli kuzuia utoroshwaji wa madin ya nyamongo, na wanyamapori wa Serengeti, ikorongo-grumeti na rasilimali nyingine??? Huo uwanja wa ndege wa kimataifa hasa utamnufaisha nani huko maporini????Mbona serengeti, grumeti game reserve kuna viwanja vya kutosha tu kwa ajili ya shughuli za watalii??kwanini hadi kiwe kiwanja cha kimataifa????Ndugu zangu watanzania, haya ni maandalizi tu yakuibiwa rasilimali zetu. Je mnadhani tanzania inahitaji kiwanja cha kimataifa kujengwa katika kijiji cha Burunga,kweli kiwanja cha ndege cha aina hii ni kipaumbele kwa sasa wakati nchi haina barabara za uhakika za kuunganisha vijiji achia mbali mikoa?????????????Toa maoni yako kuhusu hili.

Source Mwananchi Friday, 07/08 October 2011
SGRi yaahidi kuchangia ujenzi uwanja wa ndege
 
Wapendwa kuna mambo mengi yanaumiza vichwa. Mlio karibu na Wizara ya Elimu hebu nidokezeni: hivi ajira kwa WAALIMU wa Diploma na Grade "A" waliofanya mtihani may mwaka huu na matokeo kutoka mwezi AUGUST ni kwanini hawajapewa POST zao hadi leo? au shule za Tanzania WALIMU wametosha? au ndo bajeti ya MISHAHARA YAO ilipelekwa IGUNGA?

Kila kitu ni mipango wewe. Kila kitu kinakuwa politicised bila sababu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom