Kuajiriwa vs kujiajiri, Kipi bora kwako?

me1

JF-Expert Member
Jan 24, 2015
364
409
Habari za wakati wakuu..
Tukiwa tunaishi nchi ambayo sasa unaweza kulala ukiwa waziri leo na kesho ukaamka ukiwa raia wa kawaida kutokana na kasi ya mkuu wa kaya na hii kauli mbiu ya ufinyaji majipu,sasa ni wakati wa kuhimizana na kupeana muongozo juu ya mada tajwa hapo juu.

1. KUAJIRIWA
We unadhani kwanin mtu anastahili kuajiriwa? Vipi risk ya kupokonywa cheo? Je hayo ndo Malengo yako? Uko smart kiasi cha kuwa bora kwa muajiri wako? Ni faida zipi atazipata mtu kwa kuchagua kuwa mwajiriwa? Standard ya maisha ya watu walioajiriwa wenye elimu kama yako au sawa na yako ikoje? Utatimiza ndoto zako?

2.KUJIAJIRI
Kwanin ujiajiri hata kama kazi zipo? Vipi mtaji unatoa wapi? Una skill ya management kumiliki watu utaokua nao? Una akili ya biashara? Na vp risks? n.k

Hebu njoo useme kwanini unaona ni sawa kuajiriwa au kujiajiri huku ukitoa sababu za msingi kumshawishi msomaji juu ya msimamo wako

Tuambie unaingizaje kipato na hapo ulipo unaona dalili za kutimiza malengo yako? Vipi rise n falls unazopitia na changamoto zote?

Share na sisi.Karibu tujadili.
 
Kujiajiri ndiyo mpango mzima kwa kipindi maana itakufanya kuwa huru yani "financial freedom " mbali na kuwa huru kifedha pia kujiajiri kunakusadia kufanya kazi katika mawanda na weledi unaoutaka n.k

Hivyo basi katika karne hii bora ujiajiri kuliko kuajiriwa ila kwa wale wanaotaka sifa waonekane wanakaa kwenye viti vya kuzunguka tafuta ajira ila aliejiajiri anapata mkwanja mrefu sana.
 
Ahsante mkuu,lakin mbona kuna walioajiriwa na wanaishi maisha makubwa tu.Na vip kuhusu kila mtu akijiajir itakuaje? Na inshu ya mtaji ikoje kwa upande wako?
 
Kama mazingira ya kujiajiri yako kirafiki basi kujiajiri kutakuwa kuzuri zaidi. Kujiajiri kunapokuwa kugumu kutokana na kukosa mazingira rafiki, mtaji, exposure, business management skills na mengineyo basi unajikuta ukiendelea kuajiriwa.

Lakini pia tupo wengine ambao kwa sababu mbalimbali tumejikuta tunalazimika kuendelea kuajiriwa na wakati huo huo tukiajiri wengine. Ikitokea umepelekeshwa ofisini na mwajiri wako nawe ukirudi kwenye biashara zako kupunguza stress hasira zako unazihamishia kwa waajiriwa wako na hivyo maisha yanaendelea kusonga. Siku ikifika tutajiajiri jumla.
 
Binafsi kama una mtaji in vema ukajiajiri madhara ya kuajiriwa ni makubwa kuliko ya kujiajiri majipu
 
  • Thanks
Reactions: me1
Kama mazingira ya kujiajiri yako kirafiki basi kujiajiri kutakuwa kuzuri zaidi. Kujiajiri kunapokuwa kugumu kutokana na kukosa mazingira rafiki, mtaji, exposure, business management skills na mengineyo basi unajikuta ukiendelea kuajiriwa.

Lakini pia tupo wengine ambao kwa sababu mbalimbali tumejikuta tunalazimika kuendelea kuajiriwa na wakati huo huo tukiajiri wengine. Ikitokea umepelekeshwa ofisini na mwajiri wako nawe ukirudi kwenye biashara zako kupunguza stress hasira zako unazihamishia kwa waajiriwa wako na hivyo maisha yanaendelea kusonga. Siku ikifika tutajiajiri jumla.

Huu ndo mpango mzima.... unaajiriwa na unaajiri. Security ya maisha bora wakati wowote.
 
Kama mazingira ya kujiajiri yako kirafiki basi kujiajiri kutakuwa kuzuri zaidi. Kujiajiri kunapokuwa kugumu kutokana na kukosa mazingira rafiki, mtaji, exposure, business management skills na mengineyo basi unajikuta ukiendelea kuajiriwa.

Lakini pia tupo wengine ambao kwa sababu mbalimbali tumejikuta tunalazimika kuendelea kuajiriwa na wakati huo huo tukiajiri wengine. Ikitokea umepelekeshwa ofisini na mwajiri wako nawe ukirudi kwenye biashara zako kupunguza stress hasira zako unazihamishia kwa waajiriwa wako na hivyo maisha yanaendelea kusonga. Siku ikifika tutajiajiri jumla.
Kipi kinakukwamisha hasa na kujikuta umebaki mwajiriwa.
Na je unapata muda wa kutosha kusimamia kazi yako ya kujiajiri baada ya kutoka kwa mwajiri? Vip ufanis wa kufanya kazi mbili kwa pamoja?
 
Wengine kuajiriwa kutamu hawataki hata kuacha kazi .kama unalala bure , kula Bure ,security free na unapata tips na mshahara mkubwa ,huwezi kuacha kazi bhana ,
 
Safi sana,lakin vipi hii tumbua tumbua ya siku hizi? Huoni kama job security imepungua sana?
 
Wengine kuajiriwa kutamu hawataki hata kuacha kazi .kama unalala bure , kula Bure ,security free na unapata tips na mshahara mkubwa ,huwezi kuacha kazi bhana ,
Ajira tamu chache sana.. Nyingi ajira uchwara tu za kukufanya uishi kwa stress!!

Huku kwenye kujisimamia kuna raha yake, niliacha kazi 3yes ago na hakuna ninachojutia... Biashara zimekuwa na nimeajiri vijana pia!!
 
Kipi kinakukwamisha hasa na kujikuta umebaki mwajiriwa.
Na je unapata muda wa kutosha kusimamia kazi yako ya kujiajiri baada ya kutoka kwa mwajiri? Vip ufanis wa kufanya kazi mbili kwa pamoja?
Kama nilivyoeleza mkuu kama hali ikiruhusu ipo siku nitajikuta nakuwa fully self employed. Muda wa kusimamia kazi zangu napata kutokana na aina ya biashara ninazofanya, watu niliowaweka na pia management systems nilizoweka katika kila biashara husika.

Kuhusu ufanisi wa kufanya kazi mbili naona ni kawaida tu kwa sababu naiona, naisimamia na kuichukulia kazi yangu ya kuajiriwa kama aina mojawapo ya biashara zangu. Nikimaanisha kwa vile inanipa riziki na exposure kama ilivyo kwa biashara zangu binafsi, naichukulia kama aina fulani ya sehemu mojawapo ya kuwajibika. Mfano kama nina biashara zangu tatu za binafsi kazi yangu ya kuajiriwa naihesabu kama eneo langu la nne la kunipa riziki kama ilivyo kwa mtu aliyejiajiri jumla kwa kuwa na biashara nne tofauti. Sijui kama nimeeleweka vizuri mkuu?
 
Kwangu mm kutegemea kaz moja kwa awamu hii n kujitakia presha buree kwa ushauri hata kama umeajiriwa kujiajiri ni muhim
 
  • Thanks
Reactions: me1
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom