Kuajiriwa imekuwa utumwa kwasababu elimu hajatukomboa....! Stuka na kujitambua ndugu

Zyamwelele

JF-Expert Member
Aug 5, 2013
405
250
Habarini wanakwetu!!

Nianze kwakusema kwamba ELIMU kwa tafsiri ya kawaida ni ukombozi katika nyanja mbalimbali' ikiwa kifikra, kisiasa, kijamii au kiuchumi. Elimu itakuwa na maana pale tu inapotumiwa kama chachu ya ukombozi!!

Lakini kwa sisi watanzania wengi elimu imekuwa kama fasheni' kwamba mtu anaona ufahari kujulikana yeye msomi au yupo shule anasoma haijalishi ana malengo gani na hiyo elimu anayoitafuta au elimu aliyonayo imemsaidia nini! Hii yakutotambua dhamira ya elimu ndo imetufikisha hapa tulipo' kisiasa, kiuchumi na kifikra!!

Niliwahi kuajiriwa nikiwa nasoma' na kabla sijaamua kuchukua uamuzi wakujiajiri!! Moja yavitu ambavyo vilikuwa vinaiumiza sana nafsi yangu ni jinsi meneja alivyokuwa na kauli mbayambaya kwa wafanyakazi wenzangu' ingawa hii haikuwahi kunitokea mimi'', pia nafsi yangu ilikuwa inasononeshwa na tabia ya meneja kutembea na wadada kwakuwahidi kuwapandisha vyeo na vitisho vya hapa na pale eti kwakuwa yeye ni meneja!! Lo! Nilisononeka na kujiuliza mwenyewe thamani ya elimu tunayoihangaikia ipo wapi? Kwawaliosoma shule za bweni hasa zile za serikali wanafahamu manyanyaso ya shule ingawa si wote walipitia hiyo hali' lakini pia wanafahamu vikwazo vingi tulivyopitia kuanzia unaanza kidato cha kwanza paka cha sita. Sasa ukiwa unatafuta elimu uhangaike tena kwa mda mrefu' ukitoka hapo uhangaike kutafuta ajira' bado umepata ajara bosi wako akunyanyase' kweeli jamani? Thamani ya elimu uliyoitafuta ipo wapi? Pia hata kama unatafuta maisha lini utakuja kufurahia elimu yako na ajira yako? Inauma sana!!

Pamoja na hayo yote' nilichokuja kugundua nikwamba elimu yetu haijawa mkombozi hivyo tumekuwa watumwa kwenye ajira zetu' na hii nikutokana na yafuatayo ÷

1)Tunasoma nakukalili ili tufahuru mitihani.

2)Hatujitambui na kujiamini hivyo hatuoni kwamba elim tuliyonayo ina thamani kubwa kuliko ajira.

3)Ni wavivu wakazi na hatuhangaishi akili zetu hivyo kupenda kuwanyenyekea wakuu wakazi ili wakulee lee!

4)Wengi wetu hawapendi kusoma hivyo sheria za kazi hawazijui ndo maana wanakuwa watumwa. Eti mtu elitaka afundishwe sheria za kazi na sio kuhangaika kuzisoma mwenyewe.

5)Hatufaham haki zetu kama waajiriwa na hii ni kutokana na kutojua sheria za kazi.

6)Mawazo yakimaskini yametawala akili zetu' ndo maana mtu anaona kama bosi wake ndo anampa kula na anasahau kwamba analipwa kutokana na jasho lake.

7)Wengine wanapewa kazi na watu wao' hivyo hata kama mtu anajitambua anaogopa kusimama kwenye haki kwakuogopa kumkweza mtu aliyemsaidia kupata kazi' sasa utakuwa mtumwa paka lini?

8)Wadada mna tamaa nakujirahisisha sana.


Ushauri..

1)Ikiwa upo shule soma ukijua unasoma ili iweje na usihangaikie GPA' tafuta kuelewa! GPA nzuri ni muhimu, lakini GPA nzuri bila chochote kichwani lazima kazi iwe ngum kwako.

2)Kwamlio maofisini tambua kwamba elimu uliyonayo inathamani kuliko ajira yako' kwasababu unaweza kuitumia popote! Pia mahala ulipo kuna watu walikwepo kabla yako wapo wapi? Elim yako itakupa kazi sehem yoyote

3)Mkurugenzi, meneja, na wasimamizi wengine ni waajiriwa kama wewe' kwanini wakuumize kichwa wakatib unatekeleza majukumu yako? Hivyo unapaswa kusimamia haki na ukweli ili uifanye nafsi yako kuwa huru uwapo kazini.

4)Punguza hofu ya maisha' na amini kama ipo' ipo tu na kama haipo' haipo tu! Hii itakusaidia kujiamini.

5)Jitume kazini, jari mda na tekeleza majukum yanayokuhusu kwa wakati' na hii itakuwa siraha yako uwapo kazini.

6)Mtu akikusaidia kupata kibarua asikuendeshe' hasa pale unaposimamia haki na kweli hapaswi kukuingilia. Alitoa msaada tu' lakin msaada wake usiwe fimbo kwako.

7)Wadada jamani tambueni kama miili yeni ni hekalu ya Mungu hivyo inathamani kubwa kuliko chochote msipende kujirahisisha' mwenye mamlaka na mwili wako ni Mwenyezi Mungu na mumeo tu! Kuruhusu kukumbatiana kumbatiana na kubusiana mnamkosea hata mwenyezi Mungu na ndo maana shetani anatumia nafasi hiyo kuwatia majaribuni. Daa inauma sana!!


HITIMISHO!!
Kama umeajiriwa, unategemea kuajiriwa, na utaendelea kuajiriwa'' hakikisha una nakala ya AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI (EMPLOYMENT & LABOUR RELATION ACT) hii itakusaidia sana na amini hatokusumbua wala kukunyanyasa mtu yeyote! Maana wakuu wenu wenyewe wakijua unajitambua na kujiamini wanakuheshimu pia!

Epuka kunyanyasika kusiko na mashiko' na pinga vikali manyanyaso yasiyo na tija, simamia ukweli na hakia!!

Kwa nijuavyo nafasi nyingi za umeneja
na wakurugenzi zimeshikwa na watu wa nje'' sasa huwa unajisikiaje kuona kwamba ndani ya nchi yako mtu anakunyanyasa tena wakutoka nje ya nchi? Inauma sana.

ELMU IWE SILAHA YAKO NA IKUKOMBOE'' EPUKA UTUMWA WA FIKRA'
VINGINEVYO UTAKUFA KWA MSONGO WA MAWAZO KAMA SIO PRESHA.

MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA!!

MAPUMZIKO MEMA WANDUGU..!
 

Zyamwelele

JF-Expert Member
Aug 5, 2013
405
250
Kwabahati mbaya sana waajiri wengi wamashirika binafsi hawapendi wafanyakazi wajiunge kwenye vyama vya wafanyakazi!

Kimsingi kuwa mwanachama wa vyama vya wafanyakazi(TU) ni mhim sana' na wengi hawajui umuhim wake kwasababu matatizo hayajawakuta'' siku yakija kukukuta utatambua na kutafuta mwenyewe vilipo.

Pia kuna kitu kinaitwa TUME YA USURUHISHI NA UPATANISHO (COMMISION FOR MEDIATION & ARBITRATION ''CMA'').

Hivyo ni miongoni mwa vyombo ambavyo vipo kwaajiri ya kutetea maslahi ya wafanyakazi. Hivyo kama wewe ni muajiriwa ni mdau wao, unapaswa kuvijua vizuri na kazi zao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom