mdachi mdachi
Senior Member
- Mar 9, 2017
- 107
- 130
Katika wilaya ya Mbinga kijiji cha Ruanda mkoani Ruvuma ni moja ya sehemu ambayo yanatoka makaa ya mawe mengi
Kumekuwa na utaratibu ambao naona hauko sawa na sijajua ni Serikali inakalia kimya suala hili au ndio utaratibu unaruhusu hivyo
Huko Ruanda kuna makampuni mengi yanachimba mkaa, yapo ya kitanzania na ya kigeni
Tatizo lipo ktk utaratibu wao wa kuajiri kumekuwa na utaratibu wa kuajiri wageni kutoka bara la Asia ktk kampuni moja pale mpaka sasa namba inataka kulingana kati ya wabongo na hao raia wa bara la Asia na kwa taarifa za chini chini ni kuwa wataendelea kuja mpaka basi.
Wanaajiri mpaka kazi ambazo zilitakiwa zifanywe na wazawa mfano mafundi wa magari, mtunza store, ni kitu kisichoingia akilini kwamba hapa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla hatuna mtunza store ama hatuna mafundi wa magari
Kinachonitatiza ni kuwa kazi za ndugu zetu wabongo sasa wanafanya wageni na wanaenda kuijenga nchi yao maana wanalipwa hapa bongo ila matumizi wanaenda kufanya kwao sasa Tanzania kwanza tunakosa manufaa ya mishahara yao na pia watoto wa Kitanzania wanakosa kufaidika na keki ya taifa,
Naomba mamlaka husika ifike kuchunguza suala hili maana tunakoelekea huwenda wanakijiji na wafanyakazi wa kampuni hyo wa kibongo wanaweza kuja kushikana mashati maana wao wakija wanajiona ni mabosi na kuanza kuendesha wabongo watakavyo.
Ama kama sheria zinaruhusu pia naweza kukosolewa kuwa hao wapo sawa hata kama wakiajiri waasia wote wabongo wakabaki wafagia ofisi tu.
Nawatakia Eid njema watanzania wenzangu