Kuahirishwa kwa show za Ipupa: Muziki wake hauvutii japo ana kipaji

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,360
2,000
Duuuh! Koffie Olomide hajui muziki?? Ngoja nisikilize vibao vya Papa Plus, Julia na Petit na London kwanza.
Nikiri wazi na najua wengi hapa wananijua kuwa GENTAMYCINE ni Team JB Mpiana na Bendi yangu pendwa ya Wenge BCBG.

Ila kuacha Unafiki na Chuki napingana na wale wote ambao wanasema kuwa Koffi Olomide hana lolote.

Kuna Mtu ( Member ) nimeona mahala amesema kuwa Koffi Olomide hana lolote zaidi tu ya Kuimba kidogo kwa Kuchomokea ila Kazi kubwa wanafanya wengine.

Jamani mbona hiki anachokifanya Koffi Olomide mnachomponda nacho hata Kipenzi changu JB Mpiana nae anakifanya na hata pia Wanamuziki wengi tu wa Congo DR wanafanya hivyo?

Zamani wakati Koffi Olomide alipokuwa akitunga na Kuimba Nyimbo zote Mwenyewe mlisema kuwa alikuwa ni Mbinafsi akaamua kubadilika na kuwapa nafasi Wanamuziki wake na Yeye kuinba kidogo leo hii mnasema haimbi na hajui Kuimba. Mnataka nini nyie?

Labda kwa Faida ya wengi nitoe Elimu kidogo tu ya Mfumo wa Uimbaji wa hawa Wanamuziki wa Congo DR.

Ni kwamba mara nyingi wale wenye Bendi ( Marais akina Koffi, JB Mpiana, Werrason na wengineo ) katika Nyimbo nyingi Kazi yao kubwa nje ya Kutunga pia huwa ni Kuchomokea 'vionjo' vya maneno huku wakiwapa sana nafasi Wanamuziki wengine Kuimba ili Kuwatambulisha zaidi.

Na hata yale majina mbalimbali ambayo huwa mnasikia yakitajwa ( Mtindo unaoitwa Makanga ) katika Nyimbo zao yana maana zaidi Kibiashara kwakuwa Matajiri wengi wa Congo DR hupenda mno Kutajwa katika Nyimbo ili Kuwaongezea Umaarufu.

Ukisikia Wimbo unaanza halafu jina la Mtu linatajwa jua ameshalipa Dola 1000 na ukisikia Jina la Mtu linatajwa katikati jua amelipa Dola 500 na likitajwa mwishoni jua amelipa Dola 250 huku majina mengine mnayosikia katikati ya Wimbo yale huwa yamelipiwa Dola 100.

Na hivi ndiyo Bendi nyingi Kubwa za Congo DR zinavyojipatia Pesa zaidi achilia mbali zile za Viingilio katika Matamasha yao na ndiyo maana Wanamuziki wengi wa Congo DR ni Matajiri wakubwa sana.

Huku ( hapa ) Kwetu Tanzania ukisikia Watu wanatajwa katika Nyimbo nyingi na mbalimbali jua hawatoi ( hawalipi ) chochote kile sana sana hutoa tu Ofa za Bia kwa Wanamuziki hao au Kuwatafutia Mademu ( Mashuga Mami ) ya Mjini yawape UKIMWI na waamze Kuuana katika Bendi zao.

Koffi Olomide ni Habari nyingine na namuheshimu mno kwani nje tu ya kuwa Mwanamuziki ila pia ni Msomi mkubwa sana mwenye Masters Degree yake ya Biashara achilia mbali Degree yake ya Uchumi na pia ni Mjasiriamali mkubwa mno si tu Congo DR bali duniani.

Cc: Expected Value, Bila bila
 
juma mpemba

JF-Expert Member
Aug 1, 2017
2,860
2,000
Duh kweli fally ippupa anabahatisha ?

Huyo jamaa habahatushi sema wewe una muziki ambao umeuzoea masikion mwako na ndio maana unaona mziki wa fally huupend

Mtu mwenye tuzo za kila aina ambazo wasanii wengi wameshindwa kuzipata ngoma Kama associe Maria bakanja na nyingnezo kibao n ngoma Kali hata Bibi yako kule kaliua anatikisa tako hata

Mkali mwingine n huyu hapa FERE GOLA sikiliza ngoma Kama 100kilos 3eme Vita imana

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Uwiiiij....vocalist bora Congo nzima..fere gola lechante,,,le padre...hatari sana huyu MTU...huyu akianza kuimba hata fally anajificha chini ya kitanda.....fally nae akianza kucheza...wote tunamtazama
 
juma mpemba

JF-Expert Member
Aug 1, 2017
2,860
2,000
Sikatai wadada na wamamama wote mtampenda sana huyo jamaa kwa vitu vingine vinavyowavutia.

Ila huyo ni kiki tu kama za Diamond.
Hata kama akipata tuzo zote ni sawa tu maana hizo tuzo zinachangiwa na kura wanazompigia wadada.Lile uno,na u handsome wake hata akiimba hovyo atapendwa tu.

Ila binafsi muziki wake unani boa sana.
Bora Ferre Gola ana Rhumba nyingi nzuri.

Nyimbo za Fally Ipupa ni kama pishi la nyanya chungu lililotiwa sukari.Hazieleweki
3eme de toit,,100 kilos,,vita imana,,poison de avril,,,paka djuma..vita imana remix..hatari sana free gola
 
mbenda said

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
560
1,000
Nimeona tangazo la kuahirishwa kwa show za Fally Ipupa Dar na Mwanza.Sikusitushwa hasa kwa sababu ana miziki mingi ya kubahatisha isiyo vutia kama ambavyo ukilinganisha na mkongwe Koffi Olomide.

Fally Ipupa zaidi ya urembo na kukata mauno,ana kipaji cha sauti nzuri.
Hata hivyo sauti nzuri,urembo,na kukata mauno vinaweza tu kuwa vivutio kwa wadada na sio wanaume wapenda muziki.

Huyu jamaa niliona kama vile alipata kiki sana kwenye media za nje kama anavyopata kiki Diamond ingawa hana muziki unaovutia.

Kama mtu angetoa laki moja kwenda kwenye show,ni kwa vile tabia ya matajiri kupenda kutafuta sababu ya kukutana na hasa wakisukumwa na ushawishi wa warembo wanaoweza kuhudhuria show.
Wakati huyo Fally Ipupa akifanya show stejini,wengine waliohudhuria wako kwa ajili ya show off tu.

Huyo jamaa angeweza kuwa bora kama angekuwa kwenye kundi la Quarter Latin la Koffi Olomide.Ni sawa tu na ambavyo JB Mpiana hawezi kuwa bora bila wakali wenzie waliokuwa nao Wenge BCBG.
Unamjua ipupa au unamsikia? Hicho chombo kingine mkuuu achana nacho, nenda kaisilikilize original na ngoma zake kibaaaaa, we sikia audio tu.
 
Killboy

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
1,079
2,000
Sasa kama you're this Foolish utaonaje mazuri ya Muziki wa Bolingo wa Congo DR? Hebu kampikie Chai Mumeo awahi Kazini urejee Kitandani kulala na hilo Dela lako kama Puto.
Pole mkuu kwa kukukera ila usilazimishe nipende unachokipenda ww!!naona umeandika kwq mihemuko na mipasho kama bwabwa flan iv linalopakuliwa!ila pole sanaa kila mtu ana hobbies zake
 
TADPOLE

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
1,432
2,000
Nikiri wazi na najua wengi hapa wananijua kuwa GENTAMYCINE ni Team JB Mpiana na Bendi yangu pendwa ya Wenge BCBG.

Ila kuacha Unafiki na Chuki napingana na wale wote ambao wanasema kuwa Koffi Olomide hana lolote.

Kuna Mtu ( Member ) nimeona mahala amesema kuwa Koffi Olomide hana lolote zaidi tu ya Kuimba kidogo kwa Kuchomokea ila Kazi kubwa wanafanya wengine.

Jamani mbona hiki anachokifanya Koffi Olomide mnachomponda nacho hata Kipenzi changu JB Mpiana nae anakifanya na hata pia Wanamuziki wengi tu wa Congo DR wanafanya hivyo?

Zamani wakati Koffi Olomide alipokuwa akitunga na Kuimba Nyimbo zote Mwenyewe mlisema kuwa alikuwa ni Mbinafsi akaamua kubadilika na kuwapa nafasi Wanamuziki wake na Yeye kuinba kidogo leo hii mnasema haimbi na hajui Kuimba. Mnataka nini nyie?

Labda kwa Faida ya wengi nitoe Elimu kidogo tu ya Mfumo wa Uimbaji wa hawa Wanamuziki wa Congo DR.

Ni kwamba mara nyingi wale wenye Bendi ( Marais akina Koffi, JB Mpiana, Werrason na wengineo ) katika Nyimbo nyingi Kazi yao kubwa nje ya Kutunga pia huwa ni Kuchomokea 'vionjo' vya maneno huku wakiwapa sana nafasi Wanamuziki wengine Kuimba ili Kuwatambulisha zaidi.

Na hata yale majina mbalimbali ambayo huwa mnasikia yakitajwa ( Mtindo unaoitwa Makanga ) katika Nyimbo zao yana maana zaidi Kibiashara kwakuwa Matajiri wengi wa Congo DR hupenda mno Kutajwa katika Nyimbo ili Kuwaongezea Umaarufu.

Ukisikia Wimbo unaanza halafu jina la Mtu linatajwa jua ameshalipa Dola 1000 na ukisikia Jina la Mtu linatajwa katikati jua amelipa Dola 500 na likitajwa mwishoni jua amelipa Dola 250 huku majina mengine mnayosikia katikati ya Wimbo yale huwa yamelipiwa Dola 100.

Na hivi ndiyo Bendi nyingi Kubwa za Congo DR zinavyojipatia Pesa zaidi achilia mbali zile za Viingilio katika Matamasha yao na ndiyo maana Wanamuziki wengi wa Congo DR ni Matajiri wakubwa sana.

Huku ( hapa ) Kwetu Tanzania ukisikia Watu wanatajwa katika Nyimbo nyingi na mbalimbali jua hawatoi ( hawalipi ) chochote kile sana sana hutoa tu Ofa za Bia kwa Wanamuziki hao au Kuwatafutia Mademu ( Mashuga Mami ) ya Mjini yawape UKIMWI na waamze Kuuana katika Bendi zao.

Koffi Olomide ni Habari nyingine na namuheshimu mno kwani nje tu ya kuwa Mwanamuziki ila pia ni Msomi mkubwa sana mwenye Masters Degree yake ya Biashara achilia mbali Degree yake ya Uchumi na pia ni Mjasiriamali mkubwa mno si tu Congo DR bali duniani.

Cc: Expected Value, Bila bila
Kuna kipindi bendi zilikuwa zinamtaja sana Kongolu Mobutu mtoto wa Hayati Mobutu..jamaa alikuwa anapenda sifa kama Sabaya vile..sijajua kwa sasa hawa matajiri wanaotajwa ndio wamefulia au vipi maana kina Tchatcho Ombala,Mkubwa shabani,Bebe Ramadhani,Anna Bombole,Monsieur De Congolaise Mabamba pamba pamba,Mustafa Athumani na wengineo hawatajwi kabisa ni kama wamesahaulika hivi
 
lunatoc

JF-Expert Member
Aug 16, 2017
1,309
2,000
Fally Ipupa hana ubora huo mnaomsifia Kutwa isipokuwa anabebwa zaidi na kuwa Kwake 'very handsome' na kujua Kukata Viuno ambapo huwavutia Mashabiki zake wengi ambao 85% ni Wanawake.

Kama ungeniambia kuwa kwa sasa Congo DR Mwanamuziki 'tishio' na 'mahiri' kabisa kwa Utunzi, Uimbaji, Uchezaji na upangiliaji wa Mziki ni Ferre Gola ningekukubalia 100%

Na hata Ugomvi mkubwa baina ya 'Magwiji' Wawili JB Mpiana na Koffi Olomide ulitokana na Kitendo cha Koffi Olomide kuwachukua 'Kimafia' na kwa Bei mbaya Mwanamuziki Ferre Gola na Mpiga Drums Titina Alcapone kutoka Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana.

Na hili Kulithibitisha hilo ndiyo maana Wanamuziki akina Fally Ipupa na Ferre Gola walivyotoka Bendi ya Quarter Latin yake Koffi Olomide kwenda kuanzisha Bendi zao Mtu aliyemuumiza mno Koffi alikuwa ni Ferre Gola na siyo Fally Ipupa kwakuwa tayari katika Bendi kulikuwa na Mtu mwenye Sauti kama ya Fally Ipupa na anacheza kama Yeye aitwae Cardinale Gento.

Baada ya Ferre Gola kuondoka ( kwa Kunyakuliwa Kimafia ) na Koffi Olomide JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge BCBG aliwapata wabadala wake Wawili ambao ni akina ni Rio Biku a.k.a De Jeneiro na pia ana Mtu ana Watu Wawili wenye Sauti inayokaribia Kimfanano kama ya Fally Ipupa waitwao Shai Ngenge ( Mtoto pekee wa Mama Tajiri mwenye Migodi Congo DR ) na mwingine anaitwa Djino Equalizer ambapo huyu Djino hata Fally Ipupa alishawahi Kumvulia Kofia na Kumpigia Saluti kwa Uwezo wake na Kipaji chake Kikubwa alichonacho.
Mtusi tangu lini ukamkubali Fally Ipupa au mkongo.

PUMBAAAAAAAAVU
 
Denis Alphonce

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
303
250
Duuuh! Koffie Olomide hajui muziki?? Ngoja nisikilize vibao vya Papa Plus, Julia na Petit na London kwanza.
Koffie Olomide Hana kipaji asili Cha kuimba lakin ni mtunzi Kwa lugha ingine ni mwandishi mzuri ukaribu alikuwa nao na papaa Wemba ulimfanya aanze kuimba
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,360
2,000
Pole mkuu kwa kukukera ila usilazimishe nipende unachokipenda ww!!naona umeandika kwq mihemuko na mipasho kama bwabwa flan iv linalopakuliwa!ila pole sanaa kila mtu ana hobbies zake
Bwabwa atakuwa ni 'Babaako' tu sawa?
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
8,838
2,000
Unajua watanzania na ulimwengu wa sasa tunatabia ya kushabikia mwanamuziki kwasababu ya followers wake mitandaoni na sio uwezo wake wa kushawishi kupitia kazi zake.

Na ndio maana wasanii wengi wa sasa huwa hawana maisha marefu sababu umaarufu wao ni kutokana na kishabikiwa mitandaoni na makundi ya fans wanafiki.

Nikiwa my nephew, niece na other young blood, huwa wanasikia ngoma ambazo hawazisikii redioni. Na hii huwa inawapa shauku ya kutaka kujua hawa wanaoimba ni akina nani.

Madogo nimewaonyesha video za Michael Jackson, aisee wanavyomuelewa utadhani walizaliwa miaka yake.

Kimsingi wasanii wa sasa wanatumia unafiki wa hawa mashabiki feki kujinufaisha na kuua mziki mzuri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom