#COVID19 Kuagiza chanjo ya Covid-19 kabla ya kutoa elimu kwa raia ni matumizi mabaya(Misallocation)

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
666
Mapokezi ya chanjo ya COVID19 nchin sio mazuri, mikoa mingi wana chanjo nyingi zimebaki na watu hawajitokezi kuchanja. Hali hii inataka nchi kujitafakari namna bora ya kuwashawishi wananchi ili wakubaliane na chanjo au waweke ulazima wa kupata chanjo hiyo kwa kuweka vikwazo mbalimbali kama kutopata huduma nk.

Katika hali isiyo ya kawaida nchi inaahidi kuleta tena dozi milioni 2 wakati milioni 1 ya mwanzo bado tunahangaika nayo, inawezekana tunakopeshwa au tunapewa bure au ni sharti la kupata mikopo mingine lakini kama tunatumia fedha za wananchi ni matumizi mabaya kuchukua chanjo hizi kabla ya kuelimisha watu ili zigombaniwe na kuonekana ziko chache watu wazichangamkie.

Ushauri wangu kama tunahisi chanjo ni muhimu kwa nchi, tuanze kwa kuwaelimisha wananchi ili ziwe muhimu kwao, otherwise ni kupoteza rasilimali na nguvu ambazo tungeziweka kwenye mambo yenye muitikio hali ingebadilika.
 
Haitasaidia.

Kuna maswali mengi kuhusu janga lenyewe na kwanini kipaumbele kimewekwa kwenye chanjo hata kwa makundi ambayo yako salama.

Hii biashara ya chanjo haitafanikiwa sana japokuwa itapiga hatua nzuri tu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom