Kuachwa kimya kimya na kuachwa kwa kutamkiwa kupi kunaumiza zaidi?

Hiyo ipo sana unakuta mtu alishakuacha mda ila hataki kukuweka wazi ili yeye asiwe sababu ya kuachana kwenu kwahiyo anangoja ile point mwenzie atakapoitoa hiyo sababu ili aonekane yeye hakuamua iwe hivyo. Inakera mtu hakupendi, hakuhitaji tena lakini bado anakung’ang’ania haachi mawasiliano nawewe sijui target huwa ni nini? Kwa sababu haiwezekani umpendi/umhitaji mtu lakini bado iwe ngumu kwako kuacha mawasiliano nae, ni nini hasa huwa kinalengwa kwenye kuendeleza mawasiliano?
Hili limenigusa kwakweli
 
Mimi upande wangu niliachwa taratibu nakuja kustuka time is too late moyo wangu yaani

Step ya kwanza nilishangaa tuu kuona mpenzi wangu amekuwa mkali ghafla kwangu nikawa navumilia sikuchulia manani

Step ya pili nilianza kuona jambo dogo tunagombana au kidogo ugomvi.

Step ya tatu nilianza kushanga anabadilika tabia ukimuuliza tatizo nini ananiambia kuna kitu hakipo sawa akiwa fresh ataniambia

Step ya nne nilishangaa kila siku nimekuwa mtu wa kukusolewa yaani unashanga anakukosoa jinsi ulivyo kitabia na mwonekano basi nikawa mtu wa kuomba samahani na kubembeleza

Step ya tano alianza kunikalia kimya hanitafuti mawasiliano yakawa hafifu

Step ya Sita mkiwa ktk maongezi kila unachokiongea wewe hakitiliii manani hata ukiongea nae anaona unamchosha

Step ya saba kitu kidogo mkipishana anakimbilia kusema tuachane

Step ya nane Akawa ananiponda tuu kupitia madhaifu yangu akawa ananiona mie kama kituko au kichefufu

Ilivyofikia hio hatua nikagundua huyu haniitaji tena nilichokifanya niliamua kumove on kimya kimya ila nashukuru tuliachana kwa amani
Ulionesha ukomavu ila mara nyingi ndio namna ambazo wanatumia wanawake wa kibongo wakishapata pa kujiegesha.
 
Hili limenigusa kwakweli

Ndivyo ilivyo kwa wengi unajua ni bora ambae hakupendi/hakuhitaji kuchukua yeye hatua dhidi yako kwa sababu hana cha kupoteza kuliko wewe mwenye upendo kufanya hivyo tena bila kuwa na uhakika kama ni kweli au la. Love hurts asee sasa naamini one night stand ni bora kuliko kujiweka na kujitwisha majukumu kwa mtu mmoja ambae inafika mda haioni thamani yako.
 
Linapokuja swala la kuachwa au mtu wa kukuacha kuna staili mbili

1. Kuna mtu anakuacha kimya kimya bila kukwambia sikutaki

Watu wa aina hii yeye anakuoneshea vitendo visa vitakavyo kufanya wewe ugundue huyu mtu hanitaki tena nijiongeze

2. Kuna mwingine anakuacha kwa maneno

Watu wa aina hii yeye anakutamkia live hakutaki hahitaji kuwa na wewe kila mtu Achukue hamsini zake

Mimi upande wangu kuachwa kimya kimya ndo naumia zaidi kwani hujui kama unapendwa au laa unajikuta upo ndani uhusiano karibu miaka 3 kumbe mwenzio alishakuacha miaka 3 iliopita
Tafuta na umiliki pesa hutaachwa yaani ukiinua simu tu mchepuko unakuja ulipo, wewe kama unataka kila siku utamkiwe I love set, hny, nk unapoteza muda wako na utaumia zaidi
 
Nimewai kuachwa kimya kimya, nikahamua ku move on, siku nakutana nae hakuamini alitegemea atanikuta nimepauka....nikaja kuonana nae tena nikiwa mjamzito hapo ndo alichoka kabisa alinitafuta kwenye mtandao wakijamiii nakuanza kulalamika bila sababu nikampotezea sikumjibu.
 
Nimewai kuachwa kimya kimya, nikahamua ku move on, siku nakutana nae hakuamini alitegemea atanikuta nimepauka....nikaja kuonana nae tena nikiwa mjamzito hapo ndo alichoka kabisa alinitafuta kwenye mtandao wakijamiii nakuanza kulalamika bila sababu nikampotezea sikumjibu.
Wanaume wengi wakiacha Wanawake huwa wanafurahi ukiharibikiwa Ila ukipendeza roho huwa inawauma kweli
 
Wanaume wengi wakiacha Wanawake huwa wanafurahi ukiharibikiwa Ila ukipendeza roho huwa inawauma kweli
Yaani aliavoanza kulalamika nikashangaaa huyu si alihamua kunipotezea monyewe huyuu....sa hivi anatuma tu msg zake huko dm sijawai mjibu hata mara moja
 
msimamo ndio kitu muhimu kuliko kuua moyo kila siku na mwishoe mnaachana,unakuta kila siku ugomv maneno hakuna amani lakini moyo unavimba kwamba uendelee yatapita ukweli haya ni mapito mabaya kuliko yale ya firauni.nilichogundua kibongo kuachana huwa inachukuwa muda kuliko kutongozana yaani mwanamke au mwanaume hataki kukubali kwamba ITS OVER!hadi aje akufumanie ndio aamini
 
Wanaume wengi wakiacha Wanawake huwa wanafurahi ukiharibikiwa Ila ukipendeza roho huwa inawauma kweli
Kuna mwanamme mmoja alioa dada wa rafiki yangu. Huyu mwanaume ni katili sana mchagga wa maeneo ya Kibosho nyie wachagga mnajua huko. Alimtelekeza na pacha wa kike mmoja mlemavu. Yule dada aliteseka sana na ninakumbuka tulimchangia pesa kupeleka huyo pacha mmoja India kwa matibabu. Baadaye yule dada alitulia akaja kupata kazi nzuri maisha yakawa poa sana na kwa sasa ninafikiri ni millionnaire. Ukimuona hutaamini ni mwanamke over 50s. Huyo mkibosho ni mtumishi wa Benki Kuu. Nilikutana na rafiki wa yule dada akaniambia huyo mkibosho hata hajawahi kuwaona wale watoto kwa miaka 20 na ukoo wa huyo dada uliamua kuwaasili. Daahh mwanaume kama huyu sijui ni jini au pepo. Kuna siku nilionyeshwa na jamaa nikamtizama kwa saikolojia yangu nikiona ana roho ya kinyama sana. Unamkimbiaje Mlemavu unamwachia mke unakimbizana na house girl? Unabwaga house girl kwa aibu unakimbizana na cheap women?
 
Hiii imenikuta mimi nasema hivii nilipogundua

Hapa sina changu tena niliamua kukaa kimya yaani kukaa kimya ilivyopita week moja nae yupo kimya nilibadili namba zangu zote za simu ila

Baada ya miezi mitatu nilishangaa Ex wangu sijui kaitoa namba yangu alinipigia akaniambia naomba tuonane nahitaji tuongee basi mtu mzima bila kujitafakari si nikaenda doh sikuamini kumbe ndo nilikuwa nakuja kupigwa kibuti rasmii
Ungejua hata usingeenda😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom