"Kuachiwa Kwa Babu Seya" Makamba,Polepole,Shaka,Dr.Slaa mnakumbuka mlichosema?

Kapilipoint

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
381
343
Wanasiasa kuweni na akiba ya maneno.Kumbukeni Kamanda Lowassa amewatangulia kuijua Siasa, Katiba ya nchi anaijua, Ikulu amekaa kwani Waziri Mkuu Ana ofisi pale hakukurupuka kusema atamwachia Babu Seya aliisoma katiba.
 
ed819637d848b3fee454e6b85e5fd571.jpg
 
TUJIKUMBUSHE

TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM) KWA VYOMBO VYA HABARI.
_______________
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama hicho walihudhuria, wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha ambao walihutubia mkutano huo wa ufunguzi.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kupitia ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku.

Lowassa akiwa anatetemeka jukwaani na kuongea kwa taabu amelizungumzia suala ambalo tayari *mahakama ya rufaa imekwisha litolea hukumu. Suala hilo ni kesi ya Mwanamuziki Nguza Vicking na mwanawe Johnson Nguza waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji*.

*Mahakama imedhibitisha kuwa Nguza Vicking maarufu kama "Babu Seya" na mwanaye Johnson Nguza maarufu kama "Papii Kocha" ni *WABAKAJI, *WANAJISI na *WALAWITI*. Na hivyo wamehukumiwa *kifungo cha maisha gerezani kutokana na tabia hizo chafu katika jamii*.

*Lowassa anakuja na hadithi ya kuwaachia huru, kana kwamba anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza*. Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha. Mbakaji hawezi kupewa msamaha wa Rais. *Msaidieni Lowassa maana anaonekana haijui sheria*.

Tangu *nchi* imepata *uhuru*, hakuna *Rais aliyewahi kutoa msamaha kwa wabakaji, wala walawiti*. Lowassa anaonekana kuchanganyikiwa. Ni dhahiri kwamba CHADEMA na mgombea wao Lowassa hawajajipanga kuongoza nchi. Hawana hoja za kuwasaidia watanzania, badala yake wanategemea siasa za matukio ili kujipatia kura. Tunaomba watanzania muwapuuze.

Imetolewa na:

Shaka Hamdu Shaka,
Kaimu Katibu Mkuu - UVCCM Taifa na Mjumbe wa NEC.
30 August 2015.
 
Ndio tabia za wanasiasa, nakumbuka Chadema walivyokuwa wanamshambulia Lowassa alipokuwa CCM, alipohamia kwao lugha ikabadilika
 
Wanasiasa kuweni na akiba ya maneno.Kumbukeni Kamanda Lowassa amewatangulia kuijua Siasa, Katiba ya nchi anaijua, Ikulu amekaa kwani Waziri Mkuu Ana ofisi pale hakukurupuka kusema atamwachia Babu Seya aliisoma katiba.
Hili limepita,bado la kumrudisha Daudi Balali nchini,ili kuthibitisha dhana ya urais wa mioyo ya watanzania.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom