Kuachiwa huru kwa Freeman Mbowe na wenzake hakuna sababu nyingine isipokuwa ushahidi wa Jamhuri kutothibitisha mashitaka

Hutomsikia tena anaongea Jambo la katiba mpya

Hata asipoliongelea tutaliongelea sisi maana sio Mbowe anatulazimisha kudai katiba mpya. Kama unadhani tunamsubiri Mbowe ili kudai katiba mpya basi umepotea. Tena anatakiwa akae kimya ili tuidai, kuliko yeye aendelee kuidai na kuishia kubambikiwa kesi.
 
Hahahaha sasa Kaka shida yenu mnadai kwenye jf Tu

Ilitakiwa tuwaone mko road
 
Nani alishangalia viongozi wa dini kumuombea Mbowe msamaha, acha upotoshaji wa kijinga. Tulisema kabisa Mbowe hana kosa lolote la kuombewa msamaha. Na kama ni kuachiwa sio kwa sababu ya maombi ya viongozi wa dini maana hawakutumwa na cdm bali wao waliamua kivyao baada ya kuona ushahidi wa kihanithi wa serikali huko mahakamani, ama kwa kupangwa na serikali. Mtu anayeijua haki yake hawezi kuiomba Boss, wala kutuma mtu yoyote akamuombee msamaha. Sasa hivi tunaangalia kwanini Mbowe ameenda ikulu haraka hivyo, na tunataka kuona mwelekeo wake baada ya kukutana na rais, akilegeza msimamo tu ajue hatuko naye tena.
Maccm yanaweweseka
 
Hahahaha sasa Kaka shida yenu mnadai kwenye jf Tu

Ilitakiwa tuwaone mko road

Kwenda barabarani ni moja ya mbinu, ila zipo nyingi mno, na dunia hii ya technology, mitandao ya kijamii ni njia muhimu. Huenda ww ni mzee hivyo bado unaamini mbinu za kizamani tu, jiongeze boss. Zamani ili upate elimu ilikuwa lazima uende darasani physical, sasa hivi watu wanapata degree, PhD nk kupitia online studies na kinaeleweka.
 
Nakuelewa Sana but sio Kwa watu wa chadema hii,
 
Wadai fidia kama ni hivyo.
ASIKUDANGANYE MTU, kwa propaganda yoyote kuwa DPP kutangaza kutokuwa na nia ya kuendelea na mashitaka ya tuhuma za ugaidi na uhujumu uchumi dhidi ya M/Kiti wa CHADEMA - Taifa ndugu Freeman A. Mbowe na wenzake eti ni kwa sababu zingine zozote zile bali ilikuwa ni suala la muda tu siku hii ifike.

ASIKUDANGANYE MTU, kuwa ule ugeni wa wanaoitwa "viongozi wa dini" ikulu na kauli ya Zito Kabwe siku chache zilizopita kule Dodoma wakati wa kilichoitwa "mkutano wa Mutungi - Msajili wa vyama vya siasa kwa mwavuli wa TCD" iliyozua tafrani ya kumwombea msamaha zina influence yoyote kwa maamuzi ya DPP leo kuiondoa kesi hii mahakamani.

Yote na kote huko ilikuwa ni harakati za serikali kutafuta mlango wa kutokea tu ili kuliondoa jambo hilo mahakamani kwa sababu kila mtu aliona kwa macho na kusikia kwa masikio yake kutoka day one kuwa hakukuwa na ushahidi wa kuthibitisha mashitaka hayo.

ASIKUDANGANYE MTU, kuwa kesi hii ilikuwa ni jinai kweli kwa maana ya jinai. Huu ulikuwa mchezo na mkakati wa kisiasa wa CCM kwa mgongo wa SERIKALI dhidi CHADEMA chama kinachotishia uhai na uwepo wa CCM madarakani.

Kilichofanyika ni CHADEMA kukutwa wamejiandaa vyema kukabiliana na mkakati huu mwovu wa CCM na serikali yao.

ASIKUDANGANYE MTU bwana, kwa mchezo huu ambao waasisi ni CCM mwenyewe, CHADEMA ni washindi na wamewachapa goli za kutosha CCM na kwa aibu wakawa wametafuta mbinu ya kuumaliza mchezo apema kuepuka kushindiliwa magoli zaidi.

NARUDIA TENA, ASIKUDANGANYE MTU, kuwa kule kuwaona kina Zitto Kabwe na hawa wanaoitwa "viongozi wa dini" wakiokotezwa na kisha wakatengenezewa mazingira na kukaribishw Ikulu ili wajifanye kumsihi Rais kumsamehe Freeman Mbowe ili hili lililofanyika leo ionekana ni kwa sababu "Rais Samia kawasikia viongozi hao".

USIDANGANYIKE na hayo maigizo. Ni uongo mtupu wa kufuta aibu ya malkia na serikali yake.

ASIKUDANGANYE MTU, wote tunaelewa serikali yoyote ikiwemo hii yetu ya JMT chini ya Rais Samia Suluhu [CCM] huwa madarakani kwa mlango wa siasa na hu - mantain uwepo wake madarakani kwa mbinu za kisiasa zozote zile iwe halali ama haramu.

Katika hili la kesi ya Freeman A. Mbowe ilikuwa mbinu haramu na pengine ya kijinga na kipumbavu sana ya serikali hii chini ya CCM kujaribu kuji - maintain lakini bahati wameshindwa spectacularly.

Kwa kuwa ilikuwa mbinu haramu matokeo yake hata mikakati [strategies] zao zikawa za kijinga na kipumbavu kabisa.

Mathalani, kitendo cha Rais Samia kwenda kufyatuka uongo wa mchana kweupe akihojiwa na kituo cha TV cha BBC Swahili kuwa baadhi ya wahalifu wenzake na Freeman Mbowe walishahukumiwa na kufungwa gerezani ilikuwa uthibitisho wa kwanza wa wanamikakati (strategists) wa CCM kushindwa kabla ya mkakati kufikia hata robo tu.

CHADEMA hongereni. You are the winners. I see the light at the end of the tunnel. Keep on going. Harakati za kudai katiba bora na mpya, demokrasia na haki ziendelee.
 
Ushahidi ulikuwa dhaifu na wa hovyo.

Imelazimu Mbowe aachiwe huru, na aitwe ikulu kuombwa msamaha, na kupewa pole.
Siyo ushahidi dhaifu bali washtaki hawakuwa na ushahidi wowote kwa sababu hapakuwahi kupangwa/kutendwa uhalifu wowote na washtakiwa.
That was a CRAP!
 
Mimi kinachonishangaza ni kwa nini jaji asingemaliza mchezo kwa kusema hawana kesi ya kujibu na mchezo ukaishia pale??
Wanatengeneza tatizo halafu wanajifanya kulitatua ili wajipatie political mileage,hayo ni maigizo ya siku zote ya CCM wakiona maji ya shingo.
Tumewakamata!
 
ASIKUDANGANYE MTU, kwa propaganda yoyote kuwa DPP kutangaza kutokuwa na nia ya kuendelea na mashitaka ya tuhuma za ugaidi na uhujumu uchumi dhidi ya M/Kiti wa CHADEMA - Taifa ndugu Freeman A. Mbowe na wenzake eti ni kwa sababu zingine zozote zile bali ilikuwa ni suala la muda tu siku hii ifike.

ASIKUDANGANYE MTU, kuwa ule ugeni wa wanaoitwa "viongozi wa dini" ikulu na kauli ya Zito Kabwe siku chache zilizopita kule Dodoma wakati wa kilichoitwa "mkutano wa Mutungi - Msajili wa vyama vya siasa kwa mwavuli wa TCD" iliyozua tafrani ya kumwombea msamaha zina influence yoyote kwa maamuzi ya DPP leo kuiondoa kesi hii mahakamani.

Yote na kote huko ilikuwa ni harakati za serikali kutafuta mlango wa kutokea tu ili kuliondoa jambo hilo mahakamani kwa sababu kila mtu aliona kwa macho na kusikia kwa masikio yake kutoka day one kuwa hakukuwa na ushahidi wa kuthibitisha mashitaka hayo.

ASIKUDANGANYE MTU, kuwa kesi hii ilikuwa ni jinai kweli kwa maana ya jinai. Huu ulikuwa mchezo na mkakati wa kisiasa wa CCM kwa mgongo wa SERIKALI dhidi CHADEMA chama kinachotishia uhai na uwepo wa CCM madarakani.

Kilichofanyika ni CHADEMA kukutwa wamejiandaa vyema kukabiliana na mkakati huu mwovu wa CCM na serikali yao.

ASIKUDANGANYE MTU bwana, kwa mchezo huu ambao waasisi ni CCM mwenyewe, CHADEMA ni washindi na wamewachapa goli za kutosha CCM na kwa aibu wakawa wametafuta mbinu ya kuumaliza mchezo apema kuepuka kushindiliwa magoli zaidi.

NARUDIA TENA, ASIKUDANGANYE MTU, kuwa kule kuwaona kina Zitto Kabwe na hawa wanaoitwa "viongozi wa dini" wakiokotezwa na kisha wakatengenezewa mazingira na kukaribishw Ikulu ili wajifanye kumsihi Rais kumsamehe Freeman Mbowe ili hili lililofanyika leo ionekana ni kwa sababu "Rais Samia kawasikia viongozi hao".

USIDANGANYIKE na hayo maigizo. Ni uongo mtupu wa kufuta aibu ya malkia na serikali yake.

ASIKUDANGANYE MTU, wote tunaelewa serikali yoyote ikiwemo hii yetu ya JMT chini ya Rais Samia Suluhu [CCM] huwa madarakani kwa mlango wa siasa na hu - mantain uwepo wake madarakani kwa mbinu za kisiasa zozote zile iwe halali ama haramu.

Katika hili la kesi ya Freeman A. Mbowe ilikuwa mbinu haramu na pengine ya kijinga na kipumbavu sana ya serikali hii chini ya CCM kujaribu kuji - maintain lakini bahati wameshindwa spectacularly.

Kwa kuwa ilikuwa mbinu haramu matokeo yake hata mikakati [strategies] zao zikawa za kijinga na kipumbavu kabisa.

Mathalani, kitendo cha Rais Samia kwenda kufyatuka uongo wa mchana kweupe akihojiwa na kituo cha TV cha BBC Swahili kuwa baadhi ya wahalifu wenzake na Freeman Mbowe walishahukumiwa na kufungwa gerezani ilikuwa uthibitisho wa kwanza wa wanamikakati (strategists) wa CCM kushindwa kabla ya mkakati kufikia hata robo tu.

CHADEMA hongereni. You are the winners. I see the light at the end of the tunnel. Keep on going. Harakati za kudai katiba bora na mpya, demokrasia na haki ziendelee.

Umepiga mule mule, pekechee! Alokwazika akajinyonge.
 
Sasa Kama aliachia watuhumiwa wa ugaidi lukuki wenye ndevu nyingi na makubazi miguuni angeacha kumwamchia huyo mtuhumiwa mmoja wa tuhuma Kama hizo hizo za wenye ndevu nyingi na makubazi miguuni akaeleweka kweli?
 
Back
Top Bottom