Kuachana na siasa kwa Dr. Slaa Watanzania tunajifunza nini?

Mlyamimbo

Member
Oct 24, 2014
59
125
Tukielekea krismas ya pili tukiwa bila Dr. Slaa katika siasa za Tanzania je watanzania tunalakujifunza?

Ni ukweli usiyopingika kwamba Slaa ni miongoni mwa nembo kubwa katika siasa za Tanzania. Nimekaa nikatafakari na kujiuliza maswali mengi sana juu ya maisha ya Slaa kabla na baada ya kuachana na siasa za misimamo ya kutetea watanzani majukwaani.

Miongoni mwa maswali niliyojiuliza:
Je baada ya slaa kuachana na siasa kunachochote amepungukiwa?
Je kipindi Dr.slaa anawatetea watanzania tena kwa kujitoa kwa gharama ya uhai wake tulikuwa tunamlipa Nini?

Baada ya kujiuliza maswali hayo cjapata majibu ya kutosha, nikaamua kuachana na slaa kwani nimeanza kuingiwa na hofu kubwa sana na kuwaza zaidi.
Wanaforum wezangu hivi siku Moja Lisu, Mbowe, MNYIKA, MDEE, LEMA na wengine wote wanaotokea hadharani kukemea serikali wakiamua kujiweka kando hali itakuwaje?,

Kunaumuhimu wakuwasupport watu hawa kwani nimegundua they fighting for majority, nimegundua hata siku wakikaa Kimya hawatapungukiwa na kitu chochote bali maisha yao yataendelea kustawi na familia zao kama Slaa.
 
Tanzania Njema Yaja

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,052
2,000
Mabadiliko yapo tu. .... hata hao ulio wataja wakikaa kimya bado wapo watao kuja kupaza sauti zao.... kuna watu ni wakereketwa tu kama Tundu Lisu tangu enzi zile anaongelea tunavo ibiwa madini kwenye TV, kama kina Che Guevera vile.... tunawashukuru sana hao ambao bado wanapaza sauti kwa ajili yetu na tunaomba waendelee lakini hata wasipo kuwepo, wapo
watakao chukua nafasi zao.....
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,499
2,000
Maandamano ya kijinga yasiyokuwa na faida yamepungua sana,

na ukiona mtu kajiweka pembeni jua kapata alichokuwa anakitafuta, sisi wengine bado tunapambana na mkoloni mweusi hadi uhuru kamili utakapopatikana.
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,471
2,000
Una uhakika hao uliowataja wanatetea watanzania?

Nani aliwapa hiyo kazi?
 
Ndyali

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
1,428
2,000
Tukielekea krismas ya pili tukiwa bila Dr. Slaa katika siasa za Tanzania je watanzania tunalakujifunza?

Ni ukweli usiyopingika kwamba Slaa ni miongoni mwa nembo kubwa katika siasa za Tanzania. Nimekaa nikatafakari na kujiuliza maswali mengi sana juu ya maisha ya Slaa kabla na baada ya kuachana na siasa za misimamo ya kutetea watanzani majukwaani.

Miongoni mwa maswali niliyojiuliza:
Je baada ya slaa kuachana na siasa kunachochote amepungukiwa?
Je kipindi Dr.slaa anawatetea watanzania tena kwa kujitoa kwa gharama ya uhai wake tulikuwa tunamlipa Nini?

Baada ya kujiuliza maswali hayo cjapata majibu ya kutosha, nikaamua kuachana na slaa kwani nimeanza kuingiwa na hofu kubwa sana na kuwaza zaidi.
Wanaforum wezangu hivi siku Moja Lisu, Mbowe, MNYIKA, MDEE, LEMA na wengine wote wanaotokea hadharani kukemea serikali wakiamua kujiweka kando hali itakuwaje?,

Kunaumuhimu wakuwasupport watu hawa kwani nimegundua they fighting for majority, nimegundua hata siku wakikaa Kimya hawatapungukiwa na kitu chochote bali maisha yao yataendelea kustawi na familia zao kama Slaa.
Tunajifunza kuwa CCM walifanikiwa kumshawisha Dr Slaa kwa kumtumia Delila aka Mshumbushi kwa hele ndefu sana inayowawezesha kuishi ughaibuni maisha yao yote.
 
mwalwebe

JF-Expert Member
Dec 20, 2015
821
1,000
Mkuu mtu ambaye alikuwa anaishi bongo kwa mihogo halafu kapanda ndege kwenda Canada,katuacha wenzake bado tunakula mihogo hatumuamini tena,sasa anaishi kwa vinono vya Canada.
Akirudi toka Canada,lazima nimpokee JNIA na swali langu nimuulize Dr kama mihogo bado inapanda?
 
Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
5,178
2,000
Maandamano ya kijinga yasiyokuwa na faida yamepungua sana,

na ukiona mtu kajiweka pembeni jua kapata alichokuwa anakitafuta, sisi wengine bado tunapambana na mkoloni mweusi hadi uhuru kamili utakapopatikana.
Sema ...Tutapambana hadi MAFISADI yaliyofukuzwa CCM na kuinunua CHADEMA yatakapoitwaa tena nchi yetu.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,726
2,000
Katika siasa kuna kupokezana vijiti na niwazi alipokuwa ameshika kijiti alikuwa na mchango mkuu kwa siasa za upinzani na Chadema. Matatizo yayalitokea pale EL alipohamia CDM ingawa inaonekana Dr alishiriki siku za kwanza lakini kuna kilichotokea na kumfanya ajiweke kando. Lakini hii haimuondolei yale aliyoifanyia CDM. Hata EL alichagua chama chenye nguvu na kwa wakati huo ni CDM ndio kilikuwa imara zaidi na homa ya CCM. CDM kingekuwa hoi EL asingejiunga nao. Katika wajenzi wa CDM huwezi ukapuuza mchango wa Dr. Ni wazi CCM iliingilia kujiweka kando kwa Dr kwa faida ya chama hicho lakini ni ukweli kuwa kuna wakereketwa wa CDM waliomwaga petroli kwenye moto na hivyo kuzidi kumtenganisha Dr na CDM. Na hapa wale wa ulipo tupo wanahusika zaidi-CCM wakatumia mwanya huu nao kuitenganisha CDM na Dr na ndio tukamsikia akiongelea "asset na liability" & na kulinganisha uadilifu wa JPM vs EL. (Kwa kimantiki hapa sikukubaliana nae kama nilivyochangia huko nyuma). Sikumbuki sana kumsikia akiwananga CDM kama chama kama ambavyo sikumbuki kumsikia Mbowe akimnanga Dr kwa lugha walizotumia watu wengine (kwa nini?). Kila mmoja ana madhaifu yake lakini Dr amekuwa mwema zaidi kwa CDM ukilinganisha na Bwana yule le Prof. Naamini bado ana a soft spot kwa CDM na ndio maana "ametulia" huko aliko (Kwa nini asiendelee kuwananga CDM kama ana bifu nao?).
 
Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
5,178
2,000
Mkuu mtu ambaye alikuwa anaishi bongo kwa mihogo halafu kapanda ndege kwenda Canada,katuacha wenzake bado tunakula mihogo hatumuamini tena,sasa anaishi kwa vinono vya Canada.
Akirudi toka Canada,lazima nimpokee JNIA na swali langu nimuulize Dr kama mihogo bado inapanda?
Naye atawauliza bado mnazungusha mikono kama mazuzu? atasikitika kuona umakini wa wanaCHADEMA ulivyoporomoka kwa sasa.
Katufundisha..money is better than loyalty
...of course mkuu. Vinginevyo Lowasa angepitia wapi kuja kuinajisi CHADEMA?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom