Dodoma moja
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 307
- 177
Wasaalam wakuu wa GT naamini mko salama na mnaendelea kupambana na majukumu ya kujiingizia kipato.
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza, mimi ni Mtumishi wa Umma ambaye natarajia ndani ya muda mfupi ni step down kwenye Utumishi wa Umma kutokana na kukosa muda wa kufanya mambo yangu binafsi ya kimaisha ambayo naamini kama nitayasimamia vizuri na kuonyesha juhudi kwenye kazi yataniongezea kipato kulinganisha na hiki ninachokipata sasa kwenye utumishi wa umma.
Mambo ni mengi lakini kubwa ni kwamba utumishi wa umma umenifanya nikose uhuru lakini pia ni kazi zenye fitina, manyanyaso mengi na kunyenyekea watu na kwa nature huwa sina tabia ya kumnyenyekea mtu au kujipendekeza kwa mtu hilo kwangu ni mwiko.
Hivyo ili kuyaepuka hayo nimeamua kuachana na kazi ingawa najua nje ya ajira kuna changamoto nyingi lakini nitapambana nazo ikiwa ni njia ya kutafuta uhuru wa kujiamulia mambo yangu mwenyewe na si kupangiwa na mtu hivyo nipo tayari nasema nipo tayari narudia tena nipo tayari ila changamoto iliyonifanya nililete suala hili JF ni kupata uzoefu kwa watu walioachana na utumishi wa umma wakiwa wanadaiwa na Benki kutokana na mikopo ya watumishi.
Je, nini kitatokea endapo nitaamua kuondoka angali bado nadaiwa maana kwa sasa nina mkopo na Benki ambao utamalizika baada ya miaka 3.
Asanteni. Naombeni mawazo yenu wakuu lakini nitoe tahadhari naomba yawe mawazo ya kujenga kama huna la kushauri unaweza kupita kimya kimya si lazima ukoment chochote.