Kuacha na kuachwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuacha na kuachwa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nyani Ngabu, Jun 2, 2010.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Jun 2, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Moja ya vitu vibaya sana katika mahusiano ya kimapenzi ni kuachwa na mpenzi wako (to get dumped). Mbaya zaidi ni pale unapoachwa kwa ghafla bila hata kuona dalili. Unastukia tu mwenzako anakata mawasiliano. Hakupigii tena simu. Ukimpigia yeye hapokei. Ukimwandikia waraka wa elektroniki (email) hakujibu wala nini. Haya yote yanatokea siyo kwamba kapotea na hakuna anayejua yuko wapi. Unajua yupo kabisa na jumbe zako zote unajua anazipata lakini hazijibu kwa makusudi tu.

  Pole pole fikra za kuachwa zinaanza kukujia kichwani. Mara unaanza kushikwa na machungu moyoni. Unajiuliza mengi lakini hupati majibu. Unaanza kujiuliza pengine labda kuna kitu ulimkosea....unajiuliza weee hadi kichwa kinaanza kukuuma lakini hupati jibu. Hukumbuki hata kidogo kama ulimkosea kitu maana mara ya mwisho mlipokuwa wote kila kitu kilionekana kuwa shwari na mkaagana vizuri tu kama ilivyo desturi yenu.

  Mwishowe unakuja kustukia tu kuwa umeachwa na hiyo ndiyo hali halisi na ndiyo ukweli wenyewe. Nguvu zinakuishia mwilini. Maumivu unayasikilizia kuanzia kwenye moyo hadi tumboni. Maisha unaanza kuyaona kama hayana thamani tena. Hata hamu ya kula inaisha. Unajiuliza hivi kwa nini mimi (why me).

  Mdau, umewahi kuachwa au kumwacha mpenziyo? Kama uliwahi kuachwa ulijisikiaje na ulikabilianaje na hali hiyo? Ulilia? Ulijikaza tu kisabuni hadi ukapoa? Na kama umewahi kumwacha mpenziyo, ulimwacha achaje? Ulimwambia au ulitimka tu kimya kimya na yeye akaja kustukia baadaye?
   
 2. T

  Tall JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.SI USTAARABU KUMWACHA MTU GHAFLA .....KUNA MADHARA MENGI.
  2.UNAWEZA KUMWACHA MTU TARATIBU....HASA WAAFRICA.
  3.KABLA HUJAMUACHA MTU KWANZA TAHMINI ANAKUPENDA KIASI GANI.BAADA YA HAPO UTAJUA NAMNA YA KUMUACHA.
  4.WAPO WANAOACHANA KWA UGOMVI MATUSI, KASHFA VIPI NYIE?HAIFAI na ni aibu
  5.KUMBUKA KUWA MTU WAKO UNAEMPIGA CHINI LEO ANAWEZA VURUGA HUKO UNAKOENDA kuweni wastaarabu.
   
 3. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
   
 4. bht

  bht JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  NN unaamka asbh unajihisi kum=miss sana umpendaye unaamua kumwambia mara jibu linakuja aaaaaah hata mi nimekumiss sana lakini nimeoa last week!!!!!!!!

  experience za kuachwa with no indicators ni mbaya sana!! u might end up doing something very stupid.
  kidonda chake kigumu kupona, atahri zake huwa za muda mrefu saaana jamani!!
  kitamu wewe unakiona shubili
  una kuwa na vita against the whole world, kila mtu mbaya tu kwako......
  .............................why am I recalling this???????????
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ehheeee shosti..endelea....
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mamii jamani mi sitaki kukumbuka kichwa kinaniuma afu naweza nikaanza kupunguza mapenzi yangu kwa Bala bure.....

  hata ukikutana na mwanaume mwingine unahisi ndo wale wale tu maana mashairi yao vina na mizani ile ile tu!!!

  kuachwa kusikie redioni na usome kwenye magazeti tu, yakikufika utajuuuuuuuuuta kupenda!!!
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Bora kugombana kidogo sio ili utimize kuwa dalili za mvua ni mawingu
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Kuacha kubaya sana;

  Niliyemuacha sikupata nafasi ya kumwomba msamaha na sintoipata kwani aliji:HEHE ..........................nadhani nimeeleweka.:angry:
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  unaona sasa mnyalu................ni kitendo hatarishi sana kwa maisha ya mtu atii!!
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Nimeisoma hii mara mbili mbili na nilipomaliza kuisoma nikabaki nasmile :smiling: tu maana nilidhani imeandikwa na mimi hahahahahahaha:behindsofa: ukitulia huwa unaandika vitu vizito sana. Maelezo yako jinsi unavyojisikia unapoachwa au kudhani umeachwa ni 100% accurate ndiyo maana nikakugongea kitu.
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Jun 2, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  MJ Pole sana masikini......... jamani kuna maamuzi mengine huwa tunayatake for granted. Pole MJ
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Jun 2, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mimi nafikiri nimeshawahi kuachwa mara mbili hivi lakini sikujisikia chochote yaani nilikuwa nadhani siamini kwa sababu waachaji walikuwa wanaacha na kurudi!! Sasa sijui niliachwa au la ila tu nilikuwa naona mabadiliko and then nikichunguza nakuta wameshaanzisha mahusiano mapya mwengine sasa nikiamua kukata mawasiliano kabisa wanarudi mbio kama wamefukuzwa huko walikokuwa walikokwenda !!
   
 13. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Nilijifunza somo moja kubwa sana maishani! nyie acheni tu! Lakini naamia huko aliko amenisamehe! I take comfort in that!
   
 14. bht

  bht JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160

  amini umesamehewa MJ
   
 15. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nimeacha kabisa kuingia kwenye mahusiano ambayo nina uhakika hayatadumu. Sitaki tena kumwacha mwanamke, ilishatokea lakini nafikiri ilikuwa lazima itokee lakini inaleta machungu sana. Ni mbaya kuacha na kuachwa ingawa sometimes huwa inabidi lakini jamani
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine huwa nahisi
  mimi labda hata mapenzi yenyewe siyajui.......
  Mimi mwanamke akiniacha huwa najisemea moyoni....\
  wait till i become a billionaire.....my laugh will come last....
  How stupid i am....
  Wanasema mwanamke akikuacha it means u r not a good enough..
  Mostly financially......
  But offcourse kuna mengineyo yanachangia.....
   
 17. j

  jimy Member

  #17
  Jun 2, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona hii topic inatuhusu wengi?
   
 18. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ktk mahusiano yangu NN nimeacha mara mbili na zingine zote nimetemwa. Kutemwa kwingine kulikuwa kuchungu kuliko uchungu wenyewe kuliambana na KASHFA na MATUSI. Samahani staki kukumbuka hayo matukio, ni hatari.
   
 19. Bang'a

  Bang'a Member

  #19
  Jun 2, 2010
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman kuna watu wanaakili kuliko kuwa clever. sijapost entry siku nyingi sana. nakuja hv:
  kuachwa au kuacha, hiv vitu tujitahid kuvifanya kwa mazungumzo ya pamoja, kwan mwenzenu niliachwa halafu kwa mbwe mbwe kibao,, lakin baada ya muda wa miaka miwil familia ya aliyeniacha walipata shida na mkombozi ni mimi kutokana kaz ninayofanya. je nisaidien kabla sijawambia what i did. je ningefanyeje, nimsaidie kutatua shida ama niponde za kichwa?????????????????:angry::painkiller::yuck:
   
 20. Bi. Senti 50

  Bi. Senti 50 JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 291
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  pole!!!!!!!!
   
Loading...