Kuacha mapaja wazi hakuwezi kumvuta muoaji kamwe bali wazee wa kuchungulia tu

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
2,087
2,193
Miongoni mwa vitu adui amefanikiwa zaidi kwa kina dada ni suala la mavazi, amewaacha waende kanisani lakini amewazuia wasivae vazi la Utakatifu na kuwapa mawazi ya kikahaba. Wasichana wengi hudhania ya kuwa mwanaume ambaye ni muoaji anavutiwa na kumwonyesha mapaja au maungo yake ya Siri kumbe ipo kinyume kabisa.

Wasichana/Wamama wamejikuta watumwa na kuamua kuvalia mavazi ambayo hayastili miili yao kikamilifu, wakiamini ni Kiungo Cha kumvuta mwanaume kumbe ni Kiungo Cha kuvuta pepo wa Kiume ili wapate kumchezea na kumwacha.

Hebu fikiria mtu anasema ameokoka na anampenda YESU KRISTO, lakini anasema akivaa mavazi yenye kustili mwili wake vyema huwa ANAWASHWA. Hali hii ni hatari kwa mtu ambae anajilisha upepo kuwa ni mwenda Mbinguni.

Kuuweka wazi mwili wako Dada wa wazi hadi kuonyesha sehemu zako za Siri ambazo unapaswa uzione mwenye na Mumeo, ni kiashiria kuwa umemdharau kwa asilimia zote Roho Mtakatifu, ambapo mwili wako ni Hekalu lake.

1 Wakorintho 6:19
"Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe.

Yapo mavazi ya waenda Mbinguni na mavazi ya mawakala wa Shetani, maana kila tabia/tendo utendalo humtambulisha yule umfanyiae kazi kwa bidii zako.

2 Wakorintho 3:3
"Mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama."

Dada/Mama, usiifatishe namna ya Dunia hii maana mavazi mengine ni Ukahaba, na ndio maana tangu umeanza kuvaa nguo ambazo hazistiri mwili wako Adui amekufungulia mlango wa Mapepo wa Kiume kuwa wanakupenda na kukusifia kila kukicha, lengo ni upotezwe mazima.

Warumi 12:2
"Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu."

Adui analeta kila aina ya Fashion ili hata wateule aweze kuwatoa eneo sahihi na kuwaingiza Kuzimu bila hata wao wenyewe kuelewa.

2 Wakorintho 4:4
images (5).jpeg
images (4).jpeg
images (3).jpeg

"Ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu."

Kupenda Dunia na namna zake ni kujenga uadui dhahiri, unapovaa mavazi yasiyompa Mungu Utukufu ni kujitangazia vita na MUNGU. Nakusihi wewe ambaye huvai mavazi ya kuustiri mwili wako vyema, kupitia ujumbe huu ubadilike na uamue kuachana na tabia za Ukahaba bila wewe mwenyewe kujua.
Fanyika kuwa Hekalu Takatifu la Roho Mtakatifu ili uendelee kuhudumiwa nae.
 
Kama hilo hapo juu na Tattoo ya pistol kwenye paja linaonekana lishamba fulani hivi lilikutana na mabaharia likatestishwa starehe fulani,likasifiwasifiwa kuwa una bonge la shepu likajiona liblackamerican fulani likachora na pistol mapajani huku likisahau linaishi kwenye nchi isiyokuwa na Gang and gun culture.litaishia kugongwa na kuishi kwenye fantasy world.
 
Back
Top Bottom