Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,777
- 41,071
Kwanini tunapenda kuabudu na kusujudu kwenye altare ya watu weupe? Kila kitu kilicho kizuri na cha kuvutia twakiita hicho ni cha "kizungu"! Imefikia wakati kuwa tunashindwa kusikilizana sisi wenyewe hadi mzungu aje atuambie ndio tunasikiliza. Mswahili mwenzako akisema "shuleni zenu zina hali mbaya" tunadhania hana mpango, ila akija mzungu na kusema kitu hicho hicho.. tunapiga magoti na kusema "ni kweli Mr. Johnson!"
Hatuwezi kuendelea mpaka sisi wenyewe tuanze kujiamini na kuona kuwa na sisi tunastahili vitu vizuri. Barabara nzuri si za Kizungu.. shule nzuri si za kizungu.. nyumba yenye maji na umeme, televisheni na bustani nzuri si ya kizungu!! Hivyo vyote vyaweza kuwa vya kiafrika!! Hata makazini, semina ikiandeshwa na mswahili basi wala hatuitilii maanani ila akija Miss Smith na kasemina kake uchwara, au warsha basi wote tunafungua masikio na kusikiliza... kisa na mkasa ati kwa vile yeye ni mzungu!!
Sipendi tena sitaki kusikia kuwa Waswahili hawana mawazo mazuri au hawastahili vitu vizuri!