Ku renew line Tanzania ni kama kusajili kiwanda: Mamlaka chukueni ushauri huu

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,762
4,576
Hivi majuzi nilipoteza simu iliyokuwa na line ya mtandao fulani (sitautaja) kwakuwa ni line inayofahamika zaidi nilitembelea duka la mtandao husika ili wanisaidie kurudisha, baada ya maelekezo mafupi walinielekeza kwenda kituo cha polisi cha kati, polisi nao walinipokea na kuniuliza tarehe ya kupoteza, nikawatajia, wakaniambia niendelee kuitafuta kwa siku 7 nikikosa kabisa ndo niende kupata loss report.

Ikabidi nicheke nikamwambia kamanda jaribu kufikiri kuhusu muda pia, badae akasema sawa ila inabidi tuandike ilipotea siku 7 zilizopita nikakubali akaandika nikahisi nikisha lipia ntakuwa nimemaliza na kurud dukani.
Cha ajabu baada ya kupewa RB na kukamilisha taratibu zote za loss report, polisi walinielekeza kwenda ktk mtaa ninaoishi then mwenyekiti wa mtaa anipe barua ya utambulisho ndipo niende duka la service provider wangu ku renew.

Hapo nilichoka kwakweli.

USHAURI: Taratibu hizi zingefuatwa kipindi cha kusajili line sio ku renew line, hatahivyo kwa maendeleo ya technology kwasasa sidhani kama huu mlolongo unatija, wekeni utaratibu tufanye kilakitu online, unganisheni mifumo yenu na NIDA ili tukifanya vyote online ukitoka nyumbani unaenda dukani kuchukua line yako unasepa.
 
:D:D:D:Dmimi nikipoteza line nanunua nyingine namba muhimu ziko kwa google acc japo kuna baadhi ya watu wanapataga tabu kunipata kutokana na mambo ya kibiashara na kiofisi but haichukuagi mda mambo yanakaa sawa....ni sawa na kupoteza siku nzima au 2 kabisa ili urenew line tu
 
Kuna bandiko hapa JF linasema kwanini Alama ya Kidole isitoshe wakati wa Mamlaka inapohitaji taarifa, bila msaada wa namba ya Kitambulisho cha NIDA?
 
:D:D:D:Dmimi nikipoteza line nanunua nyingine namba muhimu ziko kwa google acc japo kuna baadhi ya watu wanapataga tabu kunipata kutokana na mambo ya kibiashara na kiofisi but haichukuagi mda mambo yanakaa sawa....ni sawa na kupoteza siku nzima au 2 kabisa ili urenew line tu
Sasa kama line ina pesa, unafanya je? Kuna mazingira ambayo ku renew line haikwepeki
 
Wameamua kukusumbua tu,nenda kituo kingine cha polisi,mi nilipoteza sim card ikiwa na kama 480,000.
Nilienda polisi wakanipa fomu baada ya hapo nikaenda vodashop hapo hapo walirenew nikaambiwa mpesa itaanza kufanya kazi ndani ya masaa 48 hadi 72 .

Hao wameamua kukusumbua tu,process yote ilikuwa ndani ya dk 20 maana kituo cha polisi haikuwa mbali na hamna barua yoyote ya serikali ya kijiji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viol,
swadakta, hata mm nlitumia utaratibu huo huo. ni jambo la siku moja tu, japo police huo utaratibu unanzia asubuhi mpaka saa 6 mchana ndo wanakupa loss report
 
Hata siku moja usiende kureport polisi kuwa umeibiwa au umepoteza line, waambie umeichoma moto bahati mbaya kwenye takataka, waambie mtoto ameikuta juu ya meza akaitafuna , etc etc. zaidi ya hapo utaambiwa usubiri uchunguzi,ufungue kesi, etc.]
Halafu usumbufu uliopata kwenye kituo chako kimoja huko kwenu usilaumu mfumo mzima, watu tunarenew line ndani ya nusu saa tu.
 
Wameamua kukusumbua tu,nenda kituo kingine cha polisi,mi nilipoteza sim card ikiwa na kama 480,000.
Nilienda polisi wakanipa fomu baada ya hapo nikaenda vodashop hapo hapo walirenew nikaambiwa mpesa itaanza kufanya kazi ndani ya masaa 48 hadi 72 .

Hao wameamua kukusumbua tu,process yote ilikuwa ndani ya dk 20 maana kituo cha polisi haikuwa mbali na hamna barua yoyote ya serikali ya kijiji

Sent using Jamii Forums mobile app

MPESA ni baada ya masaa 24 tu.
 
Hivi majuzi nilipoteza simu iliyokuwa na line ya mtandao fulani (sitautaja) kwakuwa ni line inayofahamika zaidi nilitembelea duka la mtandao husika ili wanisaidie kurudisha, baada ya maelekezo mafupi walinielekeza kwenda kituo cha polisi cha kati, polisi nao walinipokea na kuniuliza tarehe ya kupoteza, nikawatajia, wakaniambia niendelee kuitafuta kwa siku 7 nikikosa kabisa ndo niende kupata loss report.

Ikabidi nicheke nikamwambia kamanda jaribu kufikiri kuhusu muda pia, badae akasema sawa ila inabidi tuandike ilipotea siku 7 zilizopita nikakubali akaandika nikahisi nikisha lipia ntakuwa nimemaliza na kurud dukani.
Cha ajabu baada ya kupewa RB na kukamilisha taratibu zote za loss report, polisi walinielekeza kwenda ktk mtaa ninaoishi then mwenyekiti wa mtaa anipe barua ya utambulisho ndipo niende duka la service provider wangu ku renew.

Hapo nilichoka kwakweli.

USHAURI: Taratibu hizi zingefuatwa kipindi cha kusajili line sio ku renew line, hatahivyo kwa maendeleo ya technology kwasasa sidhani kama huu mlolongo unatija, wekeni utaratibu tufanye kilakitu online, unganisheni mifumo yenu na NIDA ili tukifanya vyote online ukitoka nyumbani unaenda dukani kuchukua line yako unasepa.
Labda Serikali imeamua kupunguza wateja wa kampuni za simu. Tunarudishwa kwenye enzi za mawasiliano kwa baragumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye kituo chochote makini hizo fomu za loss report huwa sishaandaliwa pale wanaondika tu kilichopotea na saini basi kazi imeisha
swadakta, hata mm nlitumia utaratibu huo huo. ni jambo la siku moja tu, japo police huo utaratibu unanzia asubuhi mpaka saa 6 mchana ndo wanakupa loss report

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unaweza kuta line yako imesajiliwa kwa alama za vidole lkn ukuenda kurenew wanakuambia hbr z loss report
Loss report sawa maana huwezi jua simu inavyopotea kiusalama lazima polisi lazima wae na taarifa hata ikitokea laini yako imetumika kwenye uarifu uwe salama

Habari za mwentekiti ndo siungi mkono
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom