Ku renew line Tanzania ni kama kusajili kiwanda: Mamlaka chukueni ushauri huu

Mi line nilikuwa nayo ila simu ilinyeshewa mvua na line haikuweza tena kusoma. Nilienda Tigo Shop wskasema nitafute loss report. Sikuelewa walikuwa na maana gani hawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
:D:D:D:Dmimi nikipoteza line nanunua nyingine namba muhimu ziko kwa google acc japo kuna baadhi ya watu wanapataga tabu kunipata kutokana na mambo ya kibiashara na kiofisi but haichukuagi mda mambo yanakaa sawa....ni sawa na kupoteza siku nzima au 2 kabisa ili urenew line tu

Imagine umepoteza laini na kuna pesa kwenye laini uiacha na kukununua laini nyingine?,kweli bangi ipigwe marufuku


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi majuzi nilipoteza simu iliyokuwa na line ya mtandao fulani (sitautaja) kwakuwa ni line inayofahamika zaidi nilitembelea duka la mtandao husika ili wanisaidie kurudisha, baada ya maelekezo mafupi walinielekeza kwenda kituo cha polisi cha kati, polisi nao walinipokea na kuniuliza tarehe ya kupoteza, nikawatajia, wakaniambia niendelee kuitafuta kwa siku 7 nikikosa kabisa ndo niende kupata loss report.

Ikabidi nicheke nikamwambia kamanda jaribu kufikiri kuhusu muda pia, badae akasema sawa ila inabidi tuandike ilipotea siku 7 zilizopita nikakubali akaandika nikahisi nikisha lipia ntakuwa nimemaliza na kurud dukani.
Cha ajabu baada ya kupewa RB na kukamilisha taratibu zote za loss report, polisi walinielekeza kwenda ktk mtaa ninaoishi then mwenyekiti wa mtaa anipe barua ya utambulisho ndipo niende duka la service provider wangu ku renew.

Hapo nilichoka kwakweli.

USHAURI: Taratibu hizi zingefuatwa kipindi cha kusajili line sio ku renew line, hatahivyo kwa maendeleo ya technology kwasasa sidhani kama huu mlolongo unatija, wekeni utaratibu tufanye kilakitu online, unganisheni mifumo yenu na NIDA ili tukifanya vyote online ukitoka nyumbani unaenda dukani kuchukua line yako unasepa.
hiyo cha mtoto usiombe ukataka kurenew line ya simu ukiwa Dodoma....duh....ni zoezi gumu sijapata kuona....ni urasimu kwenda mbele mpaka unajiuliza hili ni jiji au kijiji?
 
Back
Top Bottom