Ku nani tanzania!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ku nani tanzania!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMSOPI, Jan 19, 2011.

 1. K

  KAMSOPI New Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matukio ya hivi karibuni nchini hayapaswi kufumbiwa macho ili kulinda mustakabali wa nchi yetu..

  .Tumeshuhudia rushwa ikitawala mchakato mzima wa uchaguzi mkuu
  .Tumeshuhudia malalamiko ya wizi wa kura
  .Tumeshuhudia baadhi ya wagombea ubunge na urais wakilalamikia uchakachuliwaji wa kura
  .Tunashuhudia wafuasi wa Chadema wakipambana na polisi Arusha, na watatu kuuawa kwa kila kinachodaiwa 'kuzima njama za kuteka kituo kikuu cha polisi'
  . Na juu ya yote tunaona majibishano ya viongozi wa dini kuhusu kuhusu mauaji ya arusha.

  Wakati hayo yote yakifanyika najiuliza matendo hayo ni kudhihirisha kukomaa kwa demokrasia nchini, ama ni dalili za mgogoro mkubwa wa kijamii inayoinyemelea nchi! maana hali kama hii ikiachwa kushamiri inaweza kumomonyoa mshikamano wa nchi!

  Ama matukio hayo ni kiashiria kukithiri kwa dhulma, ulafi, na ufisadi ambao unazidi kupanua mipaka ya wenye nacho na wasio nacho?

  Tutafakari kwa pamoja.
   
 2. m

  matawi JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapa penye nyekundu ndo shida kubwa
   
Loading...