Ktk Serekali ya pamoja ya Z'bar hakuna u-ccm/u-cuf ni Ser ya Wz'bar wote kwa maslahi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ktk Serekali ya pamoja ya Z'bar hakuna u-ccm/u-cuf ni Ser ya Wz'bar wote kwa maslahi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 3, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CUF: Hatuwezi kuwalamba miguu Chadema Send to a friend Wednesday, 02 February 2011 20:51

  Hussein Issa na Elizabeth Ernest
  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema hakiwezi kuwalamba miguu viongozi wa Chadema, ili wakubali kushirikiana nao.

  Kauli hiyo, inafuatia baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kunukuliwa na vyombo vya habari juzi akisema hawawezi kushirikiana na vyama vingine vya upinzani bungeni kwa kuwa vyama hivyo vimeungana na CUF ambayo 'imefunga ndoa' na CCM na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

  Dk Slaa alisema Kamati Kuu ya Chadema imeona kuwa chama hicho, hakiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo bungeni.

  Kutokana na hali hiyo, alimuagiza kiongozi wa kambi ya upinzani kuunda baraza kivuli la mawaziri kwa kuwahusisha wabunge wa Chadema pekee. Lakini jana, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Julius Mtatiro alisema mbele ya wanahabari kuwa, chama chake hakiwezi kuilamba miguu Chadema ili ishirikiane nayo kwa kuwa haina faida yoyote kwa CUF.

  "Tunapenda kuwataarifu Watanzania wote kuwa sisi (CUF), pia hatuwezi kuwalamba miguu viongozi wa Chadema kwani jitihada zetu za kuwaambia wafanye kazi na vyama vingine tayari zimegonga ukuta," alisema Mtatiro.

  Alisema mara nyingi Chadema imekuwa na historia ya kusaliti vyama vingine vya upinzani, kutokana na kuwa na uchu wa madaraka. Alisema mwaka 2002 walifikia maamuzi ya kushirikiana kwa vyama vinne vikiwemo Chadema, NCCR na TLP, lengo likiwa kuunga mkono chama chenye nguvu mahali panapofanyika uchaguzi, lakini Chadema ilikataa.

  Alisema tofauti na matarajio ya malengo yao, katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Tunduru NCCR na TLP walijitokeza kuisaidia CUF kwa kuwa huko ilikuwa ni ngome yake, lakini Chadema walisimamisha mgombea wao na kumfanya mgombea wa CCM kushinda bila tatizo. "Chadema walijifanya mapopo, wakasaliti makubaliano yaliyowekwa na vyama vingine, wakati hata tawi hawana kule Tunduru," alisema .

  Alisema hali kama hiyo pia iliwahi kutokea katika majimbo ya Tarime, Busanda na Mbeya vijijini, ambako Chadema walikataa kutoa ushirikiano kwa vyama vingine kama walivyokubaliana na kuamua kusimamisha wagombea.

  Alisema kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Chadema ndiyo inayotakiwa kuunda kambi ya upinzani bungeni, lakini CUF iliiomba Chadema ishirikiane na vyama vingine vya upinzani ili kambi hiyo iwe imara zaidi na yenye nguvu, lakini Chadema walikataa suala hilo kwa maelezo kuwa wao hawako tayari kuungana na CUF na vyama vingine ikiwa havitashirikiana na CUF.

  "Jana Chadema wametoa kauli ya kinafiki eti wao hawawezi kushirikiana na chama kinachoongoza Dola yaani CUF, na kwamba wapo tayari kushirikiana na vyama vingine.

  " Chadema ni chama popo sana, hawajui wanachokifanya, wamelewa madaraka na kuchanganyikiwa vibaya baada ya kupata majimbo 20,"alisema Mtatiro.

  Aliifananisha Chadema kuwa ni sawa na mtu masikini sana kuamka ghafla akajikuta tajiri, hajui namna gani atatumia utajiri wake na kuanza kuwatukana majirani zake alioishi nao kwa shida na raha katika umasikini wake.

  Alisema kitendo cha Chadema kuwashambulia CUF kwamba ni sehemu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, ni dhambi kubwa, kwani Wazanzibar walitaka kuungana na CCM.


  "Chadema wamekuwa waoga mno, wanaiogopa CUF, wanajua CUF inamtandao mkubwa na mbinu ya kujiimarisha bara na hatimaye kuongoza nchi,"alisema Mtatiro.
   

  Attached Files:

 2. T

  Tata JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Mbona CUF haikuwashirikisha wapinzani wengine kwenye mazungumzo na uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar? waache malalamiko yao yasiyokuwa na msingi.
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena, hata sisi tuko na wewe, CUF wajitathmini kwanza kabla ya kuongea, vyama vililalamimka sana kwa hilo la kushirikishwa lakini CUF waji9hisi wao ni wengi kuliko hao waliotaka kushirikishwa CUF walijihisi wanaweza bila ushirikiano kwa sababu ya majority waliyonayo.
  Leo CDM wanatumia the same approach kwa kuwa umekuwa utamaduni lakini CUF wanaanza kulalamika.Huo ni mkuki kwa nguruwe.Wansheria wanatueleza kuwa mazoea hubadilika na kuwa sheria.CDM wametumia approach ya CUF na hivyo CUF wasilalamike kwani wao ndiyo waasisi wa hiyo approach
   
 4. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  hakukuwa na mazungumzo ila CUF walitoa pendekezo ambalo lilipigiwa kura za maoni na wazanzibar ikiwamo wana chadema wachache na hatimae katiba ikabadilishwa baada ya wengi kutaka serikali ya umoja wa kitaifa. Kwa kuwa katiba inasisitiza vyama viwili vikiwa vimetofautiana kwa kura chache na idadi ndogo ya wawakilishi hata CDM wakija kushika nafasi ya pili wataunda serikali ya umoja wa kitaifa kwasababu katiba ndio inataka hivyo!

  Na kadhalika CDM wakija kushinda urais znz wana jukumu la kufanya kazi pamoja na chama kinachokfuatia kuwa na kura nyingi na wawakilishi.

  Sina uhakika lakini nadhani hiyo katiba haijavitaja vyama vinavvyoweza kufanya hivyo ni CCM na CUF tu na haitaruhusiwa vyama vingine kufanya hivyo.
   
 5. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nikweli cuf haikuwashirikicha chama chengine zanzibar kuunda serekali ya umoja wa kitaifa kwa sababu ccm zanzibar ni afroshirazi na cuf zanzibar ndio cuf / mwicho wa yote wzanzibar ni wamoja na mapambano ni kuvunja muungano fake na kuwa huru na nchi yetu ya babu na bibi na nyiyi bara muna haki ya kuwa na nchi yenu ya tanganyika hamukatazwi kufanya hivyo. Na hizo munazo sema mali za wazanzibar zilizoko tanganyika tutawashia nyiyi muziendeleze na boys kurudi nyumbani ktk ardhi yao.
   
 6. n

  ngoko JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkakati mzuri. Mtikila alishasema siku nyingi kuwa Tanganyika haihitaji maexpert toka zenji kuiongoza ( by then Mwinyi alikuwa Rais) nanyi naona mmeliona hilo jema, mnaweza kuandamana kuukataa muungano
   
Loading...