KRA vs TRA: Kwanini Kenya inakusanya kodi mara 3 ya Tanzania

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,326
KRA vs TRA (Kwanini Kenya inakusanya kodi mara 3 ya Tanzania)

KRA: Kenya Revenue Authority

TRA: Tanzania Revenue Authority

Makusanyo (Tax Collection July 2019 to June 2020)

KRA-Kenya: 34 Trillion (Tsh)

TRA-Tanzania: 14 Trillion (Tsh)

Sababu ni hizi hapa.
  • Matumizi duni ya teknologia (ICT) kwa TRA
  • Kodi kubwa kwa walipa kodi TRA
  • Kazi nyingi kufanyika kwa mikono (manual processing)- TRA
  • Walipa kodi kukosa elimu ya walipa kodi: TRA
  • Kukosa ubunifu katika kuongeza walipa kodi (Tax base) : TRA
  • Kukosa uwazi kwenye viwango vya kodi kwa walipa kodi - TRA
Matumizi ya teknologia

Mfano mdogo ni ukilinganisha tovuti ya TRA vs KRA.

Tovuti ya TRA ipo duni sana na siyo tovuti ya karne hii bado ni zile tovuti static ambazo taarifa zake hazibadiliki na hazina umuhimu kwa walengwa .

Mfano.

Home page ya TRA vs Home page ya KRA.

Main menu TRA.


Ukifungua tovuti ya TRA kwanza ubnakutana na mambo yafuatayo
1600289551869.png


Ukweli ni kwamba menu yote ambayo ndiyo memyu kuu haina umuhimu wowote kwa mlipa kodi , hata wanao isimamia hii tovuti sijui wana elimu gani.

Main menu KRA
Ukifungua tovuti ya KRA unakutana na menu ifuatayo
1600289650395.png

Hii umekaa kihusika kabisa kwa mlipa kodi wa aina zote , ukifungua hapa individual unakutana na taarfiza zote na kodi kwa watu binafsi, ukifungua business unakutana na taariza zote za kodi kwa makampuni na taasisi, na investors unakutana na taarifa zote za kodi zinazo husu wawekezaji.

Home page TRA vs KRA

Home page ya TRA
.
Utakutana picha zinazo za wanasiasa, ndege za ATCL, picha ya commissioner general ,picha za barabara etc, hivi vyote havina umuhimu wowote na wala havimusaidii mlipa kodi . Ni mambo ya kizamani sana .. nadhani mkuu wa ICT TRA atakua na miaka zaidi ya 50. Picha ya CG inahusika na nini na walipa kodi.. tovuti imejaa taarifa ambazo hazina mashiko.
1600289864602.png


Home page ya KRA
Unakutana na maelezo ya jinsi ya kutafuta huduma yoyote ya kodi na kuna sehemu una chagua taarfia na huduma unayo itaka (very friendly )
1600289977543.png

Hii ni mifano tuu jinsi TRA ilivyo nyuma katika matumizi ya teknologia katika kurahisisha ukusanyaji wa kodi. Tovuti hii ya KRA inafanya kazi za watu zaidi ya 5000, na uhakika KRA itakua na wafanyakazi wachache kuliko TRA pamoja na kwamba inakusanya kodi mara 3 ya TRA.
1600290063884.png

Kwa ujumla tovuti ya TRA na KRA zina tofauti zifutazo.
  • KRA ina maelezo karibia yote ya aina za kodi na jinsi ya kulipa Pamoja na maelezo mengine ya kumsaidia mlipa kodi mkubwa na mdogo wakati tovuti ya TRA , taarifa ni chache san ana hazija pangwa kiutaratibu kiasi kwamba tovuti haina msaada .
  • KRA kodi karibia zote unalipa kwa kutumia mitandao au una faili kwa kutumia teknologia na ii unapunguza sana rushwa na kubambikiwa kodi sizizo na maana. Mfano Capital Gain tax ambayo Tanzania Tax pengine inayo ongoza kwa rushwa, Kenya una faili online na baada ya muda unapewa risiti online ya kulipia .
  • KRA imejengwa vizuri na ina taarifa ambazo zinamsadia mlipa kodi, zimehuishwa , tofauti na tovuti ya TRA ambayo imejaza taarifa ambazo hazina maana mfano: number of vistors inamsadia nini mlipa kodi, au link za taasisi za kodi ambazo hazipo Tanzania, utadhani hawana kitu cha kuweka kwenye tovuti sasa wanaamua kukusanya chochote na kujaza huko.
Kwa leo niishie hapa, nitamalizia next week.

Naamini department ya TRA mtabadirika, au tafuteni namna mkajifunze kwa wenzenu wa KRA.

Tanzania bado inanafasi ya kufikia walau nusu ya makusanyo ya kenya kama itazingatia matumizi ya tehama na kuaachana na matumizi ya binadamu kwa sehemu kubwa, lakini kwa utaratibu huu wa sasa kenya muda si mrefu itakusanya mara 4 ta Kenya.
 
Pamoja na mengi ninayokubaliana nawe pia suala la Tax base hasa ndio chimbuko la utofauti huu unaouona.

Tanzania taxbase ni ndogo sana na hii inatokana na uchache wa uwekezaji katika sekta nyingi za kibiashara kama viwanda vya kati na vikubwa.

Tukiweza kuifikia Kenya kiuwekezaji hasa kwenye sekta za viwanda na biashara zenye mchango mkubwa na multiplier effect kubwa kwenye uchumi bila shaka utaona utofauti huo unapungua ama kuwapita Kenya kimakusanyo ya Kodi.

Hapa nimezungumzia uzoefu wangu mdogo katika sekta ya kodi na Fiscal policies za nchi hii.
 
TRA imejaa wapigaji wengi, nakumbuka kuna video ambayo Magufuli aliita kikao na wana biashara, wakamfungukia ukweli wote namna huwa wanababaishwa, mtu una biashara yenye mtaji wa Tshs 10,000,000 unapotaka ulipe kodi jamaa wanapiga mahesabu wanakuambia una deni la TRA la Tshs 200,000,000

Unaambiwa ufanye maamuzi, uwape kitita fulani wakurekebishie au ukapambane mbele huko, haya yote aliambiwa rais wenu sijui kama kuna lolote la maana mlilifanya au ile ilikua show tu, tatizo mnapenda maonyesho maonyesho ya kisiasa halafu utendaji zero.

Pia Watanzania hamna desturi ya kupenda kulipa kodi, nilishangaa sana nikiwa Bongo kuona hamna mtu huhangaika kuagiza risiti ya EFD. Sasa hapo mnataka mshindane na sisi kiuchumi, pengo baina yetu litazidi kuongezeka mpaka basi.
 
TRA imejaa wapigaji wengi, nakumbuka kuna video ambayo Magufuli aliita kikao na wana biashara, wakamfungukia ukweli wote namna huwa wanababaishwa, mtu una biashara yenye mtaji wa Tshs 10,000,000 unapotaka ulipe kodi jamaa wanapiga mahesabu wanakuambia una deni la TRA la Tshs 200,000,000
Unaambiwa ufanye maamuzi, uwape kitita fulani wakurekebishie au ukapambane mbele huko, haya yote aliambiwa rais wenu sijui kama kuna lolote la maana mlilifanya au ile ilikua show tu, tatizo mnapenda maonyesho maonyesho ya kisiasa halafu utendaji zero.

Pia Watanzania hamna desturi ya kupenda kulipa kodi, nilishangaa sana nikiwa Bongo kuona hamna mtu huhangaika kuagiza risiti ya EFD. Sasa hapo mnataka mshindane na sisi kiuchumi, pengo baina yetu litazidi kuongezeka mpaka basi.
Tumekubaliana tupunguze mivutano isiyokuwa kuwa na tija. Lengo ni kuonyesha ni maeneo gani nchi ipi inafanya vizuri ili nchi nyengine ijifinze kutoka nchi nyingine.

Katika huu uzi na ule unaohusu bandari ya Dar na Mombasa, watu wamejaribu kuchangia bila ushabiki wa kujisifu au kujaribu kushusha nchi nyingine.

Jambo la kushangaza, wewe umeanza kujisifu na kutoa kashfa kwa Tanzania, jaribu kuwa na busara kidogo. Ukweli ni kwamba, niliomba tupunguze malumbano baada ya kuona Wakenya mumezidiwa katika mijadala mbalimbali, jana yote Wakenya mlipotea kabisa.

Punguza chuki na wivu, kila nchi ina mapungufu yake na mazuri yake, lengo ni kujifunza na kubadilishana uzoefu, sasa wewe unataka kuendeleza malumbano ambayo tayari Kenya mlishaanza kuzidiwa, jaribu kubadilika mkuu.
 
Tumekubaliana tupunguze mivutano isiyokuwa kuwa na tija. Lengo ni kuonyesha ni maeneo gani nchi ipi inafanya vizuri ili nchi nyengine ijifinze kutoka nchi nyingine.

Katika huu uzi na ule unaohusu bandari ya Dar na Mombasa, watu wamejaribu kuchangia bila ushabiki wa kujisifu au kujaribu kushusha nchi nyingine.

Jambo la kushangaza, wewe umeanza kujisifu na kutoa kashfa kwa Tanzania, jaribu kuwa na busara kidogo. Ukweli ni kwamba, niliomba tupunguze malumbano baada ya kuona wakenya mumezidiwa katika mijadala mbalimbali, jana yote wakenya mlipotea kabisa.

Punguza chuki na wivu, kila nchi ina mapungufu yake na mazuri yake, lengo ni kujifunza na kubadilishana uzoefu, sasa wewe unataka kuendeleza malumbano ambayo tayari Kenya mlishaanza kuzidiwa, jaribu kubadilika mkuu.
Tumieni data sahihi sio hizi takataka, halafu Tanzania hatuna chochote cha kujifunza Kenya 🚮🚮🚮🚮
 
TRA kiukweli bado wako nyuma kitendo cha tozo za kodi kutokuwekwa wazi yaani hadi mkaelewane ni ya kizamani, viwango vya kodi ni vikubwa hivyo mnaandaa watu kukwepa na kuendelea na biashara za magendo, angalia kodi za magari wanavokomoa
Inabidi TRA na taasisi nyingine za kukusanya maduhuli ya serikali zibadilike ili tuweze kuongoza uchumi wa EAC na hatimaye kuwa taifa lenye uchumi mkubwa zaidi afrika na dunia kwa ujumla.
 
Nadhani KRA wanainvolve sana technology ili kujaribu kuwavuta watu zaidi kwenye tax bracket ambayo changamoto kubwa kwa hizi nchi zetu ni walilpa kodi wachache.

Hivi maajuzi kra imelauncha mobile app itakayomuezesha mlipa kodi kulipa kodi kwa njia ya simu na services zingine. Hii nadhani inaeza kuwa na impact kubwa kwa kuwa watu wengi wataeza kuitumia kinyume na ilivyokuwa hapo awali ampapo watu wengi waliachwa nyuma.

NEW KRA APP TO ALLOW TAX PAYMENT THROUGH M-PESA


Workers and businesses can file their returns and pay taxes through their mobile phones after the Kenya Revenue Authority (KRA) launched an app for accessing its services in the race to ease duty payments and boost collection.

The Kenya Revenue Authority (KRA) said the app, dubbed KRA M-Service, that will mainly use M-Pesa is aimed at making tax transactions easier and cut the cost of compliance through removal of intermediaries.

The app will also allow taxpayers to file nil tax returns, Value Added Tax (VAT), payroll tax, excise tax and Monthly Rental Income (MRI).
Firms paying corporate tax are exclude from making payments via the app, a pointer that KRA is seeking to ease payment for small taxpayers like shop keepers, landlords and mini traders given M-Pesa has a daily transaction limits Sh300,000.

“KRA M-Service App will expand the tax base by onboarding the informal sector players who cannot use computers,” said KRA Commissioner for Domestic Taxes Elizabeth Meyo Thursday.

Through the App, taxpayers can also register for Personal Identification Number (PIN) and seek Tax Compliance Certificate (TCC).

The informal sector, also known as Jua Kali, is deemed to have limited contact with the taxation system, save for indirect consumption levies and the Jubilee administration had been banking on turnover taxes to plug revenue loopholes.

This prompted the State reintroduced the sales or turnover tax on one percent of revenues in January to capture Small and Medium Enterprises (SMEs).

The sales tax is expected to provide the KRA, under pressure to collect additional revenue, with a fresh avenue for raising taxes from players this segment, the majority of whom have not been paying State levies.
 
Back
Top Bottom