KRA: Mamlaka ya mapato Kenya yapoteza $40m kutokana na wadukuzi

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
10,327
6,849
KRA: Mamlaka ya mapato Kenya yapoteza $40m kutokana na wadukuzi

Mwanamume wa umri wa makamo ameshtakiwa kwa tuhuma za kudukua mfumo wa kifedha wa Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA).

Udukuzi huo unadaiwa kusababisha mamlaka hiyo kupoteza jumla ya shilingi bilioni nne za Kenya (dola 39 milioni za Marekani).

Alex Mutunga Mutuku, ambaye alishtakiwa makosa ya kutekeleza ulaghai kwa kutumia mifumo ya kielektroniki, alikanusha mashtaka hayo alipofikishwa mahakamani Jumanne kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation.

Upande wa mashtaka unadai Bw Mutuku alikuwa sehemu ya mtandao mkubwa wa watu waliokuwa wakiiba pesa kutoka kwa taasisi na kampuni kubwa nchini Kenya.

Alidaiwa kutekeleza makosa hayo kati ya Machi 2015 na Machi mwaka huu.

Kwa mujibu wa gazeti la Standard, wakili wa upande wa mashtaka Edwin Okello aliambia mahakama: "Sakata hii ni kubwa na inahusisha hata watu walio nje ya nchi."

Polisi waliomba azuiliwe kwa muda zaidi kuwawezesha kukamilisha uchunguzi.

Mahakama itaamua iwapo ataachiliwa huru kwa dhamana Machi 28.

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom