KPA starts moving Equipment from Mombasa port to Lamu port

Tony254

JF-Expert Member
May 11, 2017
16,017
16,427
Kuna malazy waliokuwa wakisema kwamba Lamu port ni white elephant. Sasa sijui watajificha wapi maana equipments zimeshaanza kupelekwa Lamu port sasa hivi tunavyozungumza. Wameze wembe tu hamna namna.

NEARING COMPLETION​

KPA begins moving equipment to Lamu port​

State officials assess new port's readiness for opening on June 15.​

In Summary
  • KPA has subcontracted Comarco, a leading marine and specialised contractor, to move equipment to Lamu.
  • The first three berths of the planned 32 berths have been completed at a cost of about Sh40 billion.
by CHARLES MGHENYIChief Correspondent, Coast Region
Coast
22 April 2021 - 22:00
  • 2021-04-22-kpa-begins-moving-equipment-to-lamu-port

rkIh135Lx5hMMVZWfSD90-a1-xrcqPugucp0H8wxOW02JXqCrYDs-ybVBtpjkhHCqnahWSo8oLXNUFRcL4gKOPO--cOjHvS-JPlvmFnP=s750

HEAVY EQUIPMENT​

A crane lifting containers from the Standard Gauge Railway within the Port of Mombasa on 20 April 2021.

LABAN WALOGA

Kenya Ports Authority has started moving heavy equipment from the Port of Mombasa to Lamu Port, which is over 240km from the coastal city, the management has confirmed.

On Wednesday, Treasury Cabinet Secretary Ukur Yatani, KPA acting managing director Rashid Salim and senior government and port officials toured the Lamu port to assess its readiness ahead of the official opening on June 15.

Yatani also toured the Port of Mombasa to check the equipment that will be sent to Lamu and to oversee other administrative issues at the parastatal.

The first three berths of the planned 32 berths have been completed at a cost of about Sh40 billion. The China Communication Construction Company has been at the site since 2015.

KPA has subcontracted Comarco, a leading marine and specialised contractor, with over 40 years of experience, to move the equipment in two shipments from Mombasa to Lamu.

“Yes, a special team that is handling the equipment will be at the Port of Mombasa to start the loading exercise,” said Bernard Osero, KPA’s head of corporate affairs.

According to other KPA officials handling the shipment exercise, Comarco and Port of Mombasa engineers will start loading the first shipment on Saturday and Sunday.

“The first ship will leave the Port of Mombasa on Monday and will be in Lamu on Tuesday,” said a senior official at the centre of the operation.

He said the first shipment will be for equipment that do not need stable loading and offloading. “Not very sensitive equipment,” he said.

He said currently, the Indian Ocean is very rough because of the south-east monsoon winds, therefore the second shipment of sensitive equipment will be done on May 6.

On the first shipment, the official said, they will be moving four terminal tractors, eight skeletal trailers, two forklifts, two low-bed trailers, four lateral mark buoys and assorted lifting equipment.

On May 6, KPA will transport the sensitive equipment that require stability.

They will be loading two rubber-gantry cranes, one Kenya Revenue Authority scanner, two mobile cranes and other equipment needed for the operation of the facility.

“Tentatively, we expect to begin operations before the official date of June 15,” said the official.

Two giant shipping lines, Maersk and Express, have already shown interest in using the Lamu Port, according to KPA.
 
Nyuzi kama hizi huwezi kuwaona malazy humu. Dawa ni chungu hawataki kumeza.
 
Tunamshukuru Rt. Hon Raila Odinga kwa uzalendo wake wa kuhakikisha kwamba wazo la bandari ya Bagamoyo lilimtoka kabisa kichwani swahiba yake mwendazake JPM.
Hongera sana kwake kwa juhudi na ziara zake Chato za kumnong'onezea comrade mwenzake 'siri kubwa' kuhusu bandari ya Bagamoyo na hasara ambayo ingeiletea nchi ya Tz. Yote kwa faida ya nchi ya Kenya na bandari ya Lamu.

Habari kama hizi kuhusu kufunguliwa rasmi kwa bandari ya Lamu ni sawa na kukorogea zege kwenye kaburi la wazo lote kuhusu mradi wa bandari ya Bagamoyo. Good stuff, nyang'auism hoiyeee! Zitto Kabwe alitabiri kwamba siku Kama hii itawadia. Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda
 
Soko la huduma ya bandari lipo wapi? Uganda hawawezi tumia Lamu port, South Sudan, Ethiopia sahau kabisa.
Muwache ulofa wakupeleka vyombo vya bandari lamu kutoka Mombasa zinapo hitajika, heri hata mnunue vipya..Hata reli ya Naivasha IPO pamoja na bandari kavu lakini hakuna mzigo hata shehena moja..
Nchi inaendeshwa kijuha
 
Pole sana akili maji. We understand your pain.
 
Soko la huduma ya bandari lipo wapi? Uganda hawawezi tumia Lamu port, South Sudan, Ethiopia sahau kabisa.
Muwache ulofa wakupeleka vyombo vya bandari lamu kutoka Mombasa zinapo hitajika, heri hata mnunue vipya..Hata reli ya Naivasha IPO pamoja na bandari kavu lakini hakuna mzigo hata shehena moja..
Nchi inaendeshwa kijuha
Tulizia maumivu pembeni jombaa uone karata zinalivopangwa hadi zikapangika. Bandari ya Lamu itakuwa na uwezo wa kupakua mizigo kutoka kwa meli kubwa hadi kwenye meli ndogo. Meli ambazo ndio zitakuwa zikielekea kwenye bandari zingine ndogo barani Afrika, upande huu wa bahari ya Hindi.

Wewe endelea kuwaza kwa maumivu mengi kuhusu Rwanda, Burundi sijui DRC wakati hata bandari za Tanzania pia zitalazimika kuwa wateja wakubwa wa bandari ya Lamu.

Sasa hivi shughuli za kupakua meli kubwa zinazotokea Ulaya na China. Ili mizigo isafirishwe kwenye meli ndogo kupitia bahari ya Hindi hadi kwenye bandari za nchi za Afrika, zikiwemo Beira na Durban pia, huwa zinafanyiwa kwenye bandari za Singapore na Salalah, Oman.
 
Wacha ujinga. Kama hujui kitu ni vizuri kunyamaza. Eti unasema kwamba bandari kavu ya Naivasha haina container hata moja? Uko serious kweli? Fanya research yako kwanza kabla ya kuja kupost vitu ambavyo havieleweki huku.
 
Tunamshukuru Rt. Hon Raila Odinga kwa uzalendo wake wa kuhakikisha kwamba wazo la bandari ya Bagamoyo lilimtoka kabisa kichwani swahiba yake mwendazake JPM.
Hongera sana kwake kwa juhudi na ziara zake Chato za kumnong'onezea comrade mwenzake 'siri kubwa' kuhusu bandari ya Bagamoyo na hasara ambayo ingeiletea nchi ya Tz. Yote kwa faida ya nchi ya Kenya na bandari ya Lamu.

Habari kama hizi kuhusu kufunguliwa rasmi kwa bandari ya Lamu ni sawa na kukorogea zege kwenye kaburi la wazo lote kuhusu mradi wa bandari ya Bagamoyo. Good stuff, nyang'auism hoiyeee! Zitto Kabwe alitabiri kwamba siku Kama hii itawadia. Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda
Nimesoma hio message ya Zitto. Ni message kali sana. Nimependa hio message yake.
 
Nasubiri Bandari Kubwa ya Lamu izuie Bandari Ndogo za Dar na Mombasa: Namna Maarifa Madogo Yanavyoiua Bandari ya Bagamoyo na Kuifaidisha Kenya

Kumekuwa na mijadala mikali kuhusu Mradi wa Eneo la Kiuchumi la Bagamoyo. Mjadala huo wenye malumbano ya kurushiana shutuma umekuwa mjadala mbovu sana kwenye jambo nyeti la kiuchumi Kama vile Mradi wa Bagamoyo SEZ. Wanaounga mkono wanaona fursa za maendeleo katika Mradi, wanaopinga wakiona hasara nchi itapata. Wanaopinga wanawashutumu wanaounga mkono kuwa wanataka kuuza Nchi.

Kundi la wanaopinga linaongozwa na Rais John Magufuli, Spika wa Bunge ndg. Ndugai mwanzoni alikuwa kinara wa kuunga mkono Mradi kwa hoja nzito zenye nguvu. Lakini baadaye alisalimu amri kwa hoja dhaifu sana na hivyo kujisalimisha kwa Rais Magufuli kwenye hoja nyepesi zilizojaa woga na zisizo na tafakuri yenye mwono mpana wa Uchumi wa Jiografia.

Sasa inadhihirika kuwa Rais Magufuli anatumika dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maslahi ya Jamhuri ya Kenya. Nitafafanua.

Kila nchi ina picha kubwa katika mambo inayotaka kuwa (a grand vision). Picha hiyo kubwa inapaswa kuzingatia mazingira ya nchi husika (context) na namna ya kuyatumia mazingira hayo kufikia hiyo picha kubwa. Tanzania na Kenya ni nchi ndugu ndani ya familia ya Afrika Mashariki. Nchi hizi pia ni Nchi shindani kiuchumi. Ni nchi pekee za Afrika Mashariki ambazo zote zina pwani ya Bahari (access to the sea). Lakini Tanzania ina Pwani ndefu zaidi kuliko Kenya na hivyo kuipa fursa kubwa zaidi.

Nchi zote mbili zinapakana na nchi ambazo hazina pwani. Kenya inapakana na Ethiopia, Sudani Kusini na Uganda. Tanzania inapakana na Uganda, Malawi, Zambia, Kongo DRC, Burundi na Rwanda. Tanzania ina fursa zaidi kuliko Kenya kutokana kupakana na Nchi nyingi zaidi. Kenya kwa muda mrefu imekuwa ikishika biashara ya nchi inazopakana nazo na isizopakana nazo pia. Tanzania imekuwa ikisuasua kufaidika na nafasi yake kijiografia katika kushika biashara ya eneo hili la maziwa makuu. Miji inayoongoza ushindani wa Biashara wa nchi hizi ndugu ni Mombasa na Dar es Salaam. Ni miji ya Bandari, yote ikitawaliwa na Sultan wa Zanzibar wakati fulani na baadaye wababe wa Vita za Dunia Uingereza na Ujerumani kugawana miji hiyo - Mombasa kwa Waingereza na Dar es Salaam kwa Wajerumani.

Hata hivyo Bandari zote hizi 2 zimekuwa ni Bandari za mizigo inayopita (transit goods) kwa kuwa vina vyake ni vidogo hivyo kuweza kupokea Meli ndogo tu. Meli kubwa kutoka China hufika Singapore na kupakua mizigo kuweka kwenye Meli ndogo zinazokuja kutia nanga Mombasa au Dar es Salaam. Meli kubwa kutoka Ulaya hushusha mizigo kwa Meli ndogo huko Bandari ya Salalah, Oman. Ili kuwezesha Meli kubwa kufika Pwani ya Afrika Mashariki, Nchi ndugu za Kenya na Tanzania zikaanza kuwaza na kuwazua miradi ya kufanya ili kuwa Kituo Kikubwa cha Biashara ya Bahari Eneo la Afrika Mashariki (transshipment hub). Mzozo wa kimkakati ulianzia hapo katika ya Nchi rafiki Kenya na Tanzania.

Jamhuri ya Kenya ilitumia diplomasia ya Hali ya Juu kuunganisha Nchi za Rwanda, Uganda, Ethiopia na Sudan ya Kusini kwenye Mradi wa picha kubwa wa Bandari ya Lamu. Ikazaliwa kinachoitwa ‘Northern Corridor’. Tanzania ikatengwa katika Afrika Mashariki (EAC) kikaanzishwa kitu kinaitwa ‘Coalition of the Willing’. Kenya wakazindua kwa fujo Mradi wa Bandari ya Lamu ili kuwa Bandari ya Meli kubwa za Afrika Mashariki. Marais wa nchi zote za coalition of the willing za EAC na nje ya EAC walikusanyika huko Lamu kuanzisha Mradi huo.

Uongozi wa Awamu ya Nne wa Tanzania chini ya Rais Jakaya M Kikwete nao wakaamua kutumia mtaji mkubwa wa diplomasia aliouacha Mwalimu Nyerere kujibu mapigo. Mapigo ya Lamu ni Bagamoyo. Rais Kikwete akafanikiwa kuwashawishi Rais Xi Jinping wa China na Sultan Qabos Bin Said wa Oman kuisadia Tanzania katika mpambano wa kuishika Bahari ya Hindi. China na Oman wakakubali kuanzisha Mradi mkubwa wa kituo cha Meli katika Afrika na Eneo Huru la Uchumi pale Bagamoyo. Mradi wenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 10.

Rais Jakaya Kikwete alifanya kosa analolijutia, naamini, mpaka sasa. Aliondoka madarakani bila kutia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi. Makosa haya yanaigharimu Nchi sasa kwani ushindi wa kuimiliki na kuitawala Biashara ya Bahari ya Hindi upande wa Magharibi umekwenda Kenya bila hata risasi moja kurushwa. Mradi wa Bagamoyo umehujumiwa. Umekufa.

Baada ya Utawala wa Awamu ya Tano kuingia madarakani waliokuwa ‘coalition of the willing’ wakajisogeza karibu. Rwanda ikatangaza kuegemea Central Corridor. Tanzania ikabadili mpango wake wa Kujenga Reli kutoka Dar es Salaam kupitia Uvinza mpaka Musongati nchini Burundi na sasa ikaamua kuielekeza reli Isaka kwenda Rwanda. Badala ya Uvinza kuwa Kituo cha Biashara na Mizigo kwa Nchi za Maziwa Makuu, Sasa itakuwa Kigali, Rwanda.

Rwanda tayari imefungua Kigali Logistics Platform na Bandari huru ya Masaka (Kigali) yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 35. Bandari hiyo itaendeshwa na Kampuni kubwa duniani ya kuendesha Bandari iitwayo Dubai World. Kwa mkakati huu Rwanda itabeba mzigo wote kutoka DRC na kuhudumiwa kupitia Kigali, na hivyo Uvinza (Kigoma) kujifia kwa kukosa Biashara. Tanzania imepoteza kwa Rwanda.

Kenya kwa upande wake ilianza vibaya mahusiano yake na Tanzania ya utawala mpya. Katika hali ya kuweka maslahi ya nchi yao mbele wanasiasa wa Kenya waliamua kuungana katika kile kinachoitwa ‘handshake’, na ndugu Raila Amolo Odinga akapewa rasmi kazi ya kuhakikisha anasimamia hiyo diplomasia ya Kenya inafanikiwa. Propaganda kali dhidi ya Bagamoyo zikaanza na safari za Raila kuja kuonana na Magufuli zikawa nyingi pengine wakikutana Chato na pengine kwa Siri.

Baadhi ya watendaji wakanyweshwa sumu za ubovu wa mkataba wa Mradi wa Bagamoyo (ambapo hapakuwepo na Mkataba). Serikali ya Awamu ya Tano ikatamka rasmi kuwa hawataki Mradi ule kwa sababu za kitoto kabisa, kwani walitumia nyaraka za majadiliano na Mwekezaji. Spika wa Bunge alipoinua sauti yake akanyamazishwa. Vyombo vya Habari vikalishwa sumu na Mradi ukanuka. Msemaji wa Mradi wa Bagamoyo siku zote ni Wizara ya Viwanda na Biashara, lakini ghafla Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) ndio ikawa ndio Msemaji badala ya Wizara. Na baadhi ya Watendaji wa Serikali wenye mwono wa mbali walipotoa mawazo yao wakaondolewa kwenye nafasi zao.

Baada ya mradi wa Bagamoyo kuuawa, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akapewa tuzo na nchi yake kwa kuifanya Kenya kuwa mtawala wa Bahari ya Hindi, tuzo ya ‘Maritime Champion of the Indian Ocean’. Na Rais Kenyatta akawa rafiki ya karibu ya Rais Magufuli. Nchi yetu ikiwa imepoteza miaka minne sasa bila kutekeleza mradi wa Bagamoyo.

Ujenzi wa Bandari yenye kina kirefu ya Lamu sasa kuzinduliwa rasmi Novemba, 2019. Sasa Lamu itapokea Meli kubwa za 4th Generation kama vile Suezmax, Neo-Panamax na Chinamax. Mizigo kutoka Meli kubwa itashushwa Lamu na kupakiwa kwenye Meli ndogo kuja Bandari ya Dar es Salaam na kwenda Bandari nyengine za Afrika kama Beira na Durban. Hii ndio kazi ilikuwa ifanywe na Bandari ya Bagamoyo - Mradi ambao umehujumiwa. Pia Kenya wameamua kuchukua mpango mzima wa Bagamoyo na kuutekeleza Lamu kwa kuanzisha Eneo Maalumu la Uchumi. Hapo kabla ilikuwa iwe Lamu Port Pekee.

Watawala wetu wameonyesha uwezo mdogo sana wa kung’amua mambo na kujikuta kuwa sehemu ya Hujuma kwa Nchi yetu. Faida ya kijiografia ya nchi yetu ambayo Mungu alitupa tumeipoteza. Baadhi ya watu wanashangilia ujinga huu wa kiuchumi ambao tumeufanya bila kujua. Shida kubwa ya watu wenye mamlaka ya Dola katika nchi yetu hawasomi kujiongezea MAARIFA ili kuepuka hujuma dhidi ya nchi yetu, hujuma ambazo zitaathiri vizazi na vizazi.

Tumepoteza fursa ya nchi kwa sababu za kitoto, zisizo na maana na za kipropaganda tu. Kuendesha bandari miaka 99 mara tunataka miaka 33 haiwezi kuwa sababu kwa mtu mwenye akili timamu wakati Mradi ni Joint Venture na Serikali ni mbia mwenye hisa zinazotokana na ardhi yake. Kuna mwekezaji atabeba ardhi ya Tanzania kuipeleka China au Oman? Eti Bagamoyo itaua Bandari ya Dar es Salaam, kwa hiyo Ujenzi wa Bandari ya Lamu utaua Bandari ya Mombasa? Nasubiri kuona Bandari ya Dar ikifa kwa sababu ya ujenzi wa Bandari ya Lamu.

Biashara ya Bandari ya Bagamoyo ingekuwa kwa Meli kubwa kuleta mizigo na Meli ndogo kuja kubeba kupeleka Bandari za Afrika nzima kazi ambayo haifanywi na Dar es Salaam na wala haitaweza kufanywa kwa sababu Eneo la Bandari ya Dar ni dogo. Kazi ambayo sasa itafanywa na Bandari ya Lamu.

Hujuma hii kwa Jamhuri ya Muungano haipaswi kupita bila kulipiwa. Rais Magufuli na Serikali yake wanapaswa kulipa gharama ya hujuma hii kwa Nchi yetu. Wasipolipia watakuja Viongozi wengine kuhujumu nchi yetu kama hawa. Wakiadhibiwa itakuwa somo kwa wengine. Kwa uelewa mpana kuhusu Uchumi wa Bahari soma Gazeti la The East African la October 26 - November 1, 2019: Inside Kenya’s plan to rule EA Coast.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto

Mbunge - Kigoma Mjini

Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo

Oktoba 28, 2019

"Ukweli haupendi kupuuzwa puuzwa" - TUJISAHIHISHE, Nyerere 1962.
 
Tulizia maumivu pembeni jombaa uone karata zinalivopangwa hadi zikapangika. Bandari ya Lamu itakuwa na uwezo wa kupakua mizigo kutoka kwa meli kubwa hadi kwenye meli ndogo. Meli ambazo ndio zitakuwa zikielekea kwenye bandari zingine ndogo barani Afrika, upande huu wa bahari ya Hindi.

Wewe endelea kuwaza kwa maumivu mengi kuhusu Rwanda, Burundi sijui DRC wakati hata bandari za Tanzania pia zitalazimika kuwa wateja wakubwa wa bandari ya Lamu.

Sasa hivi shughuli za kupakua meli kubwa zinazotokea Ulaya na China. Ili mizigo isafirishwe kwenye meli ndogo kupitia bahari ya Hindi hadi kwenye bandari za nchi za Afrika, zikiwemo Beira na Durban pia, huwa zinafanyiwa kwenye bandari za Singapore na Salalah, Oman.
Panamax and post Panamax ships have a very high ETA..Because the only way they can make profit is on long voyages. So forget about those landing in lamu unless they are coming from the far ends of the pacific.(Chile/Hawaii)
China/SouthEast Asia/ Japan to east Africa coast is a very short voyage, no shipping company will deploy Panamax on that route..
Ofcourse you know our main trading partners are in asia..Go figure
 
Bandari ya Mombasa lazima tu wahamishe hizo heavy Equipment maana mkakati wao wa Bomba la HOIMA umewafia mkononi,
Nadhan hiyo LAMU iko kwa ajili ya kupokea mahindi ya Rutto aliyolima Kongo ili kuwauzia wakunya
 
Unaandika upuuzi tu. Mbona post panamax zinatoka China zinafika Singapore na kushusha mizigo zitakazokuja East Africa? Distance kutoka China hadi Singapore ni ndogo sana. Wacha kujifanya mjuaji. Mbona meli kutoka Europe zinashusha mizigo zitazokuja E. Africa huko Oman? Distance kutoka Europe hadi Oman pia ni ndogo sana.
 
Hizo equipments zinazotoka Bandari ya Mombasa ni surplus equipments. Yaani extra equipments. Usidhani kwamba wanapeleka equipments ambazo bado wanazitumia.
 
Unaandika upuuzi tu. Mbona post panamax zinatoka China zinafika Singapore na kushusha mizigo zitakazokuja East Africa? Distance kutoka China hadi Singapore ni ndogo sana. Wacha kujifanya mjuaji. Mbona meli kutoka Europe zinashusha mizigo zitazokuja E. Africa huko Oman? Distance kutoka Europe hadi Oman pia ni ndogo sana.
1.Singapore is a global trade hub, you will find all manner of ships there

2. Those huge ships are expensive to run per mile than smaller ships. The volume of cargo to Lamu in global standards is a pittance.

3.Jubilee likes fellows like you and your ilk..Go figure
 
Back
Top Bottom