Kozi zenye fursa kubwa ya ajira na kujiajiri katika sekta ya Bahari

Watu kuwa wachache inamaanisha
1-kozi hailipi
2-qualification zake ni ngumu
3-uwepo wa ajira ni mdogo

So hebu tuambie zaidi juu ya ilo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kozi zinalipa Sana, hazitolewi hapa nchini, uwepo wa ajira mkubwa ndani na nje ya nchi. Pia gharama zipo juu kwenye kusoma.

Marine haina tofauti sana na Aviation, haina vigezo vikali kusoma shida ni ada zake.

Kozi yenye ugumu kusoma ni Marine Hydrographic survey hii kama umri umesogea usiende,huku ni hesabu haswa na mazoezi ya upimaji mara kwa mara ambayo hususisha hesabu nyingi.
 
Kozi zinalipa Sana, hazitolewi hapa nchini, uwepo wa ajira mkubwa ndani na nje ya nchi. Pia gharama zipo juu kwenye kusoma.

Marine haina tofauti sana na Aviation, haina vigezo vikali kusoma shida ni ada zake.

Kozi yenye ugumu kusoma ni Marine Hydrographic survey hii kama umri umesogea usiende,huku ni hesabu haswa na mazoezi ya upimaji mara kwa mara ambayo hususisha hesabu nyingi.
Unayosema ni kweli gharama zake si mchezo nimeangalia hii ya marine survey diploma yake inafika $4500.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unayosema ni kweli gharama zake si mchezo nimeangalia hii ya marine survey diploma yake inafika $4500.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama unapesa ukiwekeza kwenye hii, hao Lloyd Register jamaa ndio wanaongoza kuajiri duniani kwenye sekta ya marine. Kwanza utapewa Leseni yao hata ukiwa huku Tanzania ikitokea kazi wamepewa karibu na huku wao watakuunganisha.

Hata hivyo kazi moja ya survey mtu anachukua hela ndefu, kwa kubangaiza mtu akifanya bei ndogo ni million 2.
 
Hizi ni kozi ambazo mtu anaweza akasoma kuanzia ngazi ya Certificate,Diploma, Bachelor au Masters na akawa name fursa kubwa ya kupata kazi nchi yoyote na ni rahisi kujiajiri kwenye sekta ya bahari.

1.Marine Survey
Hii kozi ukisoma la kazi zako itakuwa ni kukagua meli kabla haijajengwa, Meli zinazofanya kazi na meli zote zinazoomba leseni za usajili.

2.Marine Cartographer
Hawa ni wachora ramani zinazotumika baharini,ziwani na mtoni katika uongozaji na kuonyesha vitu mbalimbali.

3.Marine Hydrograph Survey
Hawa kazi yao ni kupima kina kwenye maji ya bahari,ziwa na mito kisha kuandaa taarifa za eneo husika.

4.Marine accident investigation
Hawa kazi yao ni kufanya uchunguzi wa ajali za meli na kutoa ripoti za kitaalamu, kutoa mapendekezo ya namna ya kupunguza shaking baharini.

5.Maritime Law
Hii kozi mtu husomea sheria za bahari za kimataifa,mikataba kuhusu bahari name sheria kwa ujumla kuhusu biashara za bahari.

6.Port operation and Management
Hii kozi inahusisha shughuli zote za utoaji na upakiaji mizigo, utunzaji na usimamizi wa kazi za kila siku bandarini.

7.Port and Flag State Control
Mhusika atafanya kazi za ukaguzi wa meli za kigeni zijazo nchini, pia kwenye flag state control kazi zake itakuwa ni kusimamia zoezi la usajili wa meli na kuzifuta.

8.Ship Broker and Chartering
Hii kozi hutolewa na Lloyd's Register hawa ni waingereza wao watakufundisha kazi za ubroker(udalali) wa kukodisha,kuuza na meli za kukatwa screpa. Ukisoma kozi yao wao watakutafutia sehemu za uzoefu au kuwa chini ya mtu. Hawa jamaa wanapiga pesa sana endapo akiuza/kukodisha meli kamisheni lazima apewe kisheria na wengi wamejiajiri huko duniani utawakuta Singapore, London na Hongkong ndio maeneo yao.

9.Marine Technology Engineering
Hii kozi itakufanya ujifunze teknolojia katkia meli name shughuli zake kwa mifumo ya kisasa ya kompyuta.

10.Corrosion engineering
Hii ni kozi mpya imeanza miaka ya karibuni baada ya tatizo la kutu kwenye meli kuwa kubwa baharini. Waingereza wanatoa kozi hii ikilenga kuandaa mtu atakayetoa ushauri sahihi wa material zisizokuja pata kutu, uchanganyaji wa vyuma(alloy) na rangi sahihi za kutumika baharini zisizo leta athari kwenye maji.

11.Naval architecture
Hii kozi itamfundisha mtu kuchora michoro ya meli kwa kutumia kompyuta, ujenzi wa meli,material zinazotumika mpaka uimara na udhaifu wa meli itayojengwa.

12.Offshore Oil and Gas
Hii ni kozi zitazompa mtu mafunzo ya awali,kati na ubobezi kwenda kufanya kazi kwenye rig au platform za uchimbaji mafuta na gesi.

13.International Shiping and Logistics
Hii kozi mhusika atajifunza kuhusu biashara za kimataifa za usafirishaji shehena baharini.

14.Marine Insurance
Mtu atakayesoma kozi hii atajifunza namna ya bima za baharini na vyombo vyake zinavyofanya kazi, uthaminishaji wa meli na mali zake.

15.Marine renewable technology
Hii kozi mhusika atajifunza matumizi ya nishati ambazo ni rafiki kwa mazingira Kama jua,gesi,nuclear,mvuke kwenye kuendesha mitambo ya majini.

16.Marine Transportation
Hii kozi inampa mtu mafunzo ya kuongoza vyombo vya majini pia shughuli za bandari na masuala ya usafirishaji wa maji.

17.Marine Engineering
Hii kozi itamuandaa mtu kuwa injinia wa meli,na shughuli zote za mitambo ndani ya meli. Kufanya kazi kwenye mitambo mikubwa ya Diesel, uzalishaji umeme na kazi za makenika.

18.Marine electronics engineering
Hii ni kozi itayompa mtu mafunzo kwenye vifaa vya electronics kwenye Meli. Meli za kisasa zimekuwa na mifumo mingi ya umeme kuanzia vifaa vya kuongozea mpaka kwenye vyumba vya engine.

Angalizo: Kwa wale ambao wapo vizuri kiuchumi wakienda nje kusoma kwenye bara la Asia wawe makini waende kwenye vyuo vya Singapore,Japan na Korea ndio wapo vizuri hizo nchi nyingine watakuwa wameenda kubadili mazingira. Bora wabaki Africa kwenye Vyuo vya South Africa,Ghana na Egypt.

Katika Marine nchi ya uingereza ndio kinara kwa utoaji wa kozi hizo na vyuo vyao vinatambulika duniani. Pia nchi za ulaya nao wapo vizuri kwenye utoaji hizo kozi.

Kwa sasa unaweza ukasoma mtandaoni Lloyd's Register Institute,World Maritime University, Malta Maritime University wote wanatoa online course.

"SEA NEVER DRY".
Je naweza kusoma electro technical officer (ETO) baada ya diploma ya electrical engineering
 
Back
Top Bottom