Kozi gani nzuri sana ngazi ya cheti??..Msaada wa Mawazo haraka sana.

sasa wewe UZURI au UBAYA wa kozi unatumia vigezo gani kujua hivyo? maana mi sijakuelewa mara kozi nzuri mara nini...funguka unataka kozi yenye masomo mteremko au?
Wakuu Asante kwa Mawazo Mazuri.Vipi kuhusu Maendeleo ya jamii ni kozi nzuri?
 
kama upo tabora soma chuo cha ardhi kwa pass marks zako unaingia diploma 3 years land valuation ,then nafasi ya kupata kazi wizarani kwao ni rahisi sana sababu wanachukuliwa direct!au ata migodini wengi wapo huko!
 
watanzania lazima tuwe makini sana hususani ktk swala la elimu. Kabla hujasoma kozi yeyote lazima ujue kwa nini unasoma hyo kozi, nasikia uchungu sana kumsikia mtu aliyehitimu kidato cha sita hajui mustakabali wa maisha yake. Na hii inatokana na kusoma bila kuwa na vision. Si swala la kumkebehe mleta mada ila ni kumweleza ukweli kama hadi memaliza kdato cha sita hajui asome nini mustakabali wa maisha yake sio mzuri. Hapa utapata maoni mengi na unaweza ukafanyia kazi bila hata kujua ni nini ya unachokisoma, na ukipata ugumu mbele utashindwa kuendelea kwani ulichukua mawazo ya watu ukayafanyia maamuzi. Haiwezekani wewe hadi umri wako wa kuhtm kidato cha 6 hujui unataka kuwa nani! Kujua unachotaka ndio mwanzo wa kukipata na huwezi kukipata kama hujui ni kwa nini ni lazima ukipate. Hakuna kozi yeyote ya chuo kikuu haina certificate yake. Najaribu kufikiria kama uliyosema una maanisha. Maisha yako lazima uchague mwenyewe,vinginevyo!
Mtazamo wangu ni kwamba lazima ufanye kile kinachotoka ndani yako na una mapenzi ya dhati nacho.. Usije jaribu kusoma kwa sababu tu umeona watu waliosoma hyo fani wamefanikiwa.
Kaa chini fikiria juu ya ndoto zako kisha tafuta kozi zinazofanana na ndoto zako.
Kozi unayosoma lazima iwe kwenye ndto zako ili uweze kufanikiwa kimaisha na si vinginevyo. Ukisoma kozi iliyoko kwenye ndoto zako utafanikiwa hata kama wengine waliosoma hyo kozi hawafanikiwi.
Na niseme kwa uchungu kuwa vijana wengi wa kitanzania wamesoma kozi ambazo hazipo kwenye ndoto zao, na hii ni sababu mojawapo yao kuwa katika hali walizo nazo. Na hii imetokana na
1. Serikali kutoa ufadhilikwa vgezo ambavyo vitamlazimisha anayefadhiliwa kusoma kitu ambacho si ndoto zake.
2. Wazazi kuwalazimisha watoto wao wasome kozi wanazotaka wao wazazi.
Nimeandika pengine maneno magumu au ya ukali, ila ni kwa sababu mimi kama kijana sipendi tuwe na elimu lakini hiyo elimu isitusaidie katika kujikwamua kimaisha.

mkuu nashukuru kunifunza....nimepoteza dira kwa muda mrefu ndo mana nimeyumba.asante sana.
 
Asanteni Wote kwa Maelekezo Mazuri.NA THAMIN MICHANGO YENU NDIO MANA NIPO HAPA.NIMEAMUA KUSOMA KOZI YA COMMUNITY DEVELOPMENT AND SOCIAL WORK...MNAWEZA KUNISHAURI ZAID.Thanks to all Jf members
 
Asanteni Wote kwa Maelekezo Mazuri.NA THAMIN MICHANGO YENU NDIO MANA NIPO HAPA.NIMEAMUA KUSOMA KOZI YA COMMUNITY DEVELOPMENT AND SOCIAL WORK...MNAWEZA KUNISHAURI ZAID.Thanks to all Jf members

mbona unapoteza dira man?soma procurement kama ulivoshauriwa hapo juu!
 
Kozi gani nzuri kwa ngazi ya cheti?nilimaliza form six nikapata div 4 point 19 ya HKL.FORM 4 NILISOMA ARTS PURE NA KUPATA C-5 NA D-3.nimepiga vibarua nimepata hela ya ada hivyo nahitaji kujua kozi gani nzuri ngazi ya cheti.ambayo ina fursa ya ajira moja kwa moja?

Vision of wisdom yupo sahii fuata ushaur wake.....
 
Unapendelea nini zaidi?? Ni vizuri pia kusoma na kufanyia kazi kitu unachopendelea. Kozi zipo kibao, ajira zipo za kumwaga pia

Du ajira zipo za kumwaga wapi ndugu yangu,wewe CCM nini mliahidi ajira kibao sasa ziko wapi? Mbona juzi kwenye interview ya post moja ya IT Analyst post moja TANAPA tumepigana vikumbo watu 322, post ya IT System Admin GEPF tulipigana vikumbo watu 101 na kwenye post ya System Admin TANESCO applicants tulikuwa 276 post moja.Wewe hizo kazi za kumwaga umezitoa wapi.Ndugu mshauri tu asome kazi ni majaliwa ya Mungu
 
MDOGO WANGU NJOO KWANGU NITAKUPELEKA KUSOMA INDIA CHUO CHENYE HADHI NCHINI KWA BEI YA AU GHARAMA SAWA NA YA KUSOMEA HAPA NCHINI. kabetha@gmail.com
Mzee wa wisdom naomba tutafutane ili tuweke stratage ya kuelemisha vijana umuhimu wa career guidance na TALENTS IDENTIFICATION Ili watu wawe inspire to know what they know and have vision, In that regard somebody wanna know what to study and what to study,
 
wazo zuri hili,mkuu changamkia.
 
Du ajira zipo za kumwaga wapi ndugu yangu,wewe CCM nini mliahidi ajira kibao sasa ziko wapi? Mbona juzi kwenye interview ya post moja ya IT Analyst post moja TANAPA tumepigana vikumbo watu 322, post ya IT System Admin GEPF tulipigana vikumbo watu 101 na kwenye post ya System Admin TANESCO applicants tulikuwa 276 post moja.Wewe hizo kazi za kumwaga umezitoa wapi.Ndugu mshauri tu asome kazi ni majaliwa ya Mungu

It's who you know that matters, not what you know. Umenisoma?????
 
Back
Top Bottom