Kova unawafahamu Commando Yosso?

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,039
2,199
Kwa wale wenye kumbukumbu za miaka ya tisini mnaweza kukumbuka kikundi maarufu cha uhalifu jijini Dar.

Kundi hili lilikuwa ni hatari kwani liliweza kuvamia mitaa mbalimbali ya jijini Dar na kufanya uhalifu hasa hasa kuvunja majumba wakiwa kikosi.

Sikumbuki kundi hili lilidhibitiwa vipi lakini lilikuwa kundi hatari likiundwa na vijana wadogo sana.

Kuna timu ya yanga iliyowahi kufanya vizuri ilipewa jina la utani la Yanga Yosso kutokana na heka heka za kundi hili,mmoja wa wachezaji alikuwa ni Nonda shabaani papii ambaye baadaye alicheza ligi ya ufaransa.

Nashangaa kumuona kova anababaishwa na Mbwa mwitu/panya road kiasi cha kufikia kusimamisha ngoma za mchiriku ambao ni utamaduni wa watu wa pwani.

Kova pitia mafaili uone COMMANDO Yosso walidhibitiwa vipi.

Karibuni kwa wale mnaokumbuka mtupe habari zaidi za commando Yosso.
 
Ngoja waje ila hakika komandoo Yosso alifanya watu tutoke baa mapema maana hazikuwa za karibukaribu kama miaka hii.
 
kipindi cha commando yosso kova alikuwa dar cid kabla ya kwenda arusha kuwa rco kama kumbukumbu zangu xipo sahihi
 
Raia tulichoka na kuanza kusema nao kisela,tulikuwa tukitembea na mikokoteni nasi tunavamia nyumba za tunawaohisi wahuni na kuwapiga mpaka kufa na kuwapakiza katika mikokoteni na kwenda kuwakabidhisha kwenye kituo cha Polisi,hapo ndipo baadhi ya wahuni walipoona imeshakuwa soo na kuamua kukimbilia kusikojulikana na ndio ukawa mwisho wa MARA SALVATRUCHA hao.
Kamanda Kova acha kutunyima raha watu wa Pwani kwa kupiga makrufu ngoma zetu,malizana nao tu hao vijana.
Nalog off
 
komando yoso...! walivuma sana mwaka 1994! na walimalizwa kwa style ya kuwachoma moto! wananchi walichoka wakaamua kuchukua maamuzi mkononi...! ikawa wanakwenda kugonga nyumba moja moja wanauliza vizuri tu "mzee mwanao yupo? akitoka anapigwa tairi...!
 
kweli mkubwa!anatukosesha raha ya kiutamaduni.
 
komando yoso...! walivuma sana mwaka 1994! na walimalizwa kwa style ya kuwachoma moto! wananchi walichoka wakaamua kuchukua maamuzi mkononi...! ikawa wanakwenda kugonga nyumba moja moja wanauliza vizuri tu "mzee mwanao yupo? akitoka anapigwa tairi...!

Duh. Hio kali
 
kuna jamaa akilewa basi yeye hujiita komando yosso, kumbe komando yosso alikuwa hatarii.!
 
Jackbauer Kuzuia mchiriku ni sawa na kutoa amri ya "martial law" kwenye utamaduni wa watu husika!
 
Last edited by a moderator:
Jackbauer Kuzuia mchiriku ni sawa na kutoa amri ya "martial law" kwenye utamaduni wa watu husika!

Kova siku zote anatumia masaburi sana kwenye maamuzi, na ata mshauri wake ni shidah sana.

Atumi princple hii ya Jeshi (see, judge and act)

Yosso nakumbuka walinifanya kutoka baa mapema sana na wakumbuka sana, na walipotezwa na wananchi kwa kuwapiga mataili.
 
Last edited by a moderator:
Yosso walimalizwa kwa mtindo wa "mguu kwa mguu mpaka kwao alafu anafanywa barbique mbele ya jamaa zake"
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom