Kova: Tumewanasa viongozi wa 'Mbwamwitu'

kitkat

Member
May 23, 2014
16
0
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watu sita wanaodaiwa ni viongozi wa kundi la ‘Mbwa Mwitu' linalojihusisha na vitendo vya uvamizi na uporaji wa mali za watu kwenye nyumba na maduka jijini humo.


Kamanda wa Polisi kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kutokana na kukamatwa kwa viongozi hao na kupatikana kwa taarifa za makundi hayo jeshi lake litafanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa hadi wahusika wote wakamatwe.

"Hawa viongozi tunao, tumeshawahoji na wamekiri ni kweli wamekuwa wakijihusisha na vitendo hivyo kwa kutumia makundi yao," alisema Kova na kuongeza: "Sisi tunaanza kuwasaka hao vijana kwa sababu tumeshapata taarifa za kutosha kutoka kwa wenzao…tunafahamu wapi pa kuwapata."

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Athuman Said (20), Joseph Ponela na Clement Peter (25) wakazi wa Kigogo, Roma Vitus (37), Mwanshishe Adam(37) na Daniel Peter (25)wakazi wa Temeke.

Taarifa hiyo imekuja siku moja baada ya kusambaa kwa taarifa za kundi hilo la vijana zaidi ya 300 kuvamia mitaa mbalimbali ya jiji hilo, kupora mali na kujeruhi watu.

Kamishna Kova alisema kuwa jeshi lake lilifanikiwa kuwakamata viongozi hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema akisisitiza kwamba hatua inayofuata ni kuwasaka vijana wanaowatuma kufanya uhalifu huo.

"Hii itakuwa operesheni endelevu tunayoianza mwezi huu hadi mwezi Julai mpaka tuhakikishe tumewakamata wahalifu hawa na tatizo hili limetokomea,"alisema Kova kwa msisitizo.

Alisema jeshi lake limejipanga kukabiliana na wahalifu hao na kuwa wananchi waache kuwa na hofu kutokana na taarifa za uvumi zinazosambazwa kwenye mitandao kuhusu uhalifu unaofanywa na vijama hao.

"Ningependa kuwatoa hofu wananchi kuhusiana na uvumi unaoendelea kwenye mitandao…tunaomba wananchi wawe watulivu waendelee na shughuli zao kama kawaida. Jeshi langu limejipanga vizuri kuwadhibiti hao vijana. Hao vijana hawana uwezo wa kutushinda sisi" alisema Kova

Kamanda huyo aliweka wazi kuwa askari wa kutosha wa doria wameshapangwa maeneo ambayo yametajwa kuwa na mlipuko wa makundi hayo.Maeneo hayo ni pamoja na Kigogo, Manzese, Magomeni na Mbagala.


Chanzo:
Mwananchi

 

Attachments

  • kova.jpg
    File size
    23.5 KB
    Views
    5,877

Bahimba

JF-Expert Member
May 8, 2013
510
500
Wako wapi polis walio pola furushi la hela zilizo polwa na majambazi kutoka kwa mfanyabiashara pale kaliakoo?
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,950
2,000
Kova asipige siasa......haya matukio yakijirudia kwa uzembe wa Polisi itabidi yeye awajibike......taarifa za hawa wahuni zimekera wengi.......
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Kova asipige siasa......haya matukio yakijirudia kwa uzembe wa Polisi itabidi yeye awajibike......taarifa za hawa wahuni zimekera wengi.......
Kweli mkuu kova nadhani dar itamshinda sasa apishe wenye uwezo nayo wafanye kazi.
 

jojojo

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
926
500
Kweli mkuu kova nadhani dar itamshinda sasa apishe wenye uwezo nayo wafanye kazi.

Usiwe mnafiki unateteaga kila ubaya wa viongozi wako leo Kova kasema hilo ameshindwa kipi huku sirikali yenu yote imeshindwa teteaga tu. Huna haya
 

primking

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
647
225
maneno tu hayo hmna lolote kisa wametkanwa sana mitandaoni ndo kujifanya kutoa tamko
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,274
2,000
Talaka Rejea.... Bila aibu ukamnyang'anya Nguo mbele za Watu
Huku ukitoa kashfa Mbele ya Watu..akajifunze kwa wazazi wako

Leo Unamuambia arejee kwako...
Ulivyomtaliki umesahahu....


Nakuambia mimi Sikutaki tena oooh Siwezi.
Nakuambia mimi Sikutaki tena oooh Siwezi.

Shaaban Dede shahidi bwana, siwezi...
Gulumo Shahidi bwana, Siwezi...
Bitchuka kaka oooh oohh Dede Siwezi,
Bwana Ibrahimu oooh oooh Dede Siwezi,

nakuambia mimi sikutaki tena, siwezi...
Abeli Matata ooh Dede Siwezi...
Bitchuka oooh Dede Siwezi
Shaaban Dede oooh Dede Siwezi...


Nyimbo za Miaka ya 80s na 90s zilikuwa Poa sana kuliko hizi za Kova....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom