muhosni
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 1,108
- 152
Katika mahojiano na TBC radio saa 1.30 asubuhi leo akifafanua sababu za kuzuia maandamano ya waislamu kupinga uvamizi wa Libya. Mtangazaji akataka maoni yake kuhusu ongezeko la maandamano tz.
Amesema ongezeko la maandamano nchini linasababishwa na viongozi wengi wa serikali kutokuwajibika na kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika masuala ya jamii. Ametoa mfano kwamba kama Umeme umekatika watumiaji wana haki ya kupewa taarifa nini kimesababisha, nini kinafanyika na tatizo litaisha lini.
Kwamba wanayosema viongozi yawe ya kweli na yatokee kweli. Kama kuna mabadiliko wananchi wajulishwe na washirikishwe kutafuta ufumbuzi. Kwamba wananchi hawataandamana huku wakilijua tatizo kwa kina na wakiwa bize wakilitatua. Kwamba wananchi wakishirikishwa wana uwezo mkubwa wa kutatua matatizo kuliko hata viongozi