Kova: Krismasi, Mwaka mpya Disko toto marufuku

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,058
114,526
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amepiga marufuku disko toto na milipuko ya baruti katika kusherehekea sikukuu za krismass na mwaka mpya.

Kamanda Kova amesema hayo ikiwa zimebaki siku mbili kusherekea Sikukuu ya Krismasi na siku tisa kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa 2016 ambazo mara nyingi huwa na shamrashamra na mfululizo wa matukio ya hatari yanayotokana na namna mbaya ya usherehekaji.

Amesema kuwa, anawahakikishia usalama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa kusherehekea sikuu za maulidi, krismass na mwaka mpya hivyo wananchi wanatakiwa kusherehekea kwa amani sikukuu hizo.
Kamanda Kova amesema kuwa jeshi hilo litadhibiti wahalifu watakaotumia siku hizo kufanya matukio ya kihalifu na kudhuru watu bila ya sababu
 
Kupiga marufuku disco toto ni kuwanyima watoto wetu haki ya msingi ya kufurahia siku hii muhimu ya wakristo disco lingeruhusiwa ila wamiliki wa kumbi waambiwe wazingatie taratibu za kiusalama.
 
watoto washerehekee nyumbani au play centres za watoto...zipo nyingi tu..disko ni disko na hii dhana ya disko toto ni kivuli cha kukingia ujinga wanaofanya watoto kwenye hizo kumbi za disko...Safi kova...mwakani msiruhusu na ule ujinga wa after school bash.
 
Ni jambo jema,lkn hutakuwa hujawatendea haki hawa vijana wa kesho.disco toto huchezwa jion hasa ya watoto.nadhan kamanda kova hapo ungefikiria mara mbili kabla ya maamuzi hayo,ili hawa watoto wapate haki yao ya kucheza.
Naomba kuwasilisha kiroho safi.
 
Back
Top Bottom