Kova: Kelele Zenu Ni Bure, Ahmed Msangi Ni Mtu Safi. Lazima Aongoze Tume...

Hata kama Kova atalazimisha tume yake kuendelea na kazi lakini afahamu kwamba hatutakuwa na imani na ripoti yake hata kama watatumia lugha tamu kiasi gani kuielezea.
Msangi hakubaliki na haaminiki hivyo basi tume anayoiongoza haikubaliki na haiaminiki.
 
we kova acha wehu unaunda tume ya kuchunguza nini wakati dr keshasema timu yako na uwt mnahusika? acha kutuzuga bwana unapoteza fedha zetu bure huo mziki huuwezi uwezi kutoa jibu aacha nyamafu wee
 
we kova acha wehu unaunda tume ya kuchunguza nini wakati dr keshasema timu yako na uwt mnahusika? acha kutuzuga bwana unapoteza fedha zetu bure huo mziki huuwezi uwezi kutoa jibu aacha nyamafu wee

kova Tahi.ra
 
Ikumbukwe kuwa imewahi kuelezwa kuwa waliomteka Dr.Ulimboka walionekana kuwa "very skilled". Na kuna uvumi kuwa Dr. Ulimboka alimtambua Hemedi Msangi kama mmoja kati ya watekaji wake. Ikumbukwe kuwa kuna afisa wa Ikulu aliyetajwa na Dr. Ulimboka kuwa alikuwa akimpigia simu siku ya tukio na baadaye kuonana naye huko leaders club.

Dhana kuwa Kwa nini TISS imefanikisha mkakati wake wa kumlinda Hemed Msangi?inatokana na kuwa Hemed Msangi kuhusishwa na utekaji nyara wa Dr. Ulimboka wakati huo huo yeye akiwa afisa wa upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, hivyo kuna dhana kuwa crafters wa mkakati wa utekaji wa Dr. Ulimboka ni TISS ila watekelezaji ni polisi huku main character akiwa Hemed Msangi hivyo TISS inawajibika kumlinda Hemed Msangi.

Pia dhana kuwa afisa wa Ikulu aliyetajwa na Dr. Ulimboka, ikumbukwe kuwa Dr. Ulimboka alivyozungumza kupitia kituo kimoja cha Redio hapa nchini alisikia akisema kuwa alipigiwa simu na afisa wa Ikulu ili wazungumze njia za kumaliza mgomo wa Madakatari. Hivyo TISS inahusika na usalama wa Taifa na TISS inawajibika kwa Rais moja kwa moja, hivyo dhana kuwa TISS ndio crafters wa utekaji wa Dr. Ulimboka haiwezi kutiliwa shaka, pia ukumbuke kuwa anayedaiwa kuwa afisa wa Ikulu ndio huyo alitengeneza chambo kilichomtia Dr. Ulimboka mikononi mwa watekaji nyara.

TISS imefanikishaje? Kuna dhana kuwa ikitokea mpango wa kumteka Dr. Ulimboka umebumburuka basi zigo la utekaji wa Dr. Ulimboka liiangukie jeshi la polisi ili TISS ibaki salama na polisi waonekane ndio waovu, ndipo sasa dhana inakuja kuwa TISS wakatengeneza strategic characters, ikiwemo HEMEDI MSANGI, na aliyedai kuwa ni Afisa wa Ikulu.

Dhana kuwa TISS imetengeneza character aitwaye "Afisa wa Ikulu" ni akili ndogo sana, kuwa utekaji wa Dr. Ulimboka ukifanikishwa, ionekane kuwa ni vigumu afisa wa Ikulu ama ikulu yenyewe kuhusika na utekaji wa Dr. Ulimboka kwa kuwa kama wangetaka kufanya hivyo wasingetumia mtu aliyejitambulisha kama afisa wa ikulu kwa kuwa kufanya hivyo ni kuichongea ikulu kwa umma wa Watanzania. Kwa sababu wanaamini kuwa Watanzania ni wavivu wa kufikiria na wepesi kusahau mambo nyeti basi ionekane kuwa kama kweli ikulu ingehusika kumteka Dr. Ulimboka point hiyo ionekane haina mashiko kabisa. Hivyo ndivyo ilivyokuwa dhana nzima ya hawa crafters wa mkakati wa utekaji wa Dr. Ulimboka.

Dhana kuwa TISS imetengeneza character anayejiita Joshuo Gitu Muhindi, na kilichotajwa na kijana huyo kuwa kikundi cha watekaji nyara cha watu 12 kutoka Kenya ni janja ya crafters wa TISS kulimaliza suala la utekaji kupitia Mahakama. Walipokosea ni hapa hao crafters wa TISS kumtengeneza character huyo Mkenya Joshua aonekane kama mwendawazimu na kidogo anaakili Timamu. Kitendo cha huyo Mkenya kusema mbele ya jeshi la polisi na mbele ya walinzi wa kanisa la ufufuo na uzima wakati wakimhoji akasema kuwa yeye Joshua anatatizo la kuropokaropoka na hana akili timamu ni janja ya crafters wa TISS kuwachanganya Watanzania ambao wengi wao ni average thinkers endapo watasikia maneno hayo hivyo waendelee kuamini kuwa ni sahihi kwa Mkenya kufikishwa mahakamani kwa kuwa amekiri kuhusika na utekaji wa Dr. Ulimboka.

Kwa akili za kawaida mtu akiwa kichaa ama mwendawazimu hawezi kueleza kuwa yeye ni kichaa kwa kuwa ni asili ya binadamu kutotaka kuonyesha udhaifu wake hadharani.

Dhana kuwa crafters wa TISS wakimtumia Mkenya, na jeshi la polisi likampeleka mkenya mahakamani sasa jambo hilo lisiongelewe tena katika vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wa mahakama hivyo mpango wa kulinda Hemed Msangi utafanikiwa kwa kuwa sasa hakuna mbabe atakayethubutu kusema kuwa Hemed Msangi akamatwe na kuhojiwa?

Dhana ya TISS kulitumia kanisa la ufufuo na uzima kumpenyeza Mkenya ilionekana kugonga Mwamba baada ya Askofu Gwajima kukana kwa Mkenya Joshua hakwenda kwake kutubu na wala hakuna utaratibu wa watu kutubu kwake isipokuwa Mkenya aliishia kwenye mikono ya walinzi wa kanisa ambao baada ya kumhoji wakampeleka kituo cha polisi kawe. Dhana hii inaokana kama kuwa ni dhana ya dharura iliyotumiwa na TISS eti eeh? Kwa kuwa kama kweli craftrs wangekuwa makini wasingetumia kanisa hilo baada ya kujifunza kuwa kanisani hapo watu hawaendi kutubu kwa Mchungaji bali kila mmoja hutubu dhambi zake pale anapomkosea Mungu kwa imani hiyo Mungu akimsika humponya na dhambi zake zote. Ukweli huu unathibitika pale ambapo Askofu Gwajima alipokanusha mtu huyo kwenda kwake kutubu na kuelezea kuwa kama mkenya huyo angetaka kutubu si angeenda kwao Kenya?Muda wote huo tangu tukio litendeke mkenya huyo kwanini amebakia hapa nchini? Na pia Askofu Gwajima ambaye kwa kweli mimi namsifu kwa ujasiri wake wa kuishauri serikali/jeshi la polisi limkamate na kumhoji Hemed Msangi.

Lakini swali linalonitatiza ni jee, kwa kamanda Kova kusema kwa jambo hilo lipo Mahakamani na yeye hawezi kulizungumzia je haionekani kuwa njama za Kumlinda Hemedi Msangi zimefanikiwa? Na je nani jemedari atakeibuka tena na kusema Hemedi Msangi akamatwe na kuhojiwa?Mungu amlinde Dr. Ulimboka arejee akiwa hai ili ukweli ujulikane hata kama mchakato wa kumsulubisha mkenya mahakamani ikiharakishwa. Kwa kuwa ijulikane kuwa Mkenya akikiri kosa katika mahakama Kuu, atasomewa hukumu na akipelekwa jela, suala la Dr. Ulimboka ndio litakuwa limezikwa. Hapa suluhu ni Mkono Mungu umlinde Dr. Ulimboka
 
Hadithi ya kufikirika hii mpelekee Ray,JB, Wema au Hemed watengenezee muvi
 
hawakwepi hili scandal ,Dr Uli tunakungoja kwa hamu,nawe pia usije kubali kuoewa pesa yaishe maana hawa wanafanya lolote kuua soo ,
 
Unajua kamanda kova c mchapa kazi kweli kama anavyojinad bali ni mwepec kufanya kazi kupitia media yaan hata uongo yy lazima autangaze hayo ndyo yaliyompata kipindi hiki iga mfano kwa makamanda waliopita kama wakina tiba.punguza sifa kamanda
 
Safi sana Kova,we ndo unamjua vizur na mwenye uchungu na ulimbo.ka. We ni kamanda una haki ya kutesa watu,kutosikiliza wananchi au hata victims,una haki ya kupika ripot pia,kwa mamlaka yako unaweza pia ukapindisha ukweli wa mambo na kwa vile sisi ni watu wa amani,upendo na umoja tuko pamoja na wewe kwenye movie nzima.
 
Huyu D/SGT Gabriel niliwahi kukumbana naye Kituo cha Polisi Kawe. Ni mtu HATARI SANA huyu. Usiombe akukamate!
 
wamelala kama wanavyolala bungeni wale jamaa
sasa sijui nani akawaamshe
 
Back
Top Bottom