Kova/Jeshi la polisi laonya wanaoandaa Maandamano

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
04/11/2010

Kamanda wa kanda maalumu ya kipolisi ya mkoa wa Dar Es Salaam, Suleiman Kova amesema jeshi la polisi limepokea habari za siri kuwa kuna makundi ya watu wanaohamasisha wananchi kwa malipo ili wafanye maandamamo ya shari kufuatia matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutangazwa.

Kufuatia hali hiyo, Kova amewataka wananchi kujiepusha na mikusanyiko hiyo, vinginevyo jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote watakao shiriki vitendo hivyo.


source : TBChttp://www.wavuti.com/4/post/2010/1...onya-wanaoandaa-maandamano.html#ixzz14InRp2bn
 
Kova angalia sana Jk na shemeji yake(mwema) watakuponza,wewe zuia fujo na kamwe usijaribu kuzuia Watanzania kudai haki yao.
 
Kova angalia sana Jk na shemeji yake(mwema) watakuponza,wewe zuia fujo na kamwe usijaribu kuzuia Watanzania kudai haki yao.

ataangaliaje na wewe...! UNAVYOONA ANA MACHO YA KUONA KWANI..? mtizame vizuri..! anachoona ni SISIEM TUUU...! :A S angry::A S angry:
 
Ivi mikusanyiko Tz hata kama ina kibali hailuruhusiwi?
Kova vip bwanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Kama watakuwa wameruhusiwa kazi yako ni kuwalinda I guess
Alafu maandamano gani hayo watu wanalipwa?
Yangu macho
 
Huyu kova hana akili na yeye vile vile.yeye na hao CCM wote Was***ge tu...Eti watachukua hatu mbona sijawahi kuona hata siku moja CCM wakiandamana hawachukui sheria???Jaribuni kufanya hiyo kitu na sisi tupo tayari kumwaga damu...Haki yetu bado mnatudhulimu kama noma na iwe noma tu tumeshachoka tayari,Kama askari mnazidi milioni moja tanzania nzima haya basi tutaona tu......Bora nchi ichafuke tu..........Na tupo tayari kufanya hivyo!!!
 
Etii jeshi lipo tayari what the https://jamii.app/JFUserGuide???Watu tunauchungu ndio maana inabidi tuandike hivi.....
 
kwani kuandamana tatizo? sioni kama ni vibaya as long as watu wameomba ruhusa,sasa mtu anapotkea kuwatisha watu inaonekana kuna jambo linafichwa hapo...duh..
 
kwani kuandamana tatizo? Sioni kama ni vibaya as long as watu wameomba ruhusa,sasa mtu anapotkea kuwatisha watu inaonekana kuna jambo linafichwa hapo...duh..

tuache jazba, tutapigwa virungu na mabom ya machozi...
 
For the First Time In My Life Leo Nimeona SMG Brand new wamebeba Police Yaelekea Kuna Silaha zimeandaliwa Mahususi kwa Watakao kuwa na fujo
 
Back
Top Bottom