Kova acha Usanii; Utasemaje Mtu ni Wanted na Picha Umeificha?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,318
72,742
Kamanda Kova katangaza dau la Milioni 20 kwa atakaye wezesha kukamatwa mtuhumiwa wa Makontena 329 yaliyotoka katika ICD ya Azam Bw. abdulkarim Abdi aliyekuwa mkurugenzi wa Regional Cargo Service.
Cha ajabu kulingana na gazeti la Nipashe ni kuwa Kamanda Kova hajawahi hata siku moja kukabidhi picha ya mtuhumiwa huyo kwa vyombo vya habari ili watu wasiomfahamu wamuone na kumtambua zaidi ya kutaja kiwango cha fedha za zawadi.
Huu ni usanii wa aina yake ili kuonekana kuwa Jeshi la Polisi linalengo la kumkamata mshukiwa na linafanya juhudi wakati juhudi hizo ni hewa.
 
kawaida yake
Kwa hiyo kama ni kawaida yake maana yake katika hili hakuna kitu kinafanyika. Na ina maana kuwa hata huyo anayemtuma kumsaidia kutumbua hayo majipu bado hajui kuwa anafanyiwa usanii na mtu mzoefu?
Au hajali kwani naye anafanya usanii pia?
 
wasani wanajuana
 
Kuna Hii Picha Mbona ilisambaa Sana Kwamba Ndo Mtuhumiwa Wa Makontena.. Au ni Mm tu ndo niliiona
 
Attachments

  • 1451291337550.jpg
    1451291337550.jpg
    24.8 KB · Views: 134
Kuna Hii Picha Mbona ilisambaa Sana Kwamba Ndo Mtuhumiwa Wa Makontena.. Au ni Mm tu ndo niliiona
Hiyo picha ukiibandika atakayeonekana anatafutwa ni Kova maana ndio anaonekana kwa usahihi. Jeshi la Polisi wanao utaratibu wa kutoa picha na maelezo ya mtu Wanted. Mfano baada ya picha kunakuja maelezo, mfefu ft 5' 6' maji ya kunde, anakovu jembamba shingoni, akitembea anatingisha wowowo, macho meupe nk nk.
 
Kwa hiyo kama ni kawaida yake maana yake katika hili hakuna kitu kinafanyika. Na ina maana kuwa hata huyo anayemtuma kumsaidia kutumbua hayo majipu bado hajui kuwa anafanyiwa usanii na mtu mzoefu?
Au hajali kwani naye anafanya usanii pia?
Hata anayemtuma ni msanii pia,kwahiyo ni sehemu ya washiriki katika hii movie,wanajua wanachokifanya ni full usanii
 
Hiyo picha ukiibandika atakayeonekana anatafutwa ni Kova maana ndio anaonekana kwa usahihi. Jeshi la Polisi wanao utaratibu wa kutoa picha na maelezo ya mtu Wanted. Mfano baada ya picha kunakuja maelezo, mfefu ft 5' 6' maji ya kunde, anakovu jembamba shingoni, akitembea anatingisha wowowo, macho meupe nk nk.

Je Umefuatilia Utaratibu katika Jeshi la Polisi Ukakuta Hayo Mambo Hayapo?

Mi naona Hakuna Haja Ya Kulalamika Wakati hapo Alikuwa Anaonyesha Picha Na Wala Si Tangazo Kamili...

Huo Utaratibu Upo toka zamani.. hata Yule Jamaa Aliyemuua Padri zanzibar alitangazwa namna Hiyo na Baadae Akapatikana..
 
Kuna Hii Picha Mbona ilisambaa Sana Kwamba Ndo Mtuhumiwa Wa Makontena.. Au ni Mm tu ndo niliiona

Kwa hiyo hpo imetosha kwa akili yako kila mtu anaingia ktm mitandao hivi wangechapisha magazeti yote kwa siku hâta 5 ingekuwa rahisi mimi karibia nikalibebe liarabu moja kko yanafanana sana haya mawatu
 
Yule Jamaa Aliyemuua Padri Zanzibar Alitangazwaje na Alipatikananaje.. Mbona Mnapenda Kulalamika Kwa Kila Kitu

Tena Hata Hamkuona Picha Yake Halisi Ila Picha Iliyochorwa.. Msidhani kwamba Akitangazwa Hivyo basi Jeshi la Polisi Limekaa Pembeni Linasubiri Wananchi ndo Wamkamate..... Kama Unataka Info zaidi Nenda Kituo cha Polisi Utazipata Kama Ulishamuona Mtu anafanana Naye. Saidia Polisi si Kulalamika Humu
 
Je Umefuatilia Utaratibu katika Jeshi la Polisi Ukakuta Hayo Mambo Hayapo?

Mi naona Hakuna Haja Ya Kulalamika Wakati hapo Alikuwa Anaonyesha Picha Na Wala Si Tangazo Kamili...

Huo Utaratibu Upo toka zamani.. hata Yule Jamaa Aliyemuua Padri zanzibar alitangazwa namna Hiyo na Baadae Akapatikana..
Kwa hiyo katangaza dau la milioni 20 bila kuwepo tangazo kamili? Jee huyo mtuhumiwa kama kahamia huku Nanjilinji tutamjuaje sisi?
 
Hebu Tuwekee hicho Kipande cha Gazeti la Nipashe Ili twende Pamoja Kilichosema Hajapeleka Info kwenye Vyombo vya Habari
 
Usipende kutafuniwa kila kitu. Wewe umepewa source kuwa ni Nipashe, kama wewe unacho chombo cha habari kilichotoa picha halisi na maelezo ya huyo WANTED weka hapa kupinga habari hiyo. Au wewe unayejua wasifu wa mtuhumiwa kama ulivyotolewa na Kova (Polisi) tuwekee hapa.
 
ukute mtuhumiwa alishaenda "uarabuni" kitambo anakula bata huku akiperuzi jamiiforum na kucheka comment zetu hapa.
 
Hiyo picha ukiibandika atakayeonekana anatafutwa ni Kova maana ndio anaonekana kwa usahihi. Jeshi la Polisi wanao utaratibu wa kutoa picha na maelezo ya mtu Wanted. Mfano baada ya picha kunakuja maelezo, mfefu ft 5' 6' maji ya kunde, anakovu jembamba shingoni, akitembea anatingisha wowowo, macho meupe nk nk.
ahahaha,eti anatngisha nn?wowo?!
 
ukute mtuhumiwa alishaenda "uarabuni" kitambo anakula bata huku akiperuzi jamiiforum na kucheka comment zetu hapa.
Cheka na kisha anawapigia wakubwa simu kuwa wakuda wa JF wameanza kuhojihoji. Hakuna cha majibu wala mapunye hapa
 
Back
Top Bottom