Kosea vyote lakini sio kuoa au kuolewa. Najuta

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,839
17,437
Wanasema kosea vyote lakini sio kuoa au kuolewa.

Nipo kwenye ndoa nae mwaka wa sita huu lakini sasa ni mtihani mtupu. Mke wangu ana kiburi cha asili, gubu na wivu wa kijinga sana na kwenye ndoa tuna watoto watatu.

Hakuna anachokosa natimiza wajibu wangu kama mume, sijikwezi lakini ukweli mke wangu ni miongoni mwa wanawake walio kwenye ndoa wanaopata kila hitaji bila kusita au kucheleweshewa.

Lakini hataki kubadilika ana mambo ya kipumbavu kabisa hapa naandika nikiwa na hasira sana nitamuacha tu nioe mke mwingine kama mke wa pili.
 
Wanasema kosea vyote lakini sio kuoa au kuolewa

Nipo kwenye ndoa nae mwaka wa sita huu lakini sasa ni mtihani mtupu....
Kama umeshindwa kuvumilia udhaifu wake amini nakuambia utaoa kila mwaka na ipo siku utatamani umrudie hakuna mwanadamu asiye na kasoro, utakaye muoa atakuwa hana kiburi ila ni mzinzi, utamwacha utaoa mwingine asiye na kiburi Wala uzinzi ila ni mchoyo na mchafu, utamwacha utaoa mwingine hadi utakufa una msururu
 
Ulishawahi kukojoa palipoandikwa usikojoe hapa..? Halafu wameweka alama ya mkasi na mayai mawili!.

Sasa we endelea kusema kosea vyote! nyengine hizi ni siri za mtu binafsi mkuu lea familia yako kwa upendo sijaona kosa hapo hayo ni mambo mbalimbali tu, tuliokosea tumekaa kimya sio kwamba hatuna vya kusema.
 
Wanasema kosea vyote lakini sio kuoa au kuolewa

Nipo kwenye ndoa nae mwaka wa sita huu lakini sasa ni mtihani mtupu....
Mie mkuu amani yangu haipo kuwa na mke Bora Bali kuwa na utajiri.

Nimeoa Ila kuoa ama family sio priority kivile kwangu. Mana naona hata nikizaa naleta watt duniani kwenye dunia iliyojaa mihangaiko ya maisha mpaka kero.

Smt huwa sioni purpose ya kuishi. Sawa hela pata afu ni starehe tu nazo utachoka tu najua.

Utakula ,utatembea na kila binti wa kila rangi,utalala kila hotel nzuri unayojua Ila still you won't get satisfaction in life.

Yaani hata uwe na mke sijui Kama malaika Ila sidhani our happiness is being tied to external stuffs Mana huwa inaisha ndani ya mwaka tu.

Mfano ukinunua ndinga ya ndoto yako baada ya muda utaanza kuiona Kama ni kawaida nothing new.
Ukijenga ukaishi kwako baada ya muda unaona hakuna Cha Mana,

Ukiwa na mipesa hata mabilioni utaizunguka dunia yote utachoka Mana ukienda Kama majiji kadhaa baadaye hasahasa utapiga picha Kama show off Kama wewe ni dizaini iyo.

Ila still external things won't fulfill your purpose hapa duniani.

Hii kitu plz Kama Kuna mtaalamu naomba anisaidie.

Tunafuta pesa tukijua tutakua na furaha Ila bado tu ukizipata iyo furaha hutoiona.

Hasahasa utajenga nyumba na ukiwekamo vitu vya anasa huko ndani Ila later am sure utaiona Kama ni kawaida.

Utatembelea kila gari Ila still moyo utarudi utakuambia kuwa you're normal human being.

Ila still tunatafuta vitu tukidhani may be they'll satisfy our internal happiness and peace.
 
47 Reactions
Reply
Back
Top Bottom