Wadau hasa wale wa Chama chetu cha CCM, tukubali na tuseme ukweli Uchaguzi umeisha,kuna kitu kimoja kimetuharibia Uchaguzi huu na kuwaweka viongozi wakuu katika wakati mgumu, japo tunajikaza kisabuni.
Tukubaliane kuwa uchaguzi wa mwaka huu tumevuruga, kiukweli tumejipanga kimkakati kushinda uchaguzi na tulifanya matayarisho makuu ya kuwa tunaondoka na ushindi mnono, mbinu zetu zimefanikiwa na kweli tumeondoka na kilo nzito ya ushindi haijawahi kutokea,tokea mfumo wa vyama vingi uanze.
Kosa kubwa liliweka dosari ni kushindwa kudhibiti tusitoe kipigo na mbinu zetu kuweza kupita un-noticed,hili ni kosa ambalo kwa hali yeyote itabidi tulirekebishe,mbinu zetu zingeweza kutuvusha bila ya makelele ya milango.
Moja ya kosa ni kupiga watu au tuwaite wananchi au kwa lugha inayoendana na wakati wapiga kura,kuua wapiga kura,kuwacharaza kwa kutumia marungu waya na vitu kama hivyo, Polisi wametuharibia na kututilia doa ushindi wetu wa Tsunami.
Kwa kweli hatukufanikiwa kuupata ushindi huu bila ya kumwaga damu,athari ambayo ameondoka nayo Mkapa mtu aliejutia tendo hilo. Kwa ufupi kilichofanyika Unguja hasa Pemba kimeathiri ushindi wetu ndani ya nchi na hata kimataifa,hivi kulikuwa na haja gani ya kupiga watu au kurusha mabomu ndani ya nyumba kupitia dirishani,Je hawa tuliwatuma kuyafanya yote haya,unatia bomu dirishani ,tulihitaji yote haya ili tushinde?
Wadau tumekosea sana ,ilikuwa hatuna sababu ya kupiga hata bakora mtu mpiga kura yeyote zaidi ya kutumia maji ya washawasha na mabomu ya machozi yanayopigwa nje tena pale inapobidi kuwachawanya wapiga kura sugu, na ukienda kwenye waliopigwa risasi hili ndio jambo ambalo lilikuwa liepukwe kwa hali na mali ili kuisafisha njia ya ushindi, asingekuwepo mtu wa kulalamika zaidi ya kura zimeibiwa,jingine ni lile la kuwatupa wapiga kura tuliowakusanya kama ni waleta fujo, hawa tusingeliwapiga na baada ya uchaguzi tungewashusha chini ya milango ya nyumba zao,tungelisema tu tumewahifadhi kwa ajili ya usalama wao,ingelitosha kuongeza nguvu ya ushindi wetu.
Yaani kama ni kujisafisha ni kuwasaka wahuni waliofanya matendo haya japo halafu tuwaachie kwa mbinu zetu. Wadau uchaguzi ujao asikanyagwe hata mdudu, tupange mikakati yetu tuondoke na ushindi wa karne.