Kosa moja linaposahaulisha mazuri 100 uliyoyafanya: Mkasa uliomkuta Zamaradi


SniperBoi

SniperBoi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Messages
1,111
Likes
1,100
Points
280
SniperBoi

SniperBoi

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2016
1,111 1,100 280
Jumanne hii kwenye kipindi chake cha Take One, alirusha mahojiano na mwanaume anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja, tena aliyekubuhu na ambaye maisha hayo kwake ameyakubali na anayafurahia. Hicho kimekuwa kipindi controversial kuliko vyote vilivyowahi kurushwa Clouds TV.

Kuna sababu kadhaa kwanini wananchi wengi hawajapendezwa na kipindi hicho. Kubwa na muhimu kabisa, ni kuwa mjadala wa ushoga kwenye vyombo vyetu vya habari hasa redio na runinga bado inatia ukakasi mkubwa kwa wasikiliza/watazamaji. Kwa maadili na mila zetu, shoga ni mtu anayetia hata aibu kumuona akipita mtaani, seuze akihojiwa kwenye runinga ya taifa akijieleza kwa madaha anavyotembea na wanaume wenziwe, wa kila aina.

Mijadala ya ushoga kwenye redio na TV za Tanzania ni sawa na mtoto wa kiume kuongelea mapenzi na mama yake mzazi. Inakera masikioni, wanaudhi machoni na kwa kipindi kama kile kinachoruka saa tatu usiku, muda ambao familia nyingi zinakuwa zimekusanyika sebuleni baada ya chakula cha usiku ni aibu kubwa.

Ninaamini kuwa wengi walihamisha stesheni zao kuepuka fedheha ya kumuona mtu huyo akihojiwa kama si kutamani kujificha uvunguni kwa aibu.

Jambo la pili ni ‘timing’ ya kurushwa kwa kipindi hicho. Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa waislamu ni mwezi muhimu mno. Ni mwezi wanaoutumia kurekebisha mienendo yao, kutubu dhambi zao na kuwa karibu zaidi Mungu. Hivyo kwa kurushwa kipindi kama hicho katika mwezi huu, ilikuwa ni sawa na kukiwekea kidonda chumvi.

THE MEANS DOES NOT JUSTIFY THE END!

Dhumuni la Zamaradi kukirusha kipindi hicho lilikuwa zuri na muhimu mno. Hiyo ni tabia inayokera wengi na ongezeko la vitendo hivyo linatisha. Mtangazaji huyo aliandaa kipindi hicho kutaka kujua chimbuko lake. Kwa maelezo yake alidai muda wa kunyamazia tatizo hilo umepita na ni muda wa kulizungumza bila kificho.

Lakini wakati mwingine njia inayotumika haihalalishi nia njema. Ndio maana pamoja na Zamaradi kueleza kwa kina kwanini aliamua kumhoji jamaa huyo, bado watu hawamwelewi kwasababu ukweli ni kwamba muda wa kuiweka mijadala ya aina hiyo kwa Tanzania haujafika.

Bado ushoga ni kitu cha aibu kukisikia kikijadiliwa. Na jambo baya zaidi ni kuwa shoga huyo alipewa muda mwingi wa kujieleza na kuonesha ufahari wake. Kwake yeye, maisha hayo ni sawa na kwa wengi hiyo ndiyo ilikuwa tafsiri ya kipindi hicho – kwamba kiliuza zaidi dhana ya ushoga badala ya kuikemea kwa kumwalika mtu anayejutia kujiingiza kwenye tabia hiyo ili iwe funzo kwa jamii.

Mwanazuoni mmoja wa masuala ya habari ameandika:

Kwanza,nikili wazi kumualika shoga kwenye kipindi,kama tunavyoshuhudia wanaotumia madawa ya kulevya,si kosa, kosa unamualika aje kufanya nini? Unakwenda kumuuliza nini? Unataka peleka ujumbe gani? Kama unamualika kwa nia ya kuhakikisha anaeleza madhara ya anachokifanya,kwa nia ya kuonesha ubaya wa mchezo huu ili jamii ichukue tahadhari,hakuna shida.

Nimebahatika kukiona hicho kipindi kupitia mitandao ya kijamii,na kuona mapungufu yafuatayo.

1. Mtangazaji alimuachia muda mwingi mgeni wake kueleza jinsi anavyofurahia mazingira ya mchezo huo mchafu,alitumia mbinu dhaifu ya kufanya mahojiano (space interview) wakati kwa mazingira yale alitakiwa kutumia mbinu ya ‘shotgun.’ Tunatakiwa kutumia shotgun pale unapokuwa huna imani na mgeni wako, bahati mbaya Zamaradi aliacha kutumia mbinu hii akatumia ‘space interview’ matokeo yake mgeni akatumia mwanya huo kuharibu kipindi na kuharibu nia njema ya mtangazaji ambayo kwa jinsi nilivyomsikia,asubuhi alisema alilenga kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa kumnasua mtoto na hatari. Zamaradi alitakiwa kutumia shotgun ili kutompa nafasi ya kuupamba ushoga kama alivyofanya.

Nadhani mtangazaji hakutafakari kabla ni aina gani ya mahojiano anakwenda kuyafanya,siku zote aina ya mahojiano ndiyo huamua aina ya maswali na mbinu za kuuliza. Kama Zamaradi alilenga kuandaa kipindi kinachotaka kuhakikisha ushoga unapigwa vita na kutokomezwa, aina hiyo ya mahojiano huitwa CRITIC INTERVIEW. Aina hii ya mahojiano humtaka mtangazaji kuwa critical kwa mgeni wake na mada. Anatakiwa kumbana mgeni kwa kumuonesha ubaya wa anachokifanya.

ZAMARADI BADO NI MTANGAZAJI BORA WA TV

Maisha yana changamoto nyingi sana na wakati mwingine huja kwa kushtukiza kabisa. Leo hii Zamaradi anaandamwa kwa matusi na kejeli kwenye mitandao wa kijamii kwa kuteleza mara moja kwenye kitu ambacho alipanga kwa nia njema.

Wanasema vyombo vya habari ni ‘mbwa mlinzi’ ama watchdog – kwa maana kwamba hutumika pia kulinda masuala muhimu kwenye jamii. Zamaradi alitumia kipindi hicho kama njia moja wapo ya kutafuta suluhisho la janga hilo na jinsi ya kuwanusuru watoto wetu. Bahati mbaya njia aliyotumia imeleta mrejesho hasi, tofauti kabisa na matarajio yake, na tayari madhara yameonekana.

Zamaradi anafahamika kwa uwezo wake mkubwa katika tasnia hiyo na sisi ni mashahidi, kipindi cha Take One ni miongoni mwa vipindi bora kwenye TV. Juzi tu kabla ya hapo alimwalika Sheikh Kipozeo, ambaye licha ya visa vyake, alitoa mawaidha muhimu kwa waislamu katika mwezi huu wa Ramadhan. Tusimlaumu tu Zamaradi kuteleza mara moja, bali pia tumkumbuke na kumtetea kwa mazuri 100 aliyoyafanya.

TCRA ISITOE ADHABU KWA SHINIKIZO LA WANANCHI, BALI KWA KUZINGATIA NIA HALISI YA KIPINDI HICHO

Kupitia akaunti yake ya Twitter, mamlaka ya mawasiliano Tanzania imeandika: TCRA imepokea malalamiko Kuhusu kipindi kilichorushwa na Clouds TV cha Take1. Kamati ya Maudhui inalifanyia kazi na maamuzi yatatolewa.

Nafahamu kuwa mamlaka hiyo imepokea malalamiko mengi sana kuhusu kipindi hicho na naelewa kuwa ‘kutokujua kosa si kinga katika mambo ya sheria’ lakini ningeshauri ipitie shauri hili kwa kuzingatia nia halisi ya kurushwa kipindi hicho na kutohukumu kwa pressure ya wananchi na madhara yaliyotokea.

FUNZO

Sisi tuliopo kwenye tasnia ya habari tutambue kuwa hakuna mada bomu kama ya ushoga, tuiepuke kwa uwezo wetu wote na kama kuna ulazima wa kuiongelea basi tuwe makini sana.

Pole Zamaradi, hayo ndio machangu ya fani hii ya habari.
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
23,835
Likes
53,541
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
23,835 53,541 280
Hebu tupia picha ya huyo mtangazaji na huyo shoga ili tuweze kupata picha kwenye bongo zetu hao watu wawili ni wa aina gani
 
marwa job35

marwa job35

Member
Joined
Feb 21, 2016
Messages
35
Likes
15
Points
15
Age
49
marwa job35

marwa job35

Member
Joined Feb 21, 2016
35 15 15
Sho”""""""""""""duh!yani hata kulitaja naona kichefuchefu,kuhusu kuhojiwa it's right but itumike mbinu ya maswali yatakayoibomoa hii laana
 
M

mwayena

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2016
Messages
1,683
Likes
1,577
Points
280
M

mwayena

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2016
1,683 1,577 280
mjini wanaita kiki!!!ila usipotumia akili ya ziada!! kiki inakutokea puani mazima
 
Mugunga

Mugunga

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2016
Messages
642
Likes
884
Points
180
Age
46
Mugunga

Mugunga

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2016
642 884 180
Sho”""""""""""""duh!yani hata kulitaja naona kichefuchefu,kuhusu kuhojiwa it's right but itumike mbinu ya maswali yatakayoibomoa hii laana
Sidhani kama alikuwa na nia njema,kwa sababu angetumia weledi wake kudhibiti mwenendo wa mahojiano na mgeni wake.Sisi kama watazamaji tunabaki na chaguo moja tu,kuamini kuwa Zamaladi alilenga kutetea haki za mashoga.
 
K

kumbukumbu la torati

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2016
Messages
255
Likes
285
Points
80
K

kumbukumbu la torati

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2016
255 285 80
Duuuuh BWANA YESU ingilia kati na hili maana nalo jambo
 
bushland

bushland

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2015
Messages
6,578
Likes
4,312
Points
280
bushland

bushland

JF-Expert Member
Joined Mar 6, 2015
6,578 4,312 280
Kwaherini
 
mrsleo

mrsleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2014
Messages
1,883
Likes
1,244
Points
280
mrsleo

mrsleo

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2014
1,883 1,244 280
Kama nia ilikuwa ni kuelimisha jamii, kuna shoga mmoja nazani alishawahi kuhojiwa na hiyo hiyo clouds ila ni kwa upande wa radio, yule alikuwa ni shoga alieamua kuacha na aliongea kwa majuto na hali yakuelimisha jamii, kwahiyo kama nia ilikuwa ni kuelemisha jamii angemualika tena yule yule na sio kutuletea mtu aliekubuhu as if kaja kutangaza biashara
 
Utotole

Utotole

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
6,570
Likes
3,387
Points
280
Utotole

Utotole

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
6,570 3,387 280
Kasomea wapi huo utangazaji ninachojua clouds asilimia kubwa ni wadandia fani tu na kama unatoka na bosi utakula bata
Mleta mada amesema huyo mtangazaji ni mahiri na bora. Bahati mbaya kwenye mambo hayo niko nyuma kama mkia wa sungura.
 
K

KAMANDA MKUBWA

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
291
Likes
22
Points
35
K

KAMANDA MKUBWA

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
291 22 35
Shida ni kuwa utangazaji na uandishi hauna taaluma, watu wa mipasho , wachekeshaji , watukanaji wote wanaruhusiwa, huyo apewe adhabu kali, hakuna namna
 
Ficus

Ficus

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Messages
1,435
Likes
942
Points
280
Age
32
Ficus

Ficus

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2013
1,435 942 280
Watanzania tu wanafiki sana, mbona Zamaradi kaielezea vizuri tu nia ya kumuhoji mtu wa sample hiyo. Kukimbia tatizo sio njia ya kulitatua.
 
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
46,042
Likes
16,563
Points
280
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2012
46,042 16,563 280
TCRA wanapaswa kutoa adhabu kali kama ambavyo hufanya kwa vyombo vingine hakukuwa na uelimishaji kwenye habari ile zaidi ya utangazaji wa ushoga
 
N

niah

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Messages
4,978
Likes
5,652
Points
280
N

niah

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2015
4,978 5,652 280
Watanzania tu wanafiki sana, mbona Zamaradi kaielezea vizuri tu nia ya kumuhoji mtu wa sample hiyo. Kukimbia tatizo sio njia ya kulitatua.
Watu wajifunze kupitia huyo kijana ili wajue kuwa ni hormones corrupted na siyo wanapenda. Mbona mnawasikliza zeruzeru, watu wenye sehemu mbili?
 
N

niah

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Messages
4,978
Likes
5,652
Points
280
N

niah

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2015
4,978 5,652 280
Tunapokea misaada na mikopo toka kwenye serikali zinazotoza kodi toka mashoga kama uk, USA, EU na bado tunasema hatutaki kusikia mambo hayo. Baniani mbaya kiatu chake dawa!!!!
 
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2016
Messages
1,469
Likes
1,812
Points
280
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2016
1,469 1,812 280
Nimeshindwa kuisikiliza hata robo yake tu, nimejisikia vibaya sana
Ni upuuzi mkuu ambao hauwezi kusameheka, ..

Hakuna hata editors waliokipitia hiki kipindi kabla ya kwenda hewani na kuasses impact yake kwa public?
Huu ndo ujinga wa media house kuwa karibu na kujipendekeza kwa wakuu wa nchi na kuona kila wafanyalo lipo right.
 
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2016
Messages
1,469
Likes
1,812
Points
280
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2016
1,469 1,812 280
Watanzania tu wanafiki sana, mbona Zamaradi kaielezea vizuri tu nia ya kumuhoji mtu wa sample hiyo. Kukimbia tatizo sio njia ya kulitatua.
Inategemea na tatizo.
 
maneka

maneka

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
363
Likes
249
Points
60
maneka

maneka

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
363 249 60
Umefafanua vema, ila nia yako ya kumsafisha Zamaradi nachelea kusema kuwa huenda wewe ni team zamaradi na unajua makusudi halisi ya mjadala wa kueneza ushoga. Isingekuwa hivyo usingeshauri vyombo husika visimchukulie hatua. Fumbo mfumbie mjinga.....
 

Forum statistics

Threads 1,262,527
Members 485,585
Posts 30,124,904