MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,562
Wadau habarini?.........
Kuna usemi wa kingereza usemao The more mistakes one makes in life, the smarter one gets in life ------ I ask if it s applicablle in mapenzi na mahusiano..............
Source: The Hill of Wealth
Kwenye mapenzi na mahusiano makosa mengi huendelea kujirudia kila leo, wapo wanawake/wanaume ambao tumejikuta kila tunapotafuta wapenzi huangukia kwa wanaume/wanawake ambao huishia kututesa na kutuumiza kwa style ile ile.
Mbaya zaidi ni pale ambapo tumeona wanandoa ambao wametoka familia zenye tatizo (wazazi kupigana, kuachana nk) nao wamejikuta kuwa na ndoa za aina hiyo hiyo.
Ingawa we
ngi tunaamini kwamba mahusiano yanapoenda vibaya yanaweza kusaidia kufungua macho ya muhusika ili siku akimpata mpenzi mpya aweze kujifunza na kutorudia kosa lilelile. Au kama ni mtoto atokaye katika familia yenye majeraha basi atatoka na mafunzo flani ambayo yatamfanya naye ayaepuke katika familia yake mpya.
Swali : Ni kwa nini inakuwa hivi?
Je ni kutokuwa makini? au kudanganyika na kitu mapenzi au ni nini hasa....................naombeni msaada wenu