Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela aliandika kitabu chake cha kwanza akielezea maisha yake tangu akiwa wakili hadi alipotoka gerezani kiitwacho A long walk to freedom. Waliokisoma watakubaliana na hoja yangu ninayoijenga hapa.
Mandela anaeleza kwamba alipokuwa gerezani kisiwani Robin vuguvugu mle jela lilikuwa likiendelea na ilifika mahala wafungwa walikuwa wakikubaliana ni aina gani ya mgomo wataufanya.
Mara nyingi walikuwa wanaishia kugoma kula (hunger strike). Lakini Mandela anaeleza kuwa binafsi hakuwa anaipenda migomo ya kula. Hivyo kila lilipoletwa wazo la kugoma kula Mandela alikuwa kwenye upande wa waliopinga wazo lile na mara zote ilibidi wafikie muafaka kwa kupiga kura. Kwamba tugome kula au tusigome.
Mandela anaeleza kuwa siku zote wenye wazo la kugoma kula walishinda kwa wingi wa kura.
Hadi hapa hakuna tofauti na CHADEMA kupiga kura kugomea hotuba ya Rais Kikwete yaani Walkout. Pia hakuna tofauti ya Zitto Kabwe na Mandela hadi hapa. Mandela hakupenda hunger strike wakati Zitto hakupenda Walkout. Kina Mandela walishindwa maoni yao kwa kura kama Zitto na wenzake walivyoshindwa juzijuzi.
Sasa tuone utekelezaje wa maamuzi ya upigaji kura kati ya Zitto Kabwe na Nelson Mandela.
Mandela anaeleza kwamba japo hakuunga mkono wazo la hunger strike lakini baada ya matokeo ya kura yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kusimamia kugoma.
Na anaeleza kuwa kama msimamizi mgomo unapofika siku ya tatu alitegemea kuona ndoo za vinyeshi ziwe kavu lakini anashangaa kuona zikiwa na vinyesi vya hapa na pale kwa maana ya kwamba kuna watu walikuwa wanachomoka kimyakimya na kujificha na kwenda kula kwa kushindwa kuvuilia njaa.
Anaieleza hii kama kichekekesho lakini Mandela anaeleza jinsi ambavyo wagomaji walitakiwa kuonyesha umoja mara tu baada ya matokea ya kura. Kwamba hata kama bado kuna watu walitoroka kwenda kura lakini walifanya kwa siri sana na hadi anaandika kitabu hakuwajua.
Mandela anatufundisha nini? Anatufundisha kwamba haia haja ya kupiga kura kama wote mna wazo moja mnalotaka litumike. Ila kama kila mmoja ana wazo lake kinachofuta ni kujadiliana na kupima sababu na hasara za kila wazo.
Yakishindikana yote basi hamuwezi kupoteza muda mkijadiliana wakati uamuzi unatakiwa ufikiwe. Ndipo hapo mnaposema hoja zenu wote ni safi lakini kwa vile tumeshindwa kutoa uamuzi kwa njia ya ushawishi na maoni basi kura ndiyo iwe uamuzi utakaoheshimiwa.
Hata kwenye soka tena ya watoto wadogo tunaelewa kuwa inawezekana timu ikapenda kuanzia mechi kwenye goli la kusini labda kwa sababu siku hiyo upepo unawasaidia kutokea kusini. Kama timu pinzani haioni shinda kuanzia kaskazini basi hakuna sababu ya kupiga kura kwa kurusha shilingi.
Lakini kama wote Timu A na Timu B wanagombania golila kuanzia basi wanaweka rehani maamuzi yao kwenye matokeo ya kura. Kwamba watafuata matokeo ya kura ili kuamua cha kufanya yaani kuannzia wapi. Ndipo hapo kura inapigwa kwa kurusha shilingi. Hapa hakuna cha kur kulingana. Lazima shilingi itatoa maamuzi. Ama Timu A itashinda kwa kuanzia kusini ama Timu B.
Baada ya kupigwa kura kama walivyofanya kina Mandela au kurushwa shilingi zilivyofanya zile timu hakuna majadiliano mapya tena. Kugomea uamuzi wa kura ni sawa na kugomea maamuzi yaliyokubaliwa.
Ndiyo maana Mandela analifafanua hili kwamba japo yeye siku zote amepinga kwa hoja na kura kwamba hapendi hunger strike lakini pamoja na kushindwa amekuwa akiwa kinara wa kusimamia mgomo. Mandela anaonyesha nidhamu ya maamuzi. Alishindwa kupinga mgomo kwa ushawishi wa hoja, kisha akashindwa kwa kura hakuwa na jinsi kuukata uamuzi wa walio wengi.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Nelson Mandela, shujaa anayeheshimika duniani kote. Je, ndivyo ilivyokuwa kwa Zitto Kabwe? Wote tumejua sivyo.
Kwanza bila Zitto tusingejua maamuzi yale yalifikiwa vipi. Hivyo Zitto katusaidia kujua kuwa yalifikiwa kwa kupiga kura. Kumbe demokrasi waliyotumia kina Mandela mle gerezani ndiyo demokrasia waliyotumia CHADEMA.
Siungani na wanaolaumu Zitto kwa kutoa siri ya kilichofanyika kwani kwa katufunulia walipiga kura katuonyesha kwamba CHADEMA ni chama makini kinachoheshimu maoni ya watu na si kuendeshwa na udikteta.
Sasa baada ya kupiga kura ilitakiwa kufanya nini? Hapa Zitto anatofautiana na Mandela. Mwenzake Mandela aliamua kuwa kiongozi wa mgomo lakini Zitto hafanyi kama Mandela. Zitto alipiga kura lakini hafanyi kulingana na matokeo ya kura. Zitto anasahau kuwa kama kundi lake lingeshinda CHADEMA wangefanya kama alivyotaka yeye. Sijui napo angeenda BBC na kusema kuwa CHADEMA haikugoma kwa sababu waliokataa mgomo walikuwa wengi?
Mandela anawafundisha watu kama Zitto kwamba maamuzi yoyote yaheshimiwe maadamu hayajafikiwa kwa njia ya udikteta.
Zitto hata kama tunampenda vipi lakini mbele ya kadamnasi katuonyesha kuwa ana utovu wa nidhamu ya maamuzi. Kukataa maamuzi ni utovu wa nidhamu. Utovu ambao Mandela hautaka kuushiriki hata kama hakupenda la walio wengi.
Zitto angesema kwamba hakupiga kura kabisa, mimi nigekuwa wa kwanza kumuelewa na kumtetea. Hata mtoto wa darasa la tatu anajua nini cha kufanya baada ya matokeo ya kura. TUmecheza michezo mingi utotoni inayohusisha kupiga kura. Leo umepiga kura, wenzako wengi wamesema wanataka kugoma. Matokeo yanatoka badala ya kuyaheshimu wewe unafanya unavyotaka na unanungunika. Hivi neno utovu wa nidhamu litumike kwa vitendo gani kama si hivi!
Kama CHADEMA au Zitto mwenyewe wana mpango wa kuuwajibisha utovu huu wa nidhamu basi huu ndiyo wakati muafaka ikiwa bado mapema na wengi wakiwa nalo kichwani. Ni kweli kunaweza kuwa na mgawanyiko lakini kazi ya kuelewesha itakuchukua muda na watu wataelewa polepole wale wasiotaka kuelewa mapema. Mkisubiri utovu huu muushughulikie zaidi ya 2012 au 2013 wakati uchaguzi wa 2015 umekaribia basi mgawanyiko unaweza kuingia hadi wakati wa uchaguzi na ikala kwenu.
Linalowezekana leo lisingoje kesho.