Kosa la Lowassa lilikuwa kubwa kuliko la Pinda?

Je unaelewa kwanini Pinda aliteuliwa kuwa WM?

1. Kwasababu hakujipambanua ktk kambi yoyote kati ya zile zilizokuwa zinasigana yaani kambi ya EL na kambi ya Six.
2. Alionekana kuwa ni mtu asiye na meno(Kibogoyo), Hivyo hawezi kuathiri interest za wakubwa.
3. Alionekana hana athari kwa aliye juu yake (kiongozi wa nchi) kama vile EL alivyokuwa anamfunika JK.
 
Tatizo la nchi hii ni Rais na wala siyo mawaziri. Tanzania mwaka wa 8 huu unaisha bila kuwa na Rais. Ila tunastahili pongezi kwa kuweza kukaa miaka mingi hii bila Rais na still tunadunda tu

Post of the day!!
 
Mh.Pinda anastahili pia kama hawa kina Mathayo, Nchimbi na Nahodha pia Kagaesheki kwani imeonekana namna ambavyo wizara nyingi zimekuwa zikisuwasuwa chini ya uongozi wake yeye kama msimamizi wa shughuli zote za Serikali.
 
Hao ni mashetani wawili tofauti! moja jizi jingine zembe.teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh...
 
kama ni suala la political responsibility Pinda naye ilibidi ajiuzuru. Mbona Kagasheki hajahusika moja kwa moja na amejiuzuru?

Umesahau kauli yake kwamba kwamba mkiwakamata majangili mmalizane huko huko!
 
Hii ni kauli iliyotolewa leo bungeni moja kwa moja na mmoja wa Wabunge waliochangia mjadala wa leo kuhusu janga la oparesheni tokomeza!..... najaribu kushangaa na pia najikuta nashangaa zaidi ya kushangaa kumuona mh. Waziri mkuu pamoja na "MATUSI"yooooote ambayo amekuwa akitukanwa live na kauli za dhihaka na kebehi anazotolewa kila leo, kwanini anakuwa mgumu kuwajibika? ipi ni sababu ya msingi inayomfanya asiwajibike? CCM CCM CCM, Mshaurini huyu mtu apumzike kujilindia hadhi yake japo kwa mkewe!!
 
Tatizo la nchi hii ni Rais na wala siyo mawaziri. Tanzania mwaka wa 8 huu unaisha bila kuwa na Rais. Ila tunastahili pongezi kwa kuweza kukaa miaka mingi hii bila Rais na still tunadunda tu

Mkuu umeua kabisa kweli watz tunawza kujiongoza miaka 8 bila Rais si mchezo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hivi kosa la Lowassa na la Pinda lipi ni kubwa?

Kama Lowassa aliwajibika kwa makosa ya walio chini yake,ni kwanini Pinda analindwa?

Hivi kashifa ya Richmond na hii ya mauji,utesaji na udhalilishaji wa raia ni ipi liyo mbaya zaidi?

Hivi inatosha tu kuwawajibisha mawaziri bila waziri mkuu?

Je,huyu Raisi wetu ni mtu seriuos kweli na matatizo ya nchi hii?

Wadau,hapa si bure bali kuna jambo!

Lowassa kama dalali. Aliwahi kula mkataba wa mvua za kutengeza kwa mabomu wakati nchi kame kama Algeria hata hawafanyi hilo. Bora upigwe na poronium kuliko kuruhusu Lowassa aingie ikulu. Tutaingia porini kuokoa nchi. Hata maccm msipoamini lakini ukweli ndo huo, kwanza tutahakikisha hafanyi compaign.
 
Hii ni kauli iliyotolewa leo bungeni moja kwa moja na mmoja wa Wabunge waliochangia mjadala wa leo kuhusu janga la oparesheni tokomeza!..... najaribu kushangaa na pia najikuta nashangaa zaidi ya kushangaa kumuona mh. Waziri mkuu pamoja na "MATUSI"yooooote ambayo amekuwa akitukanwa live na kauli za dhihaka na kebehi anazotolewa kila leo, kwanini anakuwa mgumu kuwajibika? ipi ni sababu ya msingi inayomfanya asiwajibike? CCM CCM CCM, Mshaurini huyu mtu apumzike kujilindia hadhi yake japo kwa mkewe!!

hajajiuzulu amefukuzwa, you cannot wait until you are about to be fired then resign. there was no policy difference but performance reasons so he has been fired. he was confronted for low performance and forced out
 
Hiyo ranchi kaikamata leo! hao wafugaji wameharibu walikokuwa ndio maana wanahangaika now, pia sio kila penye majani basi ngombe wakae acha chuki binafsi
Ufugaji wa ranchi ndio unaotakiwa sio watu wanageuza nchi nzima eneo lao la kuchunga mifugo na kuwadhulumu wakulima haki yao.
 
Pinda alitakiwa awe wa kwanza kuachia madaraka iwe mfano kwa mawaziri waliotajwa kua mizigo maana suala mauaji tena ndani ya nchi ni fedheha kubwa naamini ya Pinda na makubwa kuliko ya Lowassa
 
Hivi kosa la Lowassa na la Pinda lipi ni kubwa?

Kama Lowassa aliwajibika kwa makosa ya walio chini yake,ni kwanini Pinda analindwa?

Hivi kashifa ya Richmond na hii ya mauji,utesaji na udhalilishaji wa raia ni ipi liyo mbaya zaidi?

Hivi inatosha tu kuwawajibisha mawaziri bila waziri mkuu?

Je,huyu Raisi wetu ni mtu seriuos kweli na matatizo ya nchi hii?

Wadau,hapa si bure bali kuna jambo!

hapana. lowassa aliwajibika kwa makosa yake. alikuwa anaandika vimemo mwenyewe kushinikiza richmond ipewe tenda.
 
El amekamata ranchi ekari 9000 tanga, wafugaji wanahangaika kutafuta malisho? Pinda amekamata ranchi wapi? You can't compare the two
yaaa pinda hakuwa na zengwe na mtu yeyote ila kagasheki ndiyo alikuwa kawakalia watu vibaya , vile vile lowasa naye alipigwa zengwe sana na sitta na ndiyo maana akachomoka mapema .mheshimiwa pinda mkakati wa kutochomoka ulishasetiwa mapema na wabunge wa CCM , na wao wakaahidi basi mawaziri watoke kama mnataka kumnusuru waziri mkuu , na ndiyo maana sikuona sababu ya makinda kuumwakia machali wakati anaongea huku anataka kugawa form za kumkataa waziri mkuu , makinda alikuja juu wakati alitakiwa amuache tu amalize muda wake na kama form angezigawa tu, kwa utaratibu anaoujua machali, lakini kwa kuwa upepo ulikuwa unaharibika spika anna makinda akuchelea kujionyesha uhalisia wake kwa pinda
 
labda hujuhi lakini naamini unajua ila unajifanya umesahahu,
1. Issue ya RICHMOND alisimamia yeye kama waziri mkuu akishirikiana na IKULU na kama utakumbuka ilisemwa ilikuwa Raisi aende sema Mwakyembe walificha ficha wakaamua Lowassa ajitoe kafara.

2. Hili la sasa lilisimamiwa na wizara zenyewe na halijawahi kuwa chini ya waziri Mkuu.
So kama alivyosema Mwanasheria mkuu KILA MTU NA LWAKE.

WAZIRI MKUU anahusika Moja kwa moja na UTESAJI NA MAUWAJI ya raia kwa kauli yake aliyoitoa ndani ya Bunge Kuwa raia 'wapigwe tu'na askari hata kabla ya kufikishwa mahakamani.Kijeshi tamko la waziri mkuu ni AMRI na tutegemee maafa zaidi kwani pamoja na kujifanya amesikitishwa na yaliyotokea bado hajatoa tamko la kubatilisha kauli yake ya kipigo.Masikini WABUNGE wengi walimpigia MAKOFI bila kujua madhara ya Ushabiki wa vyama na ndio maana wanaona aibu kumwambia ukweli.
 
Oja yako ni ya msingi sn muheshimiwa, kwa hakika hii nchi hatuna viongozi, ispokuwa tuna vilaza watupu! We watanzania tumefikia hatua tunaishi kama tuko fafur! Hii nchi ni ya kwetu sote sema kuna watu tumewapa tu dhamana ya uongozi kwa kuwa wote hatuwezi kuwa viongozi, hivyo mti akiona km dhamana tuliyompa haiwezi bas atoke akaangalie mambo mengine huko mbele kwa mbele kuliko kutuletea upuuzi hapa, laiti km jakaya akilifumbia macho na hili, kutakuwa na walakin tu! Kwa hakika pinda na watu wake wa chin wajiuzulu tu"!!!!!
 
Kikubwa kinachomsumbua ni njaa, maana c anajiita mtoto wa mkulima! Na kwa hapa ilipofikia inatisha ( mkulima kala mbegu......)
 
Back
Top Bottom